KAMATI kuu ya chadema jana imetangaza kuwatimua uanachama madiwani watano wa chama hicho katika halmashauri ya jiji la Arusha, akiwepo Naibu Meya, Estomih Mallah kwa tuhuma za kudharau maamuzi ya chama hicho.
Madiwani hao, Mallah wa kata ya Kimandolu, John Bayo(Elerai), Reuben Ngoi(Themi) Charles Mpanda(Kaloleni) na Diwani wa viti maalum,Rehema Mohamed, kutokana na kufukuzwa uanachama kisheria sasa wamepoteza nafasi zao za udiwani.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa chadema, Freema Mbowe, alisema kamati kuu ya chadema imefikia maamuzi hayo magumu baada ya jitihada zote za kumaliza mgogoro huo kukwama.
“kwa masikitiko makubwa kamati kuu ya chadema kutokana na mamlaka kikatiba imewafukuza uanachama madiwani watano kwa kukataa kutekeleza maamuzi halali ya chama”alisema Mbowe.
Hata hivyo, jana wakizungumza na mwananchi katika hoteli ya Darban waliyokuwa wamefikia madiwani, hao, walieleza kupinga uamuzi huo na wameahidi kukata rufani katika baraza kuu la chadema.
“tulikuja Dodoma tukijua tunakuja kufukuzwa lakini, tuliamini huenda busara zingetumika na kutambua kuwa maamuzi yetu ya kuingia katika muafaka yalikuwa ni sahihi kwa manufaa ya mji wa Arusha”alisema Mwenyekiti wa madiwani hao, Mallah.
Hata hivyo, walisema wanatarajia kukutana na wananchi waliowachagua na kueleza kilichotokea hapa Dodoma.
Akizungumzia maamuzi hayo, Mbowe alisema kamati kuu ilipokea taarifa ya utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa julai 17 mwaka huu, iliyowataka madiwani hao, baada ya kusaini muafaka huo,kujiuzuru.
Mbowe alisema madiwani hao, pia waliagizwa kuomba radhi kwa makosa waliyokuwa wamefanya kutokana na mwafaka uliofikiwa baina yao na madiwani wa CCM na TLP bila ridhaa ya chama.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
1 comment:
Kuvutia tovuti. Keep Blogging!
Post a Comment