Wednesday, August 10, 2011

Mama wa mapacha watatu aomba msaada kwa wadau

Mapacha watatu na mama yao.
Mapacha wakiwa katika picha ya pamoja.
NEEMA ya kupata watoto mapacha watatu kwa mpigo aliyoipata mkazi wa Manzese, Dar es Salaam, Amina Abubakar, imegeuka balaa na sasa mwanamke huyo anaomba msaada wa kuwasomesha.
Akizungumza ofisi za gazeti hili jana, Amina alisema sababu ya kuomba msaada huo ni kutokana na mapacha hao kufikisha umri wa kwenda shule wakati maandalizi aliyojitahidi kufanya hayajazaa matunda, huku muda unazidi kusogea.
Alisema hatua hiyo inatokana na mwanaume aliyekuwa na uhusiano naye kumkimbia tangu kuzaliwa kwa watoto hao miaka minne iliyopita.
Amina alisema alikuwa na uhusiano wa mapenzi na mwanaume ambaye alikuwa mfanyabiashara eneo la Mabibo, ambaye alikuwa anafika Dar es Salaam kutoka mkoani na kuondoka wakati yeye akiwa mamalishe.
Alisema baada ya kupata ujauzito, mwanaume huyo hakuonekana tena hadi anajifungua hajui alipo.
“Nilipokuja hapa wakati wanangu wakiwa na miezi minane nilipata msaada mkubwa baada ya Kampuni hii kunitoa kwenye gazeti nawashukuru sana, kwa hiyo nimerudi tena ili nione kama nitapata msaada wa kuwalipia ada,” alisema Amina.
Alisema hivi sasa anaendelea na biashara ya mamalishe, lakini kutokana na maisha kuwa magumu hata mahitaji muhimu ya watoto anashindwa kuyatimiza.
Kwa yeyote atakayeguswa anaomba awasiliane naye kupitia namba zifuatazo: 0718 263 968. Au Pia waweza kumpigia simu mwandishi wa habari hizi 0655 110 105

Habari hii imendikwa na Gedius Rwiza: SOURCE: MWANANCHI

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...