Wednesday, May 12, 2010

Rais Kikwete mgeni rasmi harambee ya CCM


MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA KILIMANJARO, MAMA NSILO SWAI AKIONGEA KUHUSU HARAMBEE YA KUCHANGIA CHAMA HICHO MKOANI KILIMANJARO ITAKAYAYOFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM (PICHA NA MPIGA PICHA WETU)

********************************************************************************

RAIS Jakaya Kikwete atakuwa mgeni rasmi kwenye chakula cha hisani kuchangia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro itakayofanyika jijini Dar es Salaam kesho.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro Nsilo Swai alisema kuwa harambee hiyo ina lengo la kuchangisha fedha za kugharamia shughuli za uchaguzi mkuu mwaka huu na kuendeleza chama.

Harambee hiyo itafanyika kwenye hoteli ya Golden Tulip ambapo viongozi wa juu wa chama na serikali, wawakilishi wa mashirika wabunge wote wa CCM wa Mkoa wa Kilimanjaro, wakereketwa wa CCM, pamoja na wafanyabiashara wadogo na wakubwa kutoka mkoa wa Kilimanjaro watahudhuria.

Mama Nsilo Swai alisema kuwa harambee hiyo itaanza saa moja usiku ambapo kiingilio itakuwa ni Sh 50,000 kwa mtu mmoja na Sh 60,000 kwa Bibi na Bwana.

“Nawaomba wanaKilimanjaro walioko Dar es salaam na wakereketwa wa Chama Cha Mapinduzi wote kwa ujumla kuhudhuria na kuchangia chama chao”, alisema.

Swai aliongeza kuwa mbali na uchangiaji fedha taslimu pia kutakuwa na mnada wa vitu mbalimbali kama sehemu ya uchangiaji katika shughuli hiyo. Harambee hiyo itapambwa na burudani kutoka kwa bendi ya Msondo Ngoma ya jijini Dar es Salaam.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...