Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe akiwa Mbele ya Kaburi la Mama yake mzazi Bi
Shida Salum muda mfupi baada ya kuzikwa jana kwenye makaburi ya Rubengela mjini Kigoma
Umati wa wananchi wa mkoa kigoma na viongozi kutoka mikoa mbalimbali wakielekea makaburini tayari kwa mazishi ya Shida Salum Mama mzazi wa mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe.
Wananchi waliohudhuria mazishi ya shida Salum Mama yake Mzazi Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu huyo wakielekea makaburi ya Rubengela mjini Kigoma kwa mazishi.
Mbunge wa Rombo(CHADEMA), Mhe. Joseph Selasini(Kulia)Mbunge wa Kigoma Mjini-CCM Peter Serukamba(wa pili Kushoto)wakiwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini-Chadema Zitto Kabwe (katikati)wakielekea kwenye mazishi ya mama Mzazi wa Mheshimiwa Zitto kabwe bi Shida Salum mjini Kigoma
Mbunge wa Kuteuliwa na Rais James Mbatia(wa tatu kushoto)akijadilia jambo na mwenyekiti wa Chama cha wananchi(CUF)Profesa ibrahim Lipumba wa tatu kushotokwenye mazishi ya mama Mzazi wa Mheshimiwa Zitto kabwe bi Shida Salum mjini Kigoma Jana

Baadhi ya Wabunge wakiwa katika msiba wa mama mzazi wa Mbunge mwenzao Zizzto Kabwe (wapili kushoto aliyefuatana na baba yake Zuberi Kabwe) mjini Kigoma na Juu ni Kaburi alipo zikwa mama mzazi wa Zitto Kabwe.
No comments:
Post a Comment