BI KIDUDE
Kwa Taarifa zilizopatikana punde, ni kuwa yule mwimbaji maarufu na
mkongwe wa muziki wa Mwambao FATMA BINTI BARAKA alimaharufu kama Bi
Kidude amefariki hii leo...Taarifa hizo pia zimethibitishwa na ndugu wa karibu wa Bi Kidude! Chanzo cha umauti ni maradhi yatokanayo na uzee!
Bi Kidude amefariki ktk hospitali ya Hindu Mandal... Atakumbukwa kwa umahili wake ktk nyimbo za Taarabu ndani na nje ya nchi...alama ya Utamaduni wa Mzanzibar ktk matamasha ya muziki kama ZIF na Sauti za Busara.
...itakumbukwa hivi karibu Bi Kidude na baadhi ya Wanamuziki nguli kama Muhidin Ngurumo walitunukiwa Nishani ya heshima ktk mambo ya muziki pale Ikulu....
Wasifu Wake:
Mwanamuziki mkongwe katika Taarab Fatuma Bint Mbaraka maarufu kwa jina la Bi Kidude amefariki dunia muda mchache uliopita huko Bububu Zanzibar, sehemu alikokuwa anaugulia kwa kipindi sasa. Mwili wake utahamishiwa kwake Rahaleo na mazishi yatakuwa kesho. Bi Kidude alizaliwa katika kijiji cha Mfagimaringo, alikuwa binti wa mchuuzi wa nazi, hakuna anayejua haswa Bibi huyu alizaliwa tarehe ngapi, kuna hata mawazo kuwa alikwishafikisha miaka 102.
Katika mwaka 1920 tayari alikuwa amekwisha anza kuimba katika vikundi vya sanaa kule kwao, mwaka 1930 alijiunga na Egyptian Musical Club ya Dar es Salaam na kuzunguka miji mingi ya Tanganyika wakati ule , mwaka 1940 alirudi Zanzibar ambako awali alikuwa amekimbia kwa kuwa aliozwa kwa nguvu na mtu aliyemzidi sana umri.
Bi Kidude pia liwahi kuimba na Sitti Binti Sadi wakati wa ujana wake, na katika maisha yake Bi Kidude amekwisha zunguka mabara yote akiimba katika majukwaa na wanamuziki maarufu ulimwenguni.
No comments:
Post a Comment