Monday, May 31, 2010

Ziara ya TEA katika picha


MWALIMU WA TAASISI YA TEKNOLOJIA NA SAYANSI MBEYA ,BW DANIEL SIKONDE (KUSHOTO) AKITOA MAELEKEZO KWA WAJUMBE WA BODI YA MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA (TEA) JUU YA MOJA YA VIFAA VYA KUFUNDISHIA VILIVYOTOLEWA NA MAMLAKA HIYO, KWA VIFAA VILIVYOTOLEWA NA TEA VINA THAMANI YA SHILINGI MILIONI 436.PICHA KWA HISANI YA ABDUL NJAIDI.

Mchakato wa kumfanya Mwalimu Nyerere kuwa Mtakatifu


Rais Museveni akimkaribisha Mama Maria Nyerere shereheni huko Namugogo wikiendi hii. Chini akimwagilia mti alioupanda kama kumbukumbu ya siku hii
Hizi ni baadhi ya picha za mchakato wa kumuombea baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere kuwa mwenyeheri na baadaye kuwa Mtakatifu. Huwezi kuwa mtakatifu kabla hujawa mwenyeheri.
Kesho kutakuwa na ibada ya kumuombea Mwalimu Nyerere kuwa Mwenyeheri na hatimaye kuwa Mtakatifu katika kanisa lilipo Namugongo ambapo inatarajiwa kuwa marais au wawakilishi kutoka katika baadhi ya nchi za Afrika watahudhuria ibada hiyo.
Familia ya Mwalimu iliwasili Hapa uganda Jumamosi kwa ajili ya Ibada hiyo. Mbali na familia ya baba wa taifa mamia kwa maelfu ya watanzania pia wameondoka nchini 28 kuelekea huko namugongo kwa ajili ya ibada ya hija inayofanyika kila mwaka June 3 katika kanisa hilo.
Mama Maria yuko pamoja na Kikundi cha sala za wanamaombi cha Marian Healing faith Centre cha River Side, Ubungo jijini Dar. PICHA NA HABARI KWA HISANI YA Michuzi

Friday, May 28, 2010

Miss Dar Inter College




Mshindi wa Miss Dar Inter College , Rose John wa chuo cha ustawi wa jamii (katikati) akiwa amepozi kwenye picha na zawadi mshindi wa pili ,Cassiana Milinga kutoka chuo cha biashara CBE (kulia) na mshindi wa tatu Marylidya Boneface naye kutoka chuo cha Ustawi wa Jamii. Picha na Silvan Kiwale

Thursday, May 27, 2010

Moto ni balaaa




Hicho ni kiwanda cha kutengenezea maakasha ya kuhifadhia samaki (Boya Box) Falcom Packaging Ltd kikiteketea kwa moto. Picha kwa hisani ya jeshi la Polisi Mwanza.

Tuesday, May 25, 2010

JK ahisi ahisi hatari EAC



MWENYEKITI wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais Jakaya Kikwete ametaka viongozi na wanajumuiya wa Umoja huo kuepuka kuchukua hatua au kutoa matamko yatakayochokoza mataifa jingine wanachama au viongozi na watu wake kwani kufanya hivyo kutahatarisha umoja.

Rais Kikwete aliyasema hayo jana alipohutubuia Bunge la jumuia hiyo mjini Nairobi Kenya katika mkutano wa tatu wa Bunge hilo.

“Ninawataka viongozi wote wa Afrika Mashariki, waandishi wa habari, watu wenye ushawishi katika jamii, wachambuzi wa masuala mbalimbali ya jamii, kuepuka kuchukua hatua au kutoa kauli ambazo zitachokoza taifa, viongozi na au watu wake,” alisema Rais Kikwete.

Alisema vitendo hivyo vitavuruga uelewano imani iliyoanza kujijenga miongoni mwao, ambalo ni jambo muhimu kwa ushirikiano huo wa kikanda.

“Haya masuala ndiyo yanayoharibu imani iliyokuwapo, ambayo ni muhimu kwa mafanikio ya ushirikiano wa Afrika Mashariki. Ni lazima tutambue maneno na uchokozi ndivyo vilivyoisambaratisha jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977,”alisema.

Alisema kukosekana kwa imani miongoni mwa mataifa wanachama ndiko kulikoiporomosha jumuiya ya mwanzo ya Afrika Mashariki hivyo akataka kutorejewa tena makosa ya awali.

“Ni lazima tujizuie kurudia makosa tuliyoyafanya awali. Najua, kutaibuka tofauti miongoni mwetu, lakini hebu basi tutafute njia muafaka za kukabiliana nazo. Ni lazima tuepuke kutoa matamko ya uchokozi dhidi ya wengine hadharani, hii itavuruga kuaminiana na kuua moyo uliojengwa wa kiudugu na kushirikiana,”alisema.

