Mwili wa marehemu Nyaga poul Mawalla ukiwa katika kanisa la Kilutheri nchini Kenya usharika wa Uhuru Highway kwa ajili ya misa
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe,Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili
Lazaro Nyarandu na Sir George kahama wakiwa kanisani wakishiriki misa ya
maziko ya marehemu Nyaga Mawalla.
Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini
Chadema wa tatu kushot Mh Godbless Lema ni miongoni mwa waombolezaji
waliokuwa kanisani nchini Kenya.
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro wilani Simanjiro mkoani Manyara Christopher
Ole Sendeka na Waziri wa zamani wa mambo ya ndani Laurence Marsha
wakiwa kanisani nchini Kenya maziko ya marehemu Poul Mawalla
Kiongozi wa Dini wa Kanila la Kilutheri Kenya la Uhuru Highway akiongoza Mazishi.
Jaji Mark bomani nae alikuwa ni miongoni mwa waombolezaji walioshiriki mazishi hayo.
Sir George Kahama na mkewe wakiweka shada la maua katika Kaburi la Marehemu Nyaga Mawalla.
Mwenyejiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mkewe wakiweka shada la maua
Wanafamilia wakiweka mashada ya maua
Wabunge na Mawaziri mbalimbali wa
serikali ya Jamhurti ya Muungano wa Tanzania, wakiweka mashada ya
maua, pichani mbunge wa kahama -CCM James Lembeli akiweka shada la mau
nyuma yake ni naibu waziri wa maliasili na utaliii Lazaro Nyalandu
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akiweka shada la Maua
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt Batilda Burianiakiweka shada la maua
Baadhi ya jamaa wa karibu wa Marehemu
Nyaga ambao ni wabunge wakiweka Shada la Maua pichani ni mbunge wa
Arusha Mjini -Chadema Mh Godbless Lema na Mbunge wa iringa Mjini Chadema
Mchungaji Msigwa
Familia ya Marehemu Nyaga Mawalla wakiwa wenye simanzi nzito wakati wa Mazishi hayo.
Watoto wa Marehemu Nyaga wakiwa na ndugu zao.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt Batilda Buriani akiwa na mwanasheria
maarufu Jijini Arusha anayemiliki kampuni ya uwakili ya Law /Access
Advocates Mosses Mahuna wakiwa nje ya kanisa la Lutherani nchini Kenya.
----
Mazishi
ya Marehemu Nyaga Mawalla, aliyekuwa Mwasisi na Mkurugenzi wa Makampuni ya Mawalla
ya Jijini Arusha yamefanyika jana jijini Nairobi Kenya katia Makaburi ya Jumuia
ya Langata.
Mapema
kabla ya Mazishi hayo yaliyohudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali na
familia na marafiki ilifanyika Misa ya kumuombea Marehemu katika Kanisa la
KKKK, Uhuru Highway.
Miongoni
mwa Viongozi waliohudhuria Mazishi hayo ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk.
Batilda Burian, Viongozi wastaafu, Sir. George Kahama, Mwemyekiti wa Chadema,
Freeman Mbowe, Wabunge, Mawaziri wanasheria mabalimbali wa ndani na nje ya
Tanzania.
Marehemu
Nyaga Paul Mawalla alifariki Machi 22, 2013 jijini Nairobi alikokuwaa amelazwa
kwa matibabu Hospitali ya Nairobi.
No comments:
Post a Comment