Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Maagi akizungumza wakati wa makabidhiano ya nyumba 40 ambazo zimenunuliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT)
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Maagi akizungumza wakati wa makabidhiano ya nyumba 40 ambazo zimenunuliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT)
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Maagi akimkabidhi hati ya Umiliki wa Nyumba Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Uendeshaji wa BoT, Leonard Kisarika wakati wa makabidhiano ya nyumba 40 ambazo zimenunuliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT)

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Maagi akimkabidhi funguo za mojawapo ya nyumba Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Uendeshaji wa BoT, Leonard Kisarika wakati wa makabidhiano ya nyumba 40 ambazo zimenunuliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT)

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Uendeshaji wa BoT, Leonard Kisarika akifungua mlango wa nyumba mojawapo wakati wa makabidhiano ya nyumba 40 ambazo zimenunuliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT)
Jumatano (Juni 11, 2014) Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Maagi alikabidhi nyumba 40 ambazo zimenunuliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Makabidhiano hayo yalifanyika mjini Dodoma kwenye eneo la Medeli Manispaa ya Dodoma. Nyumba hizo zina thamani ya Sh bilioni 4.8 kwa wastani wa Sh milioni 117 kwa kila nyumba.
Maagi alisema NHC imejenga nyumba zenye viwango ambavyo BoT walivihitaji na makubaliano ya ujenzi huo yalifanyika Jumanne (Juni 10,2014) na wahandisi wa BoT walipata fursa ya kuangalia wakati ujenzi unaendelea.
Alisema unaponunua nyumba NHC unapata kwa ubora na ukubwa mteja anaouhitaji na kunapunguza gharama kwani unalipa kwa awamu wakati ujenzi unapoendelea.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Uendeshaji wa BoT, Leonard Kisarika alisema walifikia uamuzi wa kujenga nyumba Dodoma kutokana na kuwa na harakati za kufungua ofisi mkoani Dodoma.
“BoT iko kwenye mradi wa kujenga ofisi Dodoma lakini tukapewa changamoto na bodi kuwa hatuwezi kufungua ofisi bila kuwa na nyumba za kukaa wafanyakazi na katika harakati tukapata mpango wa ujenzi wa nyumba eneo la Medeli tukafuatilia na kuingia nao mkataba,” alisema.
Kwa upande wake, Meneja Usimamizi wa Miradi wa NHC, Haikamen Mlekio alisema mradi mzima una nyumba 150 na Benki Kuu wameweza kununua nyumba 40 ambazo ni za kisasa.
Pia alisema eneo hilo lina huduma mbalimbali ikiwemo maduka na saluni ili kupunguza usumbufu kwa wakazi wa nyumba hizo kwenda umbali mrefu kutafuta huduma hizo. mwisho
Kabla ya tukio hilo Jumanne (Juni 10, 2014) Shirika la
Nyumba la Taifa kupitia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bwana Felix Maagi, lilitiliana
saini na Halmashauri mpya ya Wilaya ya Busokelo iliyowakilishwa na Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpya Busokelo, Meckson Moses Mwakipunga pamoja na
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Saidi Mderu. mkataba wa ujenzi wa nyumba 14 za bei
nafuu kwa shilingi bilioni 1.2 ikianzia na malipo ya Sh milioni 500 katika
hafla iliyofanyika Hoteli ya New Dodoma.
Makabidhiano hayo yalishuhudiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, (Kazi Maalum), Profesa Mark Mwandosya na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Aggrey Mwanri, Waziri wa
Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe, Mbunge wa Rungwe Magharibi, Profesa David
Mwakyusa, Mbunge wa viti maalumu, Dk Mary Mwanjelwa, Mbunge wa Ileje Nikusuma
Aliko Kibona, Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa na Naomi Kaihula Mbunge wa
Viti maalumu.
Mradi huo unatarajiwa kuanza Julai 2014, na unategemewa
kukamilika Agosti 2015 ikiwa ni muda wa takribani mwaka. Mradi huu una nyumba
za gharama nafuu 14 tu zitakazouzwa kwa Halmashauri ya wilaya ya Busokelo,
zikiwa ni nyumba za vyumba vitatu vya kulala, sebule, jiko la kisasa na
maegesho ya magari ya ziada. Mradi huu utagharimu kiasi cha shilingi
1,112,109,880 ikiwa ni wastani wa shilingi milioni 79 kwa kila nyumba.
No comments:
Post a Comment