Alisema ni lazima mataifa hayo wanachama yafahamu kuwa hakuna ushirikiano unaweza kusonga mbele kukiwa na mazingira mabaya ya kutoaminiana na kupoteza imani miongoni mwao. SOURCE: HOTUBA YA RAIS.

Tume ya kurekebisha sheria


Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Jaji Fredrick Werema akikabidhiwa ripoti mbalimbali zilizofanyiwa kazi na Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) na Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Japhet Sagasii wakati alipoitembelea tume hiyo leo, wengine ni Naibu Katibu Mtendaji (Utafiti) Adam Mambi (wa pili kulia ) na Naibu Katibu Mtendaji (Mapitio) Angela Bahati .

Waganda wamtangaza mtakatifu


KAMPALA, Uganda
JULIUS Kambarage Nyerere, rais wa kwanza wa Tanzania, Juni mosi atatangazwa rasmi na Waganda kuwa Mtakatifu, ikiwa ni sehemu ya shamrashamra ya kukumbuka Siku ya Mashahidi wa Dini.
Taarifa kutoka nchini Uganda zimeeleza kwamba baadhi ya wakuu wa nchi za Afrika na mjane wa Nyerere, Mama Maria Nyerere pia watahudhuria sherehe hizo zinazotarajiwa kufanyika huko Namugongo nchini Uganda.
Mwaka jana, Rais Yoweri Museveni wa Uganda alishiriki katika kampeni za kutaka Nyerere, ambaye serikali yake ya awamu ya kwanza iliongoza vita vya kuundoa utawala wa kijeshi wa Uganda, atangazwe kuwa mtakatifu.
Kampeni hizo zilianza mwaka 2006 baada ya Vatican kukubali ombi lililowasilishwa na askofu wa Jimbo la Musoma lililo kaskazini mwa Tanzania.
Maandalizi ya sherehe hiyo yanaendelea kwa kiwango cha juu na msimamizi wa shughuli hiyo, Padri Dennis Ssebuggwawo alisema shamrashamra hizo zitatanguliwa na siku tisa za maombi maalum, zitakazoanza Mei 26 na kuisha Juni 2.
Alisema jimbo la Moroto ndiyo litakakuwa mwenyeji wa sherehe hizo mwaka huu na zitakazoongozwa na neno lenye kichwa cha habari “Nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari (Mathayo28:20)".
Mashahidi 22 wa dini wa Kanisa Katoliki waliuawa kati ya mwaka 1885 na 1886.
Hata hivyo, rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (Tec), Askofu Yuda Thadei Ruwa’ichi amesema kuwa hatua hiyo ni upotoshaji wa makusudi na si sahihi. SOURCE; NEWVISION UGANDA & MWANANCHI

Tanesco yapata mkurugenzi mpya



BODI ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) imemteua Mhandisi William Mhando kuwa mkurugenzi mkuu mpya wa shirika hilo na mteule huyo ameahidi kupambana na tatizo la mikataba mibovu.
Taarifa iliyotolewa jana na Tanesco imeeleza kuwa uteuzi huo wa kuziba nafasi hiyo moto iliyoachwa wazi na Dk Idris Rashid ,unaanza rasmi Juni mosi, mwaka huu.
"Nashukuru kwa uteuzi huo, lakini najua nina challenge (changamoto) nyingi. Kuna mambo mengi ya kuwafanyia wananchi ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa umeme wa uhakika," alisema Mhando alipoongea na Mwananchi jana baada ya uteuzi huo.
"Changamoto nyingine ni usambazaji wa umeme vijijini, kuboresha huduma kwa wateja na upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mipango ya shirika."
Mkurugenzi huyo mpya aligeukia matatizo ya shirika hilo na kusema kuwa atahakikisha mikataba yote mibovu inapatiwa ufumbuzi na kuweka mkakati wa kudhibiti isijirudie baada ya Tanesco kukumbana na kashfa ya mkataba inayokula fedha za walipa kodi kama ya IPTL na ule uliotingisha nchi wa Richmond Development LLC.
Pia kwa sasa iko kwenye mgogoro wa mkataba wa ugavi wa nguzo za umeme na kampuni ya Sao Hill, ambayo ilikuwa ikilaumiwa kwa kushindwa kutimiza malengo ya kuzalisha nguzo zaidi ya 9,000 hadi kufikia Machi 31.
Mhando ameteuliwa kushika nafasi hiyo akitokea katika kitengo cha usambazaji umeme na masoko cha shirika hilo ambako alikuwa meneja mkuu.
Uteuzi wa Mhando unafikisha ukingoni vita kubwa iliyoripotiwa kuwepo baina ya bodi ya wakurugenzi na menejimenti ya Tanesco, ambazo zilikuwa zikidaiwa kuwa kila moja ilitaka mtu wake arithi nafasi ya Dk Idris ambaye aliachia ngazi ghafla Septemba 2009 baada ya awamu yake ya kwanza kumalizika. SOURCE:MWANANCHI

Monday, May 24, 2010

Liyumba aramba mvua mbili jela


Liyumba apatikana na hatia, ahukumiwa kwenda jela miaka miwili!
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo imesoma Hukumu dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Amatus Liyumba,Katika hukumu hiyo Liyumba amepatikana na hatia na kuhukumiwa kwenda jela miaka miwili dhidi ya kesi ya utumiaji mmbaya wa madaraka .

