Monday, June 30, 2014

Kampuni ya Green Waste Pro Ltd yaadhimisha sherehe ya kutimiza miaka miwili katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa‏‎

1
Mkurugenzi wa Green WastePro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo akizungumza jambo kwenye sherehe ya kutimiza miaka miwili kwa kampuni hii ya kufanya usafi katika jiji la Dar es salaam hususani kwenye manispaa ya Ilala.2
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Kheri Kessy akizungumza jambo kwenye sherehe ya maadhimisho ya miaka miwili ya Kampuni ya Green WastePro Ltd kwenye ukumbi wa makumbusho siku ijumaa tarehe 27, 2014.
3

Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Kheri Kessy akizungumza jambo kwenye sherehe ya maadhimisho ya miaka miwili ya Kampuni ya Green WastePro Ltd kushoto ni Mkurugenzi wa Green WastePro Ltd bwana Mark Anthony Shayo na kulia ni afisa Mazingira katika manispaa ya Ilala Mr. Mapunda.4

Ndg. Said Mazingira wa Kampuni ya Green WastrePro Ltd, akisoma risala kwa mgeni rasmi.5

Mkurugenzi wa Green WastePro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo akizungumza jambo na mgeni rasmi Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Kheri Kessy.
6
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Kheri Kessy akimkabidhi cheti mfanyakazi wa Green WastePro Ltd Bi. Anna Emili kama mfanyakazi bora

7

Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Kheri Kessy akimkabidhi cheti mfanyakazi wa Green WastePro Ltd, Bi. Mwajabu Said kama mfanyakazi bora.
8
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Kheri Kessy akimkabidhi cheti mfanyakazi wa Green WastePro Ltd, Bi. Sia Ulio kama mfanyakazi bora.
9
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Kessy akimkabidhi cheti mfanyakazi wa Green WastePro Ltd Bi. Fatma Salehe kama mfanyakazi bora.
10
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Kessy akimkabidhi cheti mfanyakazi wa Green WastePro Ltd, Ndg. Hamza Saidi kama mfanyakazi bora

11

Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Kessy akimkabidhi cheti mfanyakazi wa Green WastePro Ltd Bi. Hassan Juma kama mfanyakazi bora
12
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Kessy akimkabidhi cheti mfanyakazi wa Green WastePro Ltd, Ndg. Kelvin Jonas kama mfanyakazi bora

13

Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Kessy akimkabidhi cheti mfanyakazi wa Green WastePro Ltd, Ndg. Sudi Juma kama mfanyakazi bora

.14
Mh. Kessy akimkabidhi cheti mfanyakazi wa Green WastePro Ltd, Ndg. Salum Juma kama mfanyakazi bora.15
Mh. Kessy akimkabidhi cheti mfanyakazi wa Green WastePro Ltd, Bi. Marry Baraka kama mfanyakazi bora.16

Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Kessy akimkabidhi cheti mfanyakazi wa Green WastePro Ltd, Bi. Carolina Ilomo kama mfanyakazi bora.

16a
Wafanyakazi wakimsikiliza mgeni rasmi.16b
Ulifika muda wa kufungua Shampeni kwa ajili ya kusherekea miaka miwili ya Green WastePro Ltd.16c
Wafanyakazi wakapa kuonja kidogo Shampeni.17 
Picha ya Pamoja kati ya Mh Naibu meya na Mkurugenzi Mkuu wa Waste Pro Ltd.
18
Wafanyakazi wa Waste Pro Ltd wkipata picha ya pamoja na mgeni rasmi.

EVANS AVEVA RAIS SIMBA

10Matokeo yametangaza na Evance Aveva amechaguliwa kuwa rais mpya wa klabu ya Simba ya jijini Dar es salaam huku Makamu wa rais akichaguliwa Bw. Godfrey Nyange Kaburu matokeo ya uchaguzi huo yametangazwa jana alfajiri naidadi kamili ya kura walizopata tutawapatia baada ya muda, Kwa upande wa kamati ya utendaji waliochaguliwa ni Idd Kajuna, Coliins Friesh, Ally Suru na Saild Tully kwa upande wa mwanamke ni Jasmin.

