Wednesday, September 30, 2009

Bunge la Jumuiya ya Madola


Rais wa Chama cha Mabunge ya jumuiya Ya Madola Samwel Sitta (kulia) akibadilishana mawazo na Spika wa Bunge la India Meira Kumar (kushoto) jana wakati wa mkutano wa 55 wa CPA unaoendelea mjini Arusha. Wengine ni wajumbe wa mkutano huo kutoka India (katikati)


picha ya Pamoja ya Kamati tendaji ya CPA pamoja na Rais wa Chama hicho Samweli sitta(katikati) na katibu wa Chama cha Mabunge ya jumuiya ya madola Dk William Shija (wa kwanza kushoto waliosimama). Kamati hiyo inahudhuria mkutano unaoendelea mjini Arusha. Picha zote na Anna Itenda - Maelezo- Arusha.

Rais akutana na Spika wa Bunge la Marekani


President Kikwete and his delegation during as meeting with the speaker of the House of Representatives Nancy Pelosi at her Capitol Hill office in Washington DC yesterday(photos by Freddy Maro)

President Jakaya Mrisho Kikwete with the Speaker of the House of Representatives of the USA Nancy Pelosi in her office at Capitol Hill, Washington DC yesterday. President Kikwete held talks with the speaker on bilateral issues.

Tuesday, September 29, 2009

Serikali yanunua jengo la Ubalozi Washington




RAIS Jakaya Kikwete juzi alifungua jengo jipya la ofisi za ubalozi wa Tanzania mjini Washington DC lililonunuliwa kwa dola 10.415 za Kimarekani (sawa na Sh13.5 bilioni za Kitanzania).
Akihutubia wakati wa sherehe za ufunguzi, Rais Kikwete alisema jengo hilo pia ni ishara ya kisiasa na kidiplomasia ya kukua kwa uhusiano baina ya Tanzania na Marekani.
Rais Kikwete aliwaambia mabalozi wa nchi mbalimbali, maofisa wa serikali ya Marekani na viongozi wa asasi mbalimbali za kimataifa kwamba uhusiano wa Tanzania na Marekani haujawahi kuwa mzuri kama ilivyo sasa.
Rais