Friday, October 09, 2015

MAADHIMISHO YA MIAKA 70 YA UMOJA WA MATAIFA NCHINI TANZANIA KUFANYIKA DAR ES SALAAM

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maandalizi ya sherehe za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa pamoja na kutolea ufafanuzi malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs) yenye lengo la kufuta kabisa umaskini.(Picha zote ne Geofrey Adroph wa Pamoja Blog).
DSC_0181Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maadhimisho ya kuundwa kwa Umoja wa Mataifa yatakayofanyika siku ya Jumanne Tarehe 13, Oktoba katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez.
Baadhi ya Maofisa wa Umoja wa Mataifa na maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiendelea kufuatilia yanayojiri kwenye mkutanoni na waandishi wa habari.
Waandishi wa habari wakifuatilia kinachoendelea mkutanoni.
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kulia) wakiwa wameshikilia lengo namba 1 na 13 kati ya malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.
Mwanafunzi wa shule ya msingi ya Agha Khan, Iman Kawambwa akiwa ameshikilia lengo namba 4 kati ya malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...