Rais Jakaya Kikwete Alipokutana na Wataalamu Watatu wa Utafiti wa Chanjo ya Malaria Kutoka Ifakara Health Institute Mjini Malabo, Equatorial Guinea

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Dr Ally Olot, mtafiti wa chanjo ya malaria na kiongozi wa watafiti wa Ifakara Health Institute (IH) I Malabo, Equatorial Guinea) walipomtembelea kwenye makazi yake mjini Malabo ambako Rais alikuwa anahudhuria mkutano wa kawaida wa Umoja wa Afrika. Wengine ni Dr. Mwajuma Chemba ambaye ni Mtalaamu mratibu wa tafiti za chanjo ya malaria, na Elizabeth Nyakarungu, Mtaalamu wa maabara, utambuzi wadudu wa malaria
 Rais Kikwete aliwapongeza sana watafiti hao pamoja na taasisi ya IHI kwa kuiletea sifa Tanzania katika fani ya utafiti nje ya nchi.

Watafiti hao wako Equatorial Guinea (EG) kwa mwaliko wa serikali ya nchi hiyo kwa ajili ya kutoa msaada wa kitaalamu katika utekelezaji wa mradi wa utafiti wa chanjo ya malaria iitwayo PfSPZ na kuwafunza wenzetu kuhusu maarifa ya fani hii ya utafiti wa chanjo ya malaria. IHI ni shirika la utafiti lenye kufanya tafiti za afya nchini Tanzania lenye uzoefu wa miaka zaidi ya miaka hamsini. Mfano mmoja wa mafanikio yake ni utafiti uliopelekea vyandarua vyenye dawa kutumika kama moja wapo ya njia za kujikinga na malaria nchini Tanzania.

SHEREHE ZA KUAGA WASTAAFU WA JESHI LA MAGEREZA MKOANI MWANZA ZAFANA JIJINI MWANZA


  Aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoani Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Mstaafu, Raphael Mollel akitoa nasaha zake kwa niaba ya Wastaafu wote wa Jeshi la Magereza Mkoani Mwanza katika sherehe za kuwaaga Wastaafu wa Magereza Mkoani Mwanza.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa hotuba fupi kwa Maofisa wa Jeshi la Magereza na Wageni Waalikwa (hawapo pichani) katika Sherehe za kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza Mkoani Mwanza.
  Wageni Waalikwa katika sherehe za kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza Mkoani Mwanza wakitosi vinywaji na Meza Kuu kama inavyoonekana katika picha.
  Meza Kuu katika sherehe za kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza Mkoani Mwanza (katikati) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja ambaye pia ndiye aliyekuwa Mgeni rasmi katika sherehe hizo zilizofana katika Ukumbi wa Gereza Kuu Butimba, Mwanza.
  Maafisa na Askari wa Magereza Mkoani Mwanza wakimsikiliza Mgeni rasmi Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani) wakati akitoa hotuba yake fupi katika sherehe za kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza Mkoani Mwanza katika Ukumbi wa Bwalo la Gereza Kuu Butimba, Jijini Mwanza.

