Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akimkaribisha Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili eneo la Rahaleo Mjini Mtwara Oktoba 10, 2015.ili kuweka jiwe la msingi katika mradi wa nyumba za makazi na biashara unajengwa na NHC.
Sehemu ya majengo ya mradi wa nyumba za makazi na biashara unaojengwa na NHC eneo la Rahaleo Mjini Mtwara unavyoonekana sasa.Mrdai huu uliwekewa jiwe la m,singi na Mhe. Rais wa Tanzania jana.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angela Jasmin Kairuki akitoa maelezo ya namna Wizara inavyosaidia sekta ya nyumba na kumkaribisha Mhe. Rais kuzungumza na wananchi waliofika eneo la Rahaleo kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi kwenye nyumba za makazi na biashara zinazojengwa na NHC.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Kikwete akitoa hotuba alipoenda kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa nyumba za makazi na biashara unaotekelezwa na NHC eneo la Rahaleo Mjini Mtwara.
Sehemu ya umati wa wananchi waliofika eneo la Rahaleo Mjini Mtwara kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la nyumba za makazi na biashara zinazojengwa na NHC uliofanywa na Mhe. Rais Jakaya Kikwete.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akitoa maelezo kwa Mhe. Rais Kikwete ya mradi wa nyumba za makazi na biashara unaojengwa na NHC eneo la Rahaleo Mjini Mtwara.
Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa nyumba za makazi na biashara unaojengwa na NHC eneo la Rahaleo Mjini Mtwara.
Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC Bw. Haikamen Mlekio akitoa maelezo ya michoro ya mradi wa Rahaleo kwa Mheshimiwa Rais mara baada ya kuuwekea jiwe la msingi.
Mheshimiwa Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wafanyakazi wa sekta ya ardhi wa kanda ya kusini muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye nyumba za makazi na biashara zinazojengwa na NHC eneo la Rahaleo- Mtwara.
Mheshimiwa Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa NHC muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa nyumba wa Rahaleo Mjini Mtwara.
Mheshimiwa Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kampuni ya CRJE ya China ambao ndiyo wakandarasi wa mradi wa nyumba za NHC zinazojengwa eneo la Rahaleo-Mtwara. Mradi huu utakuwa na Hoteli ya kisasa na nyumba za makazi 96 ambazo zitauzwa kwa wananchi.
Wafanyakazi wa NHC wa Mtwara na Lindi wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu Bw. Nehemia Mchechu(mwenye suti) na Viongozi wa Menejimenti mara baada ya kufanikisha sherehe za Mheshimiwa Rais kuweka jiwe la msingi katika mradi wa nyumba wa Rahaleo.
No comments:
Post a Comment