Monday, May 03, 2010

JK: Sihitaji kura za wafanyakazi



RAIS Jakaya Kikwete leo ameushangaza umma wa Watanzania baada ya kuanza kukiuka misingi iliyokiunda Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kuwaheshimu Wakulima na Wafanyakazi pale alipokutana na wazee wa MSkoa wa Dar es Salaam na kutoa hotuba kali akiwashutumu viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafabnyakazi Nchini (Tucta) kuwa ni wanafiki kwa kuendelea kushinikiza mgomo wa wafanyakazi licha ya mazungumzo yanayoendelea kati yao na Serikali.

“Hawa viongozi wa Tucta walisema sisi serikali ni watu wasioambilika… hawa viongozi wa Tucta ni waongo,” alisema Rais Kikwete akisisitiza kuwa hii ni moja ya sababu iliyomfanya jana awajibike kujibu.

“Sasa iweje tunakubaliana hili, kesho yake asubuhi unazungumza kama hatujakubaliana,” alisema Rais na kusisitiza: “Ninayo kila sababu kuhoji dhamira zao iwapo kweli wana nia thabiti ya kuwabeba wafanyakazi ama wana lao jambo.”

Kauli ya TUCTA

"Rais katumia lugha isiyo nzuri, hutuba yake imejaa vitisho na si demokrasia pia lugha aliyoitumia siyo nzuri na mbaya zaidi ametoa tamko lake bila ya kutusikiliza,"alisema Nicholaus Mgaya, Naibu Katibu Mkuu wa Tucta.

"Kwa muda wote tumekuwa tukijadili agenda tatu, kodi kwa wafanya kazi, maboresho ya mafao ya uzeeni na mishahara, lakini, Rais alizungumzia mishahara pekee jambo ambalo siyo haki,"alisema Mukoba na kuongeza:

"Kauli ya Rais Kikwete kwamba tulikubaliana kukutana Mei 8 mwaka huu kuzungumzia suala la mishahara, siyo ya kweli kwani hata taarifa ya Baraza la Majadiliano ya pamoja inaonyesha kuwa tulikubaliana kutokubaliana," alisema.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...