WASHIRIKI 20 WA SHINDANO LA TMT WAINGIA RASMI KAMBINI JANA USIKU, TAYARI KWA SAFARI YA KUWANIA MILIONI 50


 Muonekano wa TMT House ambayo washiriki 20 wa Shindano la Tanzania Movie Talents wameweka kambi rasmi kuanzia jana Usiku kwa mchakato wa kuwania Milioni 50 katika fainali itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa nane
 Mmoja kati ya Washindi watatu kutoka Kanda ya Kusini, Mwanaafa Mwizago akiingia rasmi kambini hapo jana wakati wakitokea kwenye matembezi. Washiriki wote 20 ambao ni washindi kutoka Kanda sita za Tanzania sasa wapo kambini kwaajili ya kujifua ili kuwania kitita cha Shilingi Milioni 50 katika fainali kubwa itakayofanyika mwisho wa Mwezi wa nane.
 Baadhi ya washiriki wa Fainali ya Shindano la TMT wakiingia kambini hapo jana Usiku
 Washiriki wakiwa ndani ya Nyumba ya TMT tayari kwa kambi
Washiriki wakipewa maelekezo mara baada ya kuwasili kambini hapo jana.Picha zote na Josephat Lukaza - Lukaza Blog
-
Na Josephat Lukaza - Proin Promotions - Dar Es Salaam.
Washiriki 20 kutoka Kanda sita za Tanzania wameingia rasmi kambini hapo Jana mara baada ya kumaliza zoezi la Kupima Afya, kutembezwa sehemu mbalimbali za Jiji la Dar pamoja na Ofisi za Global Publishers.
Washiriki hao watakaa kambini kwa Siku 64 ambapo wataanza rasmi kufundishwa Hapo kesho siku ya Jumatatu na walimu kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na Chuo Cha Sanaa Bagamoyo ambapo baadae sasa baadae zoezi la kuanza kuwapigia kura washiriki hao litaanza na hatimaye watanzania ndio watakuwa majaji kwa washiriki hao ambapo mshindi mmoja wa Shilingi Milioni 50 atapatikana katika Fainali itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa Nane.
Zoezi la Upigaji kura litaanza mapema wiki ijayo ambapo washiriki wote watakuwa tayari washapewa namba za ushiriki na hatimaye watanzania kuweza kuwachagua washiriki wanaowaona wana vipaji.
Zoezi hili la kupiga kura litapelekea Washiriki wawili kuondolewa kila wiki katika Kambi ya TMT ambapo pona yao ni kutoka kwa Watanzania ambao ndio watakuwa majaji kwa kuwapigia kura.
Vilevile Mara baada ya washindi hawa wa kanda kuingia kambini Vipindi vyetu vitaendelea Kurushwa kila siku ya Jumamosi Saa 4 Usiku na Kurudiwa kila Siku ya Jumapili Saa 10 Jioni na Jumatano Saa tano usiku kupitia Runinga ya ITV.
Tunawaomba watanzania kuendelea kutizama vipindi vyetu kwani vimekuwa na mvuto wa hali ya juu sana lakini pia kuendelea kuwawezesha  Washiriki wanaowaona wana vipaji ili kuwa ushindi.
Namba za washiriki zitaanza kuonekana katika Kipindi chetu kijacho ambapo Sasa watanzania wataanza kuwapigia kura kwenda namba 15678Na ili kuweza Kufahamu taarifa zaidi za TMT unaweza kutuma neno "TMT" kwenda namba 15678.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Akutana na Wazee Kutoka kata ya Nsimbo katika Jimbo la Kigoma Kusini na Wazee Kutoka Kijiji cha Kwaraa, Babati

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Wazee kutoka kata ya Nsimbo katika jimbo la Kigoma Kusini baada ya kuzungumza nao ofisini kwake  bungeni mjini Dodoma Juni 28, 2014
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na wazee kutoka kijiji cha Kwaraa, Babati  wakiwa na Mbunge wao wa Babati Mjini, Kisyeri Chambiri (watatu kushoto) ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Juni 28, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na  wazee kutoka kata ya Simbo wilayani Uvinza, ofsini kwake mjini Dodoma Juni 28, 2014. Kulia ni Mbunge wa Kigoma Kusini, David kafulila (kulia) na wa sita kushoto ni Mbunge wa kigoma Mjini Peter Serukamba.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

VIDEO:Shetta ft. Diamond Platnumz- Kerewa (Official Video)



HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO P. PINDA (MB), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WAKATI WA KUHITIMISHA MKUTANO WA KUMI NA TANO WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TAREHE 28 JUNI, 2014

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda
---
 HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO P. PINDA (MB), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WAKATI WA KUHITIMISHA MKUTANO WA KUMI NA TANO WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TAREHE 28 JUNI, 2014
  UTANGULIZI


a)    Masuala ya Jumla

Mheshimiwa Spika, 1.    Naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa Rehema kwa kutupatia uzima na afya hadi kufikia siku ya leo. Tumekuwepo hapa kwa takriban miezi miwili ambapo tumeweza kupokea na kujadili Taarifa za Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi za Serikali kwa mwaka 2013/2014 na Mwelekeo kwa mwaka 2014/2015 kwa Wizara mbalimbali na hatimaye kupitisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2014/2015. 