Hukumu hiyo imetolewa muda mfupi uliyopita baada ya kumuona mtuhumiwa ana kosa la kutumia vibaya madaraka na hivyo kustahili kwenda jela. Hata hivyo, wakili wa mtuhumiwa, Majura Magafu, hakuridhika na hukumu hiyo kwa madai kuwa kuna makosa mengi ya kisheria yamefanyika hivyo anakata rufaa na kwamba taratibu za kutimiza rufaa hiyo, zinaanza leo leo.

Wakati wote wa kusomwa kwa hukumu hiyo, Liyumba alionekana kutokwa jasho na hivyo shati lake lote kuloa. Hali mahakamani hapo ilikuwa tete kutokana na kugawika kwa mitizamo ya watu, wapo walioona hakutendewa haki na wengine kusema miaka miwili ni midogo ukilinganisha na uzito wa tuhuma alizokuwa akikabiliwa nazo. Picha zaidi za tukio zitawajia baadae kidogo....

===================

Awali Liyumba alifikishwa mahakamani hapo akiwa pamoja na aliyekuwa meneja miradi wa BoT Deogratius Kweka, ambapo kwa pamoja walikabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kutumia vibaya madaraka aliyokuwa nayo, jambo lililopelekea serikali kupata hasala ya sh bilioni 221, kupitia ujenzi wa majengo pacha ya BoT.

Hata hivyo kabla ya kuanza kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka, upande wa mashtaka ulimuachia aliyekuwa mshtakiwa mwenza wa Liyumba {Kweka}, na kumshitaki Liyumba kwa kesi hiyo.Upande huo wa mashtaka uliita mahakamani hapo mashahidi 8, wakiwamo waliokuwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa BoT, pamoja na kutoa vielelezo mbali mbali vinavyohusiana na kesi hiyo.

Baada ya ushahidi huo kumalika kusikilizwa, Mahakama ilifikia uamuzi wa kumfutia Liyumba shtaka la kuisababishia serikali hasala ya bilioni 221 baada ya Upande huo wa serikali kupitia ushahidi na vielelezo vyake kushindwa kuithibitishia mahakama hiyo kama Liyumba alihusika na kosa hilo.Kufuatia uamuzi huo, mahakama ilimtaka Liyumba kujitetea juu ya uhusika wake katika shtaka la kutumia vibaya madaraka aliyokuwa nayo.

Katika utetezi wake Liyumba alijitetea mwenyewe kama shahidi wa kwanza kutoka upande wa utetezi, na baadae alimwiita shahidi wa pili ambaye ni Bosco Ndimbo Kimela, aliyekuwa katibu wa BoT.Baada ya kumaliza usikilizwaji wa ushahidi huo, mahakam hiyo ilizitaka pande zote mbili kuwasilisha hoja zao za kisheria, ambapo alipanga kusoma hukumu dhidi ya Liyumba ifikapo May 24, 2010.

source: michuzi blog

Sunday, May 23, 2010

JK apokea vifaru


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amwshikilia SANAMU ya Faru wakati wa sherehe za kuwapokea Faru Watano kati ya 32 kutoka Afrika ya Kusini.Sherehe za kuwapokea Faru hao walioko katika Kontena katika gari nyuma ya Rais zilifanyika katika uwaanja wa ndege wa Seronera katika mbuga ya wanyama Serengeti juzi jioni.Kulia ni Waziri wa mazignira wa Afrika ya kusini Buyelwa Sonjica aliyekabidhi Faru hao kwa niaba ya Serkali ya Afrika ya Kusini.Kushoto ni Waziri wa Utalii na maliasili Shamsa |Mwangunga (Photos by Freddy maro)

Twiga Stars yaiangamiza Eritrea 8-1



TIMU ya taifa ya Tanzania ya wanawake Twiga Stars imetoa kipigo cha mbwa mwizi kwa Eritrea kwa kuichakaza kwa mabao 8-1 kwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika.

