Friday, June 20, 2014

DARAJA LA TABATA KINYEREZI, LAKATIKA BAADA YA MZEMBE MWENYE SEMI TRAILER KUPITA

Semi-Trela likiwa limebeba kontena likiwa limeanguka baada ya kulielemea  kwa uzito na kulivunja daraja la chuma katika barabara ya Banana-Kinyerezi maeneo ya Tabata jijini Dar es salaam jana jioni. 
Haikuweza kufahamika mara moja lilikuwa limebeba mzigo gani na kama dereva alikuwa anajua daraja hilo ni kwa magari yenye uzito wa wastani  wa tani 7 tu au ni kiburi tu.  Hakika Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli  na jeshi lake wana kazi ya ziada kuhakikisha uzembe kama huu hautokei na haujirudii.…
Semi-Trela likiwa limebeba kontena likiwa limeanguka baada ya kulielemea  kwa uzito na kulivunja daraja la chuma katika barabara ya Banana-Kinyerezi maeneo ya Tabata jijini Dar es salaam jana jioni. Haikuweza kufahamika mara moja lilikuwa limebeba mzigo gani na kama dereva alikuwa anajua daraja hilo ni kwa magari yenye uzito wa wastani  wa tani 7 tu au ni kiburi tu.  Hakika Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli  na jeshi lake wana kazi ya ziada kuhakikisha uzembe kama huu hautokei na haujirudii. 

Mawasiliano ya barabara yamekatika na kusababisha wakazi wa Tabata Kinyerezi kutafuta njia mbadala kutokana na gari kubwa la mizigo kuvunja daraja la muda lililowekwa wakati ujenzi wa daraja kuu ukitegemewa kuanza.

Gari hilo (Pichani) lililokuwa linatoka njia panda Segerea kuelekea Tabata Kinyerezi ilikuwa limebeba kontena lenye mzigo mzito huku likipita katika daraja hilo la chuma. Daraja hilo lilishindwa kuhimili uzito huo na kusababisha kuvunjika na gari hilo kudondokea katika mto Msimbazi.

Kutokana na hali hiyo wakazi Tabata Kinyerezi wanalazimika kupita Tabata Segerea na Tabata Barakuda.

Daraja hilo jipya la mchepuko limebomolewa kabisa na lori kubwa ambalo akili ya kawaida inasema daraja hilo lisingeweza kuhimili uzito huo.

Kwamba mwenye gari na dereva wake wameamua kupitisha gari hilo zito kwa makusudi, huo ni uhujumu uchumi.
PICHA ZA : http://immamatukio.blogspot.com/

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...