Tuesday, June 24, 2014

CHINA NA TANZANIA ZAZINDUA UJENZI WA JENGO LA TAASISI YA MWALIMU NYERERE JIJINI DSM

Picha na 1Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao (wa pili kushoto) akiwa  na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (katikati), akiwasili eneo litakapojengwa jengo la Taasisi ya wa Mwalimu Nyerere karibu na bandari jijini Dar es salaam.Picha na 2Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao (kushoto) na Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (kulia) kwa pamoja wakizindua jiwe la msingi katika eneo litakapojengwa jengo la Taasisi ya  Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.Picha na 3Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao (katikati) na Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (wa pili kulia) kwa pamoja wakizindua wakimwaga mchanga kuashiria kuanza kwa ujenzi jengo la Taasisi ya  Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.Kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania Lu Youqing.Picha na 5Mama Maria Nyerere (kushoto) akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa jengo la Taasisi ya  Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
Picha na 6Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye (kulia) kuhusu picha ya mfano ya mwonekano wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere pindi litakapokamilika.Picha na 7Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamini Mkapa (kushoto) na Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF).Picha na 8Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao (wa pili kushoto) akisalimiana na Mama Maria Nyerere mara baada ya hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF) jijini Dar es salaam wakishuhudiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.Picha na 9Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao ( kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda, Mama Maria Nyerere, Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi na Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa.Picha na 10Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao ( kushoto) akisalimiana na aliyekuwa Rais wa Bunge la Afrika, Balozi  Getrude Mongella wakati wa hafla ya uzinduzi wa jingo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.Picha na 11Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi (Kulia) na Mama Maria Nyerere wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere.pPicha na 4
Viongozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam. Kutoka kushoto ni Mama Maria Nyerere, Rais Mstaafu wa Wawamu ya tatu, Benjamini Mkapa,Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...