Sunday, May 09, 2010

Fainali za Kiduku







Fainali ya mashindano ya kucheza mtindo wa taarabu unaoitwa KIDUKU (Pichani) ambao vijana wa kiume huvaa nguo za kike na kukata mauno kama wanawake ilifanyika Mei 2 huku shutuma kali zikiwaendea waandaaji wa mashindano hayo kuwa wana malengo ya kuwaharibu watoto wa kiume. Mtindo wa KIDUKU uliobuniwa na mtangazaji mahiri aliyekuwa akitangaza
katika kituo cha televisheni ya Afrika Mashariki EATV, Maimartha wa Jesse umekuwa gumzo katika jiji la Dar es Salaam, kutokana na jinsi mchezo huo ulivyo wahusisha vijana wenye umri chini ya miaka 18.

Wengi wa vijana huwa ni watoto wa shule za msingi na sekondari wengine wakitokea tu mitaani kushindana kucheza mchezo wa Kiduku.

Hivi karibuni Maimartha aliandaa shindano la kumtafuta bingwa wa kiduku mwaka 2010 ambalo limewashirikisha vijana toka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.

Miongoni mwa vikundi vinavyoshiriki ni Vidoleki, Mazombi, Wanaume fasti, Wakali wa kitengo, Wakupoteza, Stavanga na Mazombi.

Katika shindano hilo mshindi wa kwanza alitarajiwa kupata zawadi ya dola 250, mshindi wa pili atapata music system na watatu wangeambulia feni. Fainali ya mashindano hayo ilifanyika Mei 2 mwaka huu katika ukumbi wa Travertine uliopo magomeni.

Kwa upande mwingine wapenzi wa muziki wa taarab wamekuwa na maoni tofauti kutokana na vijana hao kucheza huku wakiwa wamevalia nguo za akina dada jambo ambalo wengi wanalihisi kuwa linaweza likawa ni njia mojawapo ya kuwapotosha vijana hao kwa kujiingiza katika njia ya uasherati ikiwa ni pamoja na kuwa mashoga.

3 comments:

Anonymous said...

Halafu tunalalamika watoto wanafeli mitihani, hawasomi wakati serikali inaruhusu vitu kama hivi viendelee, nakumbuka wakati fulani serikali iliwahi kupiga marufuku ngoma na nyimbo zilizokuwa na mwelekeo wa kuvunja maadili mfano tokomile, chakacha, mchiririku nyimbo mfano enyi dada zetu (hii ni meli tu naipakua)wa msondo, mambo kwa soksi wa Remmy n.k
Binafsi sielewi idara ya utamaduni, Basata vinafanya kazi gani.
HAYA ACHA TUENDELEE KUTENGENEZA WASENGE WENGI ILI WAJE WATUSUMBUE BAADAE

Anonymous said...

NI VIPI KAMPUNI YA SIMU IMEWEZA KUSHIRIKI KUAANDAA SHINDANO LA WASENGE? AU KUNA MAMENDE NDANI YA KAMPUNI HIYO?

Anonymous said...

WATU WA MEDIA WEKENI AGENDA KWENYE AIBU HII HILI TAIFA LINAANGAMIA
hii ni Aibu kubwa Kaka Charaz kwa sababu tunahitaji wasomi kwa kizazi hiki na vijavyo MAIMARTHA WA JESSE anatia aibu kwa kuharibu maadili ili tu yeye apate pesa tena anawatumia watoto ambao pengine uelewa wao ni mdogo.Sio MAIMARTHA hata TIGO kampuni yenye jina zuri inajiharibia image yake kwanini isidhamini matamasha ya kimasomo mashuleni na vyuoni kwani wanafunzi hao wanahitaji udhamini kwenye matukio yao wanadanganywa na wafanyabiashara kwa manufaa yao.

SERIKALI IMELALA BASATA MNAFANYA NINI?WIZARA YA HABARI NA UTAMADUNI MNAFANYA NINI??TAIFA LETU LINAANGAMIA TUTAKUWA NA UKIMWI KIWANGO CHA AJABU KWA KUINGIA MAPENZI YA JINSIA MOJA KAMA ASIA.HUU MWELEKEO UNALETA USHOGA.INAUMA SANA.....

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...