Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto)
akiongea jambo na Balozi wa Uingereza nchini Dianna Melrose mara baada
ya kumalizika kwa mazungumzo baina yao yaliyofanyika jana jijini Dar es
Salaam. Balozi huyo aliahidi kuendelea kushirikiana na wizara hiyo
katika sekta ya Vijana, Utamaduni, Michezo na kuendelea kutoa mafunzo
kwa maafisa habari wa Serikali na Taasisi zake.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella
Mukangara (kushoto) akisalimiana na Joseph Paync ambaye ni afisa
miradi kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini alipomtembelea ofisini kwake
jana jijini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa Uingereza nchini Dianna
Melrose.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara
akibadilishana kadi ya mawasiliano (Business Card) na Balozi wa
Uingereza nchini Dianna Melrose alipomtembelea ofisini kwake jana jijini
Dar es Salaam. Ubalozi wa Uingereza umeahidi kushirikiana na wizara
hiyo katika sekta ya Vijana, Utamaduni, Michezo na kuendelea kutoa
mafunzo kwa maafisa habari wa Serikali na Taasisi zake.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto)
akimshukuru Balozi wa Uingereza nchini Dianna Melrose kutokana na
ubalozi huo kutoa mafunzo ya mitandao ya kijamii (Social Media) kwa
maafisa Habari wa Serikali na Taasisi zake yaliyofanyika mwezi wa tatu
mwaka huu. Balozi huyo alimtembelea waziri Dk. Mukangara ofisini kwake
jana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumsalimia na kuimarisha
mahusiano baina ya Wizara hiyo na Uingereza.
Balozi wa Uingereza nchini Dianna Melrose (kulia) akimweleza Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara jinsi nchi
yake itakavyoendelea kushirikiana na wizara hiyo ikiwa ni pamoja na
kutoa mafunzo kwa maafisa Habari wa Serikali na Taasisi zake.Picha na Anna Nkinda – Maelezo
No comments:
Post a Comment