Mshambuliaji wa Twiga Stars, Mwanahamisi Omary alifunga mabao manne peke yake huku Asha Rashidi akiziona nyavu hizo mara tatu kwenye karamu hiyo kubwa ya mabao iliyoshudiwa ikitokea kwenye uwanja wa Uhuru.

Twiga ilipata bao lake la kwanza dakika ya sita lilofungwa na nyota wa mchezo huo Mwanahamisi aliyeunganisha vizuri mpira wa adhabu uliopigwa na Ester Chaburuma.

Kuingia kwa bao ilo kuliamsha ari ya Twiga Stars ilipata bao la pili dakika ya 19, limefungwa na nahodha Sophia Mwasikili kwa shuti la umbali wa mita 18, akipokea pasi mzuri kutoka kwa Etoe Mlezi.

Wakati Eritrea wakijuliza nini kinatokea Asha Rashidi aliwalamba chenga mabeki na kupiga shuti lililomshinda kipa Semhar Bekit na kujaa wavuni kuwa bao la tatu.

Mwanahamisi alifunga bao la nne dakika 27 kwa ufundi kwa kumchenga kipa Bekit alikipokea pasi ya Fatuma Khatib kufanya matokeo kuwa 4-0 hadi mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na wenyeji walipata bao la tano dakika 60 kupitia kwa Asha kabla ya Mwanahamisi kufunga la sita dakika 62.

Mchezo huo uliokuwa wa upande moja kwani Eritrea walionekana kushindwa kuendana na kasi ya mchezo walijikuta wakifungwa bao la saba na nane yaliyofungwa na Rashidi (74) akipokea pasi ya Etoe naye Mwanahamisi
alifunga bao lake la nne dakika 78, akimalizia kazi ya Rashidi.

Eritrea ilipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Rahwa Solomon aliyewapiga chenga mabeki na kufunga bao hilo dakika ya 90.

Makocha wa Twiga Stars, waliokuwa mafunzoni nchini Brazil, Charles Boniface Mkwasa na Adold Richard wamewasiri uwanjani hapa na kukaa kwenye viti maalumu.

Naye waziri Geogre Mkuchika amewapongeza Twiga Stars kwa ushindi mkubwa walioupata na kuwataka waongeze juhudi ili wafanye vizuri kwenye mechi ya marudiano.

Huku akiahidi kushirikiana na TFF katika kutafuta mkoa wenye baridi kwa ajili ya kuweka kambi ya timu hiyo. Imeandikwa na Doris Maliyaga; SOURCE:MWANANCHI

Jamal Khan wa Dar aibuka mshindi mbio za Magari Zig Zag

Pichani Ally Kiraka wa Tanga na Ahmed Aslam wakifurahi baada ya kukabidhiwa kombe la ushindi wa sita.

Mshindi wa mbio za magari Tanga Rally Zig Zag 2010 Jamil Khan na msoma ramani wake Rahim Suleyman
wakifurahia baada ya kupokea kikombe cha ushindi katika viwanja vya Popatlal Jijini Tanga,alitumia gari aina ya Subaru Imreza na kukimbia kwa muda wa saa 1.33.44.

Dereva mkongwe katika mashindano ya
mbio za magari Afrika Mashariki,Jayant Shah (70) akipokea kombe la ushindi wa tatu katika mashindano ya Tanga Rally 2010 na Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Ibrahimu Msengi,mkongwe huyo alishiriki kwa kuendesha gari aina ya Dutsun 260z iliyotengenezwa mwaka 1975 akiwa na msoma ramani wake Radhi Chana waliotumia saa 1.43.53.

Thursday, May 20, 2010

MEYA WA JIJI AKAMATWA KWA MAUAJI YA KATIBU CCM



SAKATA la kifo cha katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Isamilo wilayani Nyamagana mkoani Mwanza, Bahati Stephano (50) aliyefariki dunia baada ya kuvamiwa ofisini kwake na kuchomwa kisu, limeingia katika hatu nzito baada ya Meya wa jiji la Mwanza Leornad Bandiho Bihondo (64) (pichani) kukamatwa na jeshi la polisi kwa kuhusika.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Simon Sirro alisema kuwa kukamatwa kwa meya huyo kumetokana na taarifa za siri ambazo watuhumiwa watatu wa awali wamezitoa hivyo kufanya watuhumiwa kufikia wane.

Katibu huyo aliuawa mei 14, mwaka huu majira ya saa 6:30 mchana baada ya mtuhumiwa aliyetambulika kwa jina la Jumanne Oscar (30) kuingia ofisini kwa katibu huyo akisingizia kuwa na shida za kiofisi na baada ya kuruhusiwa kuonana naye alisikika wakibishana naye na baadaye alionekana akitoa kisu na kumchoma.

