Dk Kigoda, Zitto kuishtaki NSSF


*WADAI SHIRIKA HILO LINAUZA NYUMBA WANAZOPANGA KWA NJIA YA KIFISADI

Exuper Kachenje

WAPANGAJI zaidi ya 100 wa nyumba za Shirika la Taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF),Tabata jijini Dar es Salaam akiwamo Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zitto Kabwe na Naibu Waziri wa Afya Dk Aisha Kigoda, wameazimia kuliburuza shirika hilo mahakamani kupinga hatua yake ya kutangaza kuuza nyumba wanazoishi bila kuwashirikisha.

Aidha, wapangaji hao wanaowakilisha familia zao zenye watu 500 wameitaka NSSF kusitisha hatua hiyo ndani ya siku saba wakieleza kuwa imewaathiri kisaikolojia.

Hatua ya wapangaji hao wanaowakilisha familia za watu 500 wanaoishi kwenye nyumba hizo za ghorofa maarufu kama 'Tabata Phase II Housing Project' inafuatia mkutano wao walioufanya hivi karibuni.

Zitto na Dk Kigoda ni miongoni mwa wapangaji walioorodhesha majina yao na kusaini barua iliyoandikwa Desemba 10 mwaka huu, kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk Ramadhan Dau baada ya maazimio ya mkutano wao, ambapo nakala yake imepelekwa kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mbunge wa Jimbo la Ukonga Dk Makongoro Mahanga, zilipo nyumba hizo.

Katika mkutano huo wa kujadili hatua hiyo ya NSSF, wapangaji hao walisema wao ni wapangaji halali wenye mkataba unaodumu hadi mwaka 2012.

NSSF ilitangaza zabuni ya kuuza nyumba hizo za ghorofa zilizopo wilayani Ilala kupitia gazeti la Daily News toleo la Desemba 4 na 7 likieleza nia yake ni kuziuza nyumba hizo kwa mteja mmoja.

Baadhi ya wapangaji waliozungumza na Mwananchi walisema, kitendi cha NSSF kutaka kuuza nyumba hizo kwa mtu mmoja kinaonyesha dalili za ufisadi, huku wakieleza kuwa wana fununu kuwa shirika hilo lina mpango wa kuuza nyumba hiyo kwa Mtanzania mmoja mwenye asili ya kiasia.

Wamedai kuwa mtu huyo anayetajwa kuwa NSSF ipo mbioni kumuuzia nyumba hizo zinazokaliwa pia na baadhi ya vigogo, anatajwa katika kashfa mbalimbali za ufisadi nchini.

Baadhi ya vigogo wanaoishi katika nyumba hizo mbali na Zitto na Dk Kigoda ni Jaji Sumari, Balozi mstaafu Nhigula, Habbi Gunze ambaye ni Mkurugenzi wa Utangazazi katika Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA).

Zitto Kabwe, wala Mbunge wa Ukonga hawakupatikana kuzungumzia sakata hilo, lakini naibu Waziri wa Afya Dk Aisha Kigoda alikiri kuwa mmoja wa wapangaji katika nyumba hizo na kueleza kuwa hawezi kupingana na uamuzi uliotolewa katika kikao cha wapangaji kwa kuwa na yeye unamhusu.

“Mimi ni mpangaji kama wengine pale, kama kuna maamuzi yametolewa na kikao au katibu ameandika barua kwenda NSSF au kwingine huo ndio uamuzi wa wapangaji wote,” alisema Dk Kigoda na kuongeza:

Kama ni maamuzi ya kikao hayo ni ‘collective’ (shirikishi), yamekuja kwa niaba ya wapangaji wote, ‘otherwise I have no comment’.”

Mpangaji mwingine Nganga Mlipano aliliambia gazeti hili kuwa hatua hiyo ya NSSF ni kukiuka taratibu, sheria na mkataba baina yao na NSSF hivyo wao kwa umoja wao hawakubaliani na hatua hiyo wakianza mchakato wa kisheria kuupinga na kudai fidia.

"Sisi ni wapangaji wa NSSF, ni kweli, lakini kimsingi unapotaka hata kufanyia marekebisho nyumba zako ni lazima umshirikishe mpangaji wako, kinyume cha hapo ni kuvunja sheria na kumsababishia usumbufu," alisema Mlipano na kuongeza:

"Wote tumekutana, tumejadili na kuandika barua kwenda kwa mkurugenzi wa NSSF nakala tumepeleka kwa Waziri Mkuu na mbunge wetu Makongoro Mahanga tukieleza mambo manne tunayotaka NSSF itekeleze."

Kwa mujibu wa mapendekezo hayo ambayo Mwananchi imeyaona wapangaji hao wanataka NSSF kusitisha mara moja nia yake kuuza nyumba hizo kwa kufuta zabuni iliyotangaza, ikiwa pamoja na kuzuia kufanyika kwa shughuli yoyote inayohusu uuzaji nyumba hizo zenye wapangaji bado.

Pia wameitaka NSSF kuomba radhi bila masharti kwa wapangaji hao kutokana na kuwasababishia matatizo ya kisaikolojia kwa kutangaza zabuni hiyo kinyume cha sheria, na kwamba wapangaji hao wana haki ya kuzuia uuzwaji nyumba hizo kwa kuzingatia sera ya taifa inayozuia uuzaji wa makazi ya watu na kuitaka NSSF kutekeleza mapendekezo hayo kama jambo la dharura ndani ya siku saba.

Comments

Anonymous said…
Amiable post and this mail helped me alot in my college assignement. Thank you for your information.
Anonymous said…
senedou said…
replica bags aaa replica hermes bag l6n81t4j24 replica bags qatar replica bags london blog here w5a41x1z99 replica bags in dubai try here j6t65e3e11 replica ysl bags 7a replica bags