Baadhi ya wakazi wakiwa katika Banda la Mkoa wa Tanga wakati wa maadhimisho ya 16 ya Wiki ya Vijana ambayo Kitaifa inafanyikia mkoani Dodoma. Maadhimisho ya Wiki ya Vijana uratibiwa na kusimamiwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo chini ya Idara ya Maendeleo ya Vijana ambapo maadhimisho ya mwaka huu ni ya 16 tokea kuasisiwa kwake.
Picha na: Frank Shija, WHVUM
Mabanda yamaonyesho yanayotumiwa na wadau mbamlimbali wa maendeleo ya vijana katika katika maadhimisho ya 16 ya Wiki ya Vijana ambayo Kitaifa inafanyikia mkoani Dodoma na maonyesho hayo yatazinduliwa rasmi tarehe 10 (kesho) na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Kapteni Chiku Galawa katika viwanja vya Barafu mjini Dodoma. Maonyesho hayo yatahitimishwa sambamba na madhimisho ya Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Hayati. Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Watoto wa Halaiki wakiwa katika maandalizi ya lala salama tayari kwa sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru kama walivyokutwa na mpiga picha wetu leo katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.Kilele cha mbio za Mwenge waUhuru kitaifa zitafanyika tarehe 14 Oktoba mkoani hapo.
No comments:
Post a Comment