2.    Napenda kutumia nafasi hii ya awali kuwapongeza Waheshimiwa Wabunge wote kwa kazi nzuri ya kutukuka ambayo wameifanya kwa nidhamu na ufanisi mkubwa, hususan wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Serikali na Mafungu ya Wizara za Kisekta. Kipekee niwashukuru Wajumbe wa Kamati ya Bajeti chini ya Uongozi mahiri wa Mheshimiwa Mtemi Andrew John Chenge, Mbunge wa Jimbo la Bariadi Magharibi kwa kazi yao nzuri ya kuchambua Bajeti ya Serikali na Sheria zinazoambatana na masuala ya Bajeti. Changamoto zilikuwa nyingi,   lakini   kwa   pamoja   tumekubaliana   na   kuafikiana. Kazi kubwa iliyoko mbele yetu ni kwenda kushirikiana na Wananchi katika utekelezaji wa Bajeti hii ili kuwaletea maendeleo.


Mheshimiwa Spika, 3.    Katika kipindi hiki tukiwa hapa Bungeni, yapo matukio ya kusikitisha yaliyotokea ambapo baadhi ya Waheshimiwa Wabunge walipoteza Wapendwa wao. Aidha, yapo matukio ya Kitaifa yaliyosababisha kupoteza maisha ya Ndugu, Jamaa na Marafiki. Napenda kutumia nafasi hii kuwapa pole Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote waliofikwa na misiba na majanga mbalimbali, ikiwa ni pamoja na wote waliopotelewa na Ndugu, Jamaa na Marafiki.



Mheshimiwa Spika, 4.    Kipekee niwape pole ndugu, jamaa na marafiki waliopotelewa na ndugu zao na wote waliopata majeraha wakati kulipotokea Mlipuko wa Bomu pale Darajani, Zanzibar. Tukio hili la kusikitisha halipendezi kwa Nchi yetu. Niwaombe Wananchi wote kwa umoja wetu tushirikiane kuwa Walinzi katika maeneo yetu na kuwezesha kuwatambua mapema wale wote wenye nia mbaya ya kuharibu amani na utulivu katika Taifa letu.

Minister for Foreign Affairs and International Co-operation,Bernard Membe Guest of Honour at Pope's Anniversary


  Hon. Bernard Membe listens to the speech by the Apostolic  Nuncio in Tanzania, Archbishop Francisco Montecillo Padilla.
 The Minister for Foreign Affairs and International Co-operation, Hon. Bernard Kamilius Membe (MP), speaking at the ceremony, hosted by the latter in Dar es Salaam on Friday evening to mark the first anniversary of the pontificate of Pope Francis. Hon. Membe praised Pope Francis for his "focused direction on world peace and harmony." He said the word of GOD upheld by all faiths preached love, which was the cornerstone for world peace, stability and development. "I believe that the voice of the Pope will remain strong and continue to be heard and provide guidance to us and to the people of the world," he said.
 Members of the diplomatic community follow the speech by Hon. Membe
 Retired President Benjamin Mkapa (Right)  follows events at the ceremony to mark the first anniversary of the pontificate of Pope Francis. Left is the Dean of Diplomatic Corps, Ambassador Juma-Alfani Mpango
  Bishops and invited guests listen to the speech by Hon. Membe
  Archbishop Padilla bids farewell to Hon. Membe at  the end of the ceremony
 Minister Membe greets Bishop Methodius Kilaini at the function
 Minister Membe, exchanges views with the Apostolic Nuncio in Tanzania, H.E. Archbishop Francisco Montecillo Padilla (Centre) during the ceremony. Left is retired President Benjamin Mkapa.
 The Director of Europe and America in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation, Ambassador Joseph Edward Sokoine  exchanges views with the British High Commissioner to Tanzania, Ambassador Dianna Melrose, at the ceremony.
 The Minister for Lands and Human Settlements Development, Prof. Anna Tibaijuka, meets the Swedish Ambassador to Tanzania, H.E. Lenarth Hjelmaker.
 Hon. Membe has a word with Bishops.
Hon. Membe, Prof. Tibaijuka and Ambassador Mpango (Left) pose with the bishops
Invited guests follow the proceedings.Photo Reginald Philip

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...