Wednesday, May 12, 2010

Daraja la Umoja lazinduliwa



Rais Jakaya Kikwete na Rais Guebuza wa Msumbiji wakisalimia wanachi katika daraja la Umoja linalounganisha Tanzania na Msumbiji kijiji cha Mtambaswala mkoani Mtwara wakati wa uzinduzi wa daraja hilo mapema leo





Leo marais Jakaya Kikwete na mwenzake Armando Guebuza wa Msumbiji, wamezindua Daraja la Umoja linaloziunganisha nchi hizi mbili kama ishara ya mshikamano na udugu wa kihistoria uliopo baina ya watu wa nchi hizo.

Daraja hilo lenye urefu wa meta 720 na upana wa meta 13.5 ni kiunganishi kizuri kwa nchi hizi na tunatarajia litatumiwa kwa maslahi ya watu wa Tanzania na Msumbiji, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na matatizo ya barabara. Ni ukombozi kwao.

Wazo hilo lililotolewa na marais waasisi; marehemu Julius Nyerere wa Tanzania na Samora Machel wa Msumbiji mwaka 1975 na kutekelezwa na viongozi waliofuata na kukamilishwa na waliopo sasa.

Wazo limesimamiwa na mkandarasi M/s China Geo- Engineering ambaye alisimamiwa na Mhandisi Mshauri NorConsult kutoka Norway, kwa uvumilivu wao na juhudi kubwa za kukamilisha daraja hilo, ambalo litabaki kuwa alama ya uhusiano mzuri na wa kihistoria wa nchi hizi.

Ili kuenzi wazo hili na kuheshimu uamuzi wa kulijenga, ni vizuri sasa wananchi wakawa walinzi wa wenzao, dhidi ya hujuma yoyote itakayofanywa kwenye daraja hilo, hasa hii ya ukataji vyuma kwa ajili ya tamaa ya kujipatia kipato cha haraka haraka.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...