Tuesday, June 17, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT.GHARIB BILAL AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA RAIS WA BOLIVIA, EVO MORALES,AHUDHURIA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA NCHI ZA G77

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokewa na wenyeji wake wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Bolivia juzi Juni 13, 2014 kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya Nchi za G 77 na China, yanayofanyika jana Juni 15, 2014, jijini Santa Cruz, Bolivia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Meya wa Jiji la Santa Cruz,  Percy Fernandez, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Bolivia juzi Juni 13, 2014 kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya Nchi za G 77 na China, yanayofanyika jana Juni 15, 2014, jijini Santa Cruz, Bolivia. Kushoto ni Mama Zakhia Bilal.
 Makamu wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiagana na Mwenyeji wake Rais Evo Morales, Rais wa Bolivia baada ya kufanya mazungumzo saa chache kabla ya kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 50 ya nchi za G77 na China yanayofanyika jijini Santa Cruz, Bolivia. Katika mazungumzo hayo Rais Morales aliishukuru Tanzania kushiriki katika maadhimisho haya na akasisitiza kuwa uhusiano wa nchi za G77 unapaswa kuenziwa huku Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal akifafanua kuwa Tanzania ni inatambua na kuheshimu jitihada zinazofanywa na umoja huo na kwamba ni kipindi kizuri kuadhimisha miaka 50 kwa kutafakari kuhusu kutanua fursa za kukuza uchumi ili kuendeleza wananchi wa nchi hizo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Rais wa Bolivia, Evo Morales, walipokutana kabla ya kuhudhuria maadhimisho ya Miaka 50 ya nchi za G77 na China yanayofanyika jijini Santa Cruz, Bolivia, Juni 14, 2014. Katikati ni Mkalimani wa Rais wa Bolivia. Katika mazungumzo hayo Rais Morales aliishukuru Tanzania kushiriki katika maadhimisho haya na akasisitiza kuwa uhusiano wa nchi za G77 unapaswa kuenziwa huku Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal akifafanua kuwa Tanzania inatambua na kuheshimu jitihada zinazofanywa na umoja huo na kwamba ni kipindi kizuri kuadhimisha miaka 50 kwa kutafakari kuhusu kutanua fursa za kukuza uchumi ili kuendeleza wananchi wa nchi hizo.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...