Kwa mujibu wa mashuhuda baada ya kuona mabishano hayo waliamua kufuatilia na kumuona kijana huyo akitoa kisu na kumchoma katibu huyo, upande wa titi la kushoto na tumboni, baada ya kufanya hivyo inadaiwa alitoka mbio kutaka kutokomea, lakini wasamalia wema wakiwemo wafanyakazi wenzake na marehemu wamkimbiza na kumkamata akitaka kujitosa ziwani” alisema Kamanda Sirro.

Jana akizungumza na waandishi wa habari kamanda Sirro alisema, meya Bihondo alikamatwa Juzi saa 10 alasiri katika uwanjwa wa ndege wa Mwanza alipokuwa akitokea safarini jijini Dar es salaam kwa safari zake za kikazi.

‘Bwana Bihondo tunamshikilia kama mtuhumiwa, hii ni kwa sababu baada ya kufanya mahojiano na watuhumiwa wengine watatu walimtaja yeye kuwa miongoni mwa watu ambao wanahusika. Jeshi langu bado linaendelea na uchunguzi na tutamfikisha mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika” alieleza Sirro.

Bihondo anaungana na watuhumiwa wengine ambao ni Jumanne Oscar aliyekamatwa siku ya tukio na kueleza kuwa alifuatwa Kigoma kwa kazi ya kuua na mtuhumiwa Baltazal Shushi (43) ambaye naye baada ya kutiwa mbaroni alimtaja kampeni meneja wake Abdul Hausi (45) wote wamekamatwa.

Alisema licha ya Bihondo kukamatwa bado kuna watuhumiwa wengine wanatafutwa na jeshi lake (lakini hakuwataja kwa sababu za kuhofia kuharibu upelelezi) na kusisitiza kuwa jeshi lake litahakikisha linawatia mbaroni na kukomesha mtandao wa watu waliozoea kuhusika na mauaji.

‘Niwaombe wananchi wazidi kutoa ushirikiano, kwani bila ya ushirikiano jeshi langu halitaweza kuwabaini mtandaao wa wauaji” alisisitiza Sirro. Habari hii imeandikwa na Frederick Katulanda. SOURCE: MWANANCHI

President meets EU Foreign Minister


President Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with EU Foreign Minister Baroness Cathy Ashton at Dar es Salaam State House in Dar es Salaam this morning.

CC-CCM meets in Dar


President Jakaya Mrisho Kikwete chairs the CCM Central Commitee (CC) in Dar es Salaam this morning.Others in the picture are Zanzibar's President Amani Abeid Karume,Vice President Dr. Ali Mohamed Shein and The SMZ Cheif Minister Shamsi Vuai Nahodha.On the Left is CCM Secretary General Yusuf Makamba (photos by Freddy Maro).

Wednesday, May 19, 2010

Mkutano wa jimbo



Mkutano Mkuu wa Jimbo Nachingwea uliofanyika Jumamosi, Mei 15, 2010 na kuhudhuriwa na Mbunge Nachingwea Mathias Chikawe, Mbunge wa Jimbo jirani la Mtama Bernard Membe na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi na Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM wa Mikoa Mzee Ally Mtopa. Wajumbe zaidi ya 800 walihudhuria kutoka kata 27 za Jimbo la Nachingwea.

Balozi Alfonso aula



BALOZI wa Marekani hapa nchini, Alfonso Renhardt akiwa pamoja na Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Juma Mwapachu akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya jumuiya ya Afrika ya Mashariki jana mara baada ya kukabidhi hati za utambulisho kwa katibu huyo wa EAC. Picha na Mussa Juma.

Simba kubwa lamezwa na paka 1-0


Mabingwa wa soka Tanzania timu ya Simba leo imechapwa goli moja na timu ya Sofapaka mabingwa wa soka kutoka nchini Kenya katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Nyamirambo Kigali nchini Rwanda kuanzia saa tisa na nusu kwa saa za Tanzania katika mashindano ya vilabu bingwa Afrika Mashariki na Kati yanaoandaliwa na SECAFA.

Mjumbe wa kamati ya Utendaji na msemaji wa klabu hiyo aliyeshuhudia mchezo huo alijibu kwa kifupi katika simu kwamba tumefungwa goli moja, lakini habari zaidi zinasema mchezaji wa Sofapaka John Baraza ndiye aliyefunga goli hilo katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo.

Katika mchezo wa kwanza Simba iliifunga Timu ya Atraco magoli mawili kwa moja na sasa imebakiza mchezo mmoja ambao utaamua majaliwa ya timu hiyo kama itatinga kwenye robo fainali ama itaaga michuano hiyo

PROGRAMU YA MAFUNZO YA UONGOZI KWA JESHI LA POLISI




The IGP and the British High Commissioner, Diane Corner; Picture named (Round-table discussion) shows the British High Commissioner, Diane Corner (right) listening to the IGP and left is an official from DFID.

