Monday, June 02, 2014

Wafanyakazi wa Airtel watoa msaada hospitali ya Ocean Road



Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Diva’, Amitin Mbamba (kulia), akikabidhi msaada wa machela za kisasa mbili, ‘wheel chair’ mbili na bidhaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya milioni 5/-, kwa Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Mary Haule, kwaajili ya matumizi ya wagongwa katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni wanachama wa Airtel Diva.

Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Diva’, Amitin Mbamba (kulia), akikabidhi msaada wa moja kati ya ‘wheel chair’ mbili, machela za kisasa mbili na bidhaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya milioni 5/-, kwa Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Mary Haule, kwaajili ya matumizi ya wagongwa katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni wanachama wa Airtel Diva.
Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Mary Haule (kulia) akiwaongoza wanachama wa kikundi cha wafanyakazi wanawake wa Airtel Tanzania ‘Airtel Diva’, wakati walipotembelea wagonjwa wa taasisi hiyo, baada ya kukabidhi msaada wa machela za kisasa mbili, ‘wheel chair’ mbili na bidhaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya milioni 5/-, kwaajili ya matumizi ya wagongwa katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Wanachama wa kikundi cha wafanyakazi wanawake wa Airtel Tanzania ‘Airtel Diva’, wakiwa wamebeba bidhaa mbalimbali, walipotembelea wagonjwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) na kukabidhi msaada wa machela za kisasa mbili, wheel chair mbili vyenye thamani ya zaidi ya milioni 5/-, kwaajili ya matumizi ya wagongwa katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Wakibadilishana mawazo na Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Mary Haule.
Picha ya pamoja baada ya kukabidhi vifaa hivyo.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia umoja wa wanawake ujulikanao kama Airtel Divas umetoa msaada wa vifaa vya hospitali kwaajili ya wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa ya saratani katika hospitali ya Ocean road jijini Dar es salaam

Msaada huu unafatia harambee kwa ajili ya kuchangisha pesa iliyofanywa na Airtel Diva mwezi uliopita kwaajili ya kupata fedha za kuwasaidia wagojwa wanaosumbuliwa na magonjwa ya kansa katika hospitali ya Ocean Road.

Akiongea wakati wa kutoa msaada huo mwenyekiti wa Airtel Divas Amitin Mbamba alisema” Tunatambua na tunapokea kwa machungu matatizo yanatowapata wanawake na watoto wanaougua saratani na katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani kwa mwaka 2014 tuliamua kuchangisha pesa kwaajili yakutuwezesha kununua vifaa vya hospitali na kuwasaidia wanawake na watoto  pamoja na wagonjwa wengine hospitalini hapa. Na leo tunayofuraha kutoa stretcher 2 pamoja na wheelchair 2 zenye thamani ya shilingi million 5 hospitalini hapa.”

Tunaamini msaada huu utawawezesha wahudumu kupata nyenzo muhimu na kuweza kufanya kazi yao ya kutoa huduma kwa wagojwa kwa ufanisi zaidi.

“Nia yetu ni kuhakikisha tunaendelea kutoa muda wetu na rasilimali katika kushikiri na kuchangia shughuli za huduma kwa jaimii ili kukubailiana na matatizo yanayoikumba jamii inayotuzunguka hususani wanawake wenzetu” aliongeza Mbamba

Mmoja ya wajumbe wa Airtel Divas Bi Deliphina Martin Msuya alisema” tunayofuraha kuwa sehemu ya kutoa msaada kwani tunatambua umuhimu wa wanawake katika kusimamia familia,  inagusa sana kuona jinsi gani wanawake wenzetu wanavyougua au kuuguza watoto wao hospitalini hapa hivyo tunatoa wito kwa wanawake wengine huku nje mmoja mmoja au kwa makundi kuwasaidia wanawake wenzetu walio katika changamoto hizi kwani ni jukumu letu kusaidia wahitaji.

Akiongea mara ya kupokea msaada huo Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Mary Haule alisema” Hospitali yetu inaupungufu wa vifaa mbalimbali zinavyotuwezesha kuhudumia wagonjwa tunashukuru sana Airtel kwa msaada wao na kwa kuwezesha kupata hivi vifaa kwani vitatusaidia katika kutoa huduma na kuongeza ufanisi wa kazi zetu za kusaidia wagonjwa hapa hospitalini. Nachukua nafasi hii kuwaomba makampuni mengine na vikundi mbalimbali kusaidia changamoto zingine zilizopo hospitalini hapa.

Airtel Divas ni mpango ulioanzishwa Airtel Afrika nzima wenye lengo la kuwahamashisha na kuwawezesha wanawake wanaotoka katika makuzi , mila na tamaduni mbalimbali kujiamini na kufanikiwa katika maisha , mpango huu ulizindulia Airtel Tanzania March 2012.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...