Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema. Zitto Kabwe
--
Nimekuwa naulizwa kuhusu Habari za mama yangu Mzazi Bi. Shida kuvamiwa na kutishiwa bastola. Nawajibu watu Kwa ujumla kwamba
“Moja,
mie sio msemaji wa familia. Ni basi tu katika watoto wa mama yetu mie
najulikana zaidi na hivyo mama anaitwa Mama Zitto. Kwetu Kigoma haitwi
hivyo, ama Ni mama Salum au mama Lulu.
Pili,
hili Ni suala la polisi. Lipo polisi na linashughulikiwa na polisi.
Nisingependa kulisemea wakati Ni suala linalochunguzwa na polisi. Mama
yangu Ni mama wa kawaida wa kitanzania kama mama mwingine yeyote yule.
Matukio ya namna hii yamezagaa nchi nzima. Hivyo suala lake
litashughulikiwa kama yanavyoshughulikiwa masuala mengine yote ya
Watanzania. Polisi wakimaliza uchunguzi wao naamini hatua mwafaka
zitachukuliwa.
Ushauri-
tuwe makini na “Agente provocatuers” au in English “provocation agents”
nyakati kama hizi. Calmness is the best protection against
provocations. Nadhani mmenipata”
Nawatakia
Kila la kheri katika kazi za ujenzi wa Taifa letu na kuimarisha Umoja
na mshikamano wa Watanzania dhidi ya ufisadi, umasikini na ugandamizaji.
Majibu haya ameandika kupitia mtandao wa Kijamii wa facebook.
No comments:
Post a Comment