***************************************************************************************
Wiki hii Balozi wa Uingereza hapa nchini, Diane Corner, pamoja na Inspecta Generali wa Polisi, (IGP) Saidi Mwema wamezindua programu ya mafunzo ya uongozi kwa Jeshi la Polisi la Tanzania inayodhaminiwa na Serikali ya Uingereza. Mafunzo hayo, ambayo yataendeshwa na Mamlaka ya Kitaifa ya Kuboresha Idara ya Polisi ya Uingereza (NPIA) pamoja na ile ya Hampshire kwa muda wa miezi tisa (kuanzia mwezi ujao), yatakuwa na lengo la kubadilishana uzoefu na mbinu bora - kwa kujikita zaidi katika masuala ya kiuongozi na kimenejimenti.

“Mafunzo hayo ni muhimu sana kwetu hasa kwa kipindi hiki cha maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao, lakini pia ni muhimu zaidi katika jukumu zima la kudumisha amani hapa nchini,” alishukuru IGP Saidi Mwema.

Ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mafunzo hayo, hivi karibuni Ubalozi wa Uingereza uliwapeleka kuhudhuria mafunzo huko NPIA na Hampshire nchini Uingereza IGP Saidi Mwema pamoja na maafisa wengine wa Jeshi la Polisi la Tanzania, ambao ni Kamishna wa Polisi anayeshughulikia Utawala na Rasilimali, Clodwig Mtweve, Mkuu wa Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Abdulrahman Kaniki na Kamanda wa Chuo cha Polisi Dar es Salaam, Elice Mapunda.

Ujumbe huo ulipata mafunzo huko NPIA katika masuala ya utekelezaji oparesheni za kipolisi kwa kuzingatia haki za binaadamu, utoaji huduma za kipolisi, uchunguzi, utafiti na masuala mbalimbali ya kiutawala. Pia walipata fursa ya kujiunga na jeshi la Polisi Hampshire na kufanya doria, pamoja na kujenga ujirani mwema na jamii zinazozunguka. Uzoefu huu umewezesha kujenga ushirikiano wa karibu zaidi kati ya Jeshi la Polisi la Tanzania na Hampshire, na hivyo kupanua wigo wa kujifunza kutoka pande zote mbili.

"Ninayo furaha kubwa kuzindua programu hii ya Polisi. Mafunzo haya ni mchango mkubwa katika maboresho ya sekta ya sheria, ambayo sisi pamoja na Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DFID) tunafadhili. Ninatumaini ya kuwa mafunzo haya yatakuza ushirikiano baina ya Jeshi la Polisi la Tanzania na lile la Uingereza ambao kila upande utakuwa na mengi ya kujifunza kutoka kwa mwenzake,” alisema Balozi Corner.
___________________________________________________________________________

Tuesday, May 18, 2010

Uchuuzi wa samaki


Akina mama wachuuzi wa samaki katika ziwa Ndori wilayani Babati, akina mama hawa wanauza samaki mmoja shillingi 100 na wamekuwa wakisubiri ziwani samaki hao mara baada ya kuvuliwa. Picha na Mussa Juma

Monday, May 17, 2010

U.S. and Tanzania Launch Medication Assisted Therapy Program for Drug Users


From right: U.S. Ambassador Alfonso E. Lenhardt, Phillip Marmo, Minister of State in Tanzania's Prime Minister's Office - Coordination & Parliamentary Affairs and U.S. Global AIDS Coordinator Ambassador Eric Goosby - announced the establishment of the first Medication Assisted Therapy (MAT) program for drug users in sub-Saharan Africa. Services will be initiated shortly at a site in Dar es Salaam to be followed by two more sites in Zanzibar and Dar es Salaam. These services are a crucial part of HIV and health services because MAT allows drug users to return to a regular, productive and healthier life. (Photo courtesy of the American Embassy)

Mdau Ernest alamba Nondozzz ya master of IT Project Management


Vincent Ernest akiwa na washikaji zake Stephen Kassambo kushoto na Godwin Meghji wa kulia baada ya kula Nondo zake University of Maryland huko Maryland. Kalamba master of IT Project Management. Jamaa wanakata nondozzz si mchezo hawa Blogu ya Charaz blogspot na timu yake wanamtakia kila la kheri Ernest kwa kula nondozzzz

Rais Kikwete azindua Benjamin William Mkapa Special Economic Zone


Rais Jakaya Kikwete akiwa na Rais mstaafu awamu ya tatu Benjamin William Mkapa wakitembelea baadhi ya maeneo ya ukanda maalumu wa uwekezaji kwaajili ya kuuza nje lijulianalo kama (Benjamin William mkapa Special Economic Zone) huko Mabibi,Ubungo jijini Dar es Salaam, leo asubuhi. Rais Kikwete alifungua rasmi ukanda huo mpya wa uwekezaji (Picha na Freddy Maro)

Sunday, May 16, 2010

Flora Martine ndiye miss IFM 2010


Washiriki wa miss IFM wakijimwaya mwaya jukwaani

Miss IFM 2010,Flora Martin kati na mshindi wa pili Judith Osima (shoto) na wa tatu ni Esther Emmanuel wakiwa wampozi mara baada ya kuibuka kidedea kwenye kinyang'anyiro cha shindano hilo lililokuwa na ushindani mkubwa miongoni mwa washiriki hao.Picha za Silvan Kiwale.

Harambaee ya kuichangia CCM mkoa wa Kilimanjaro yafana


Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Mama Vicky Nsilo Swai akimzawadia Rais Kikwete Ramani ya Afrika yenye kuwaonyesha wanyama watano wakubwa(the big five) Simba,Tembo,Faru, Nyati na Chui muda mfupi baada ya kumalizika hafla ya kuchangia fedha kwaajili ya Uchaguzi Mkuu CCM mkoa wa Kilimanjaro jana jioni katika hoteli ya Golden Tulip jijii Dar es salaam.Katika hafla hiyo Zaidi ya shilingi milioni mia mbili zilipatikana ikiwemi ahadi na fedha taslimu.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Mama Vicky Nsilo Swai akimzawadia Rais Kikwete Ramani ya Afrika yenye kuwaonyesha wanyama watano wakubwa(the big five) Simba,Tembo,Faru, Nyati na Chui muda mfupi baada ya kumalizika hafla ya kuchangia fedha kwaajili ya Uchaguzi Mkuu CCM mkoa wa Kilimanjaro jana jioni katika hoteli ya Golden Tulip jijii Dar es salaam.Katika hafla hiyo Zaidi ya shilingi milioni mia mbili zilipatikana ikiwemi ahadi na fedha taslimu.

Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua harambee ya kuchangia fedha uchaguzi mkuu CCM mkoa wa Kilimanjaro iliyofanyika katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam jana jioni.Picha kwa hisani ya Freddy Maro.

Saturday, May 15, 2010

Kili Music awards

Sean-Kingston performance Sat May 15, 2010 at Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Mrisho mpoto akionesha tuzo yake ya wimbo bora wenye asili ya Kitanzania uitwao nikipata Nauli

Mdau mkubwa wa timu ya Yanga,Bw. Madega akikamkabidhi Diamond tuzo yake ya wimbo bora wa R&B uitwao Kamwambie

Mzee Yusuf akionyesha tuzo yake ya Mtunzi bora wa nyimbo, na pia kundi lake la Jahazi lilinyakua tuzo ya albamu bora ya taarabu iliyoitwa Daktari wa Mapenzi

Gadner Habash akimpongeza mkewe Lady Jay Dee kwa kupata tuzo ya Female Artist of the Year ambayo alipokea kwa niaba.

Thursday, May 13, 2010

Ajali ya ndege yaua 104 Libya


Mabaki ya ndege aina ya Air Bus 330, iliyopata ajali

Maafisa nchini Libya wameripoti kuwa, ndege ya abiria imeanguka katika uwanja wa ndege mjini Tripoli na kuua takriban watu 104.

Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la Afriqiyah ilikuwa safarini kutoka mjini Johannesburg, Afrika Kusini.

Maafisa wamesema ilianguka wakati ikjaribu kutua karibu na uwanja huo.Takriban abiria 93 walikuwa ndani ya ndege hiyo pamoja na wafanyakazi kadhaa wa ndege hiyo aina ya Air Bus 330.

Watu hao wanaaminika kutoka mataifa mbalimbali zikiwemo nchi za Uingereza na Afrika Kusini.Wafanyikazi 11 wa ndege hiyo wameripotiwa kuwa raia wa Libya.

Ndege hiyo ilitarajiwa kuelekea kwenye uwanja wa ndege wa Gatwick mjini London baada ya kusimama kwa muda mjini Tripoli.

Magari ya kuwabebea wagonjwa yameonekana kuelekea kwenye uwanja huo. Shirika la ndege la Afriqiyah lilianzishwa nchini Lybia mwaka wa 2001.

CHANZO: bbcswahili.com

Wednesday, May 12, 2010

Sanamu iliyoibwa Bongo na Waswiss yarejeshwa


Sanamu ya Makonde ambacho kiliibiwa kutoka Makumbusha ya Taifa Dar es Salaam, ilibwa kati ya mwaka 1984-1986 pamoja na baadhi ya mikusanyo ya mila na Sanamu hiyo kilikamatwa nchini Uswisi na hatimaye kurejeshwa hapa nchini.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga akipokea Sanamu hiyo kutoka kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dk.Ladislaus Komba.Kinyago hicho kilikutwa katika makumbusho ya Barbier Murller nchini Switzerland. Sanamu hii ilikabidhiwa nchini Mei 9 2010 na uongozi wa Makumbusho hiyo ya Switzerland

Rais Kikwete mgeni rasmi harambee ya CCM


MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA KILIMANJARO, MAMA NSILO SWAI AKIONGEA KUHUSU HARAMBEE YA KUCHANGIA CHAMA HICHO MKOANI KILIMANJARO ITAKAYAYOFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM (PICHA NA MPIGA PICHA WETU)

********************************************************************************

RAIS Jakaya Kikwete atakuwa mgeni rasmi kwenye chakula cha hisani kuchangia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro itakayofanyika jijini Dar es Salaam kesho.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro Nsilo Swai alisema kuwa harambee hiyo ina lengo la kuchangisha fedha za kugharamia shughuli za uchaguzi mkuu mwaka huu na kuendeleza chama.

Harambee hiyo itafanyika kwenye hoteli ya Golden Tulip ambapo viongozi wa juu wa chama na serikali, wawakilishi wa mashirika wabunge wote wa CCM wa Mkoa wa Kilimanjaro, wakereketwa wa CCM, pamoja na wafanyabiashara wadogo na wakubwa kutoka mkoa wa Kilimanjaro watahudhuria.

Mama Nsilo Swai alisema kuwa harambee hiyo itaanza saa moja usiku ambapo kiingilio itakuwa ni Sh 50,000 kwa mtu mmoja na Sh 60,000 kwa Bibi na Bwana.

“Nawaomba wanaKilimanjaro walioko Dar es salaam na wakereketwa wa Chama Cha Mapinduzi wote kwa ujumla kuhudhuria na kuchangia chama chao”, alisema.

Swai aliongeza kuwa mbali na uchangiaji fedha taslimu pia kutakuwa na mnada wa vitu mbalimbali kama sehemu ya uchangiaji katika shughuli hiyo. Harambee hiyo itapambwa na burudani kutoka kwa bendi ya Msondo Ngoma ya jijini Dar es Salaam.

Two Tanzanians Participate in FORTUNE/U.S. State Department Women's Mentoring Partnership Program


Irene Kiwia, Managing Director of Frontline Management Company, a communication company that deals with public relations, event management and corporate communication and Modesta Mahiga, Managing Director, Professional Approach Limited, a company that deals with human resource capacity building consultancy firm, are in the United States to participate in a four-week FORTUNE/U.S. State Department Global Women's Mentoring Partnership. This program draws on the knowledge and expertise of America’s most accomplished leaders to empower aspiring women professionals across the globe. From left Ms. Mahiga, Ms. Kiwia and Ms. Karen Grissette, U.S. Embassy Deputy Public Affairs Officer at the chancery before their departure. (Photo courtesy of the American Embassy)

Daraja la Umoja lazinduliwa



Rais Jakaya Kikwete na Rais Guebuza wa Msumbiji wakisalimia wanachi katika daraja la Umoja linalounganisha Tanzania na Msumbiji kijiji cha Mtambaswala mkoani Mtwara wakati wa uzinduzi wa daraja hilo mapema leo





Leo marais Jakaya Kikwete na mwenzake Armando Guebuza wa Msumbiji, wamezindua Daraja la Umoja linaloziunganisha nchi hizi mbili kama ishara ya mshikamano na udugu wa kihistoria uliopo baina ya watu wa nchi hizo.

Daraja hilo lenye urefu wa meta 720 na upana wa meta 13.5 ni kiunganishi kizuri kwa nchi hizi na tunatarajia litatumiwa kwa maslahi ya watu wa Tanzania na Msumbiji, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na matatizo ya barabara. Ni ukombozi kwao.

Wazo hilo lililotolewa na marais waasisi; marehemu Julius Nyerere wa Tanzania na Samora Machel wa Msumbiji mwaka 1975 na kutekelezwa na viongozi waliofuata na kukamilishwa na waliopo sasa.

Wazo limesimamiwa na mkandarasi M/s China Geo- Engineering ambaye alisimamiwa na Mhandisi Mshauri NorConsult kutoka Norway, kwa uvumilivu wao na juhudi kubwa za kukamilisha daraja hilo, ambalo litabaki kuwa alama ya uhusiano mzuri na wa kihistoria wa nchi hizi.

Ili kuenzi wazo hili na kuheshimu uamuzi wa kulijenga, ni vizuri sasa wananchi wakawa walinzi wa wenzao, dhidi ya hujuma yoyote itakayofanywa kwenye daraja hilo, hasa hii ya ukataji vyuma kwa ajili ya tamaa ya kujipatia kipato cha haraka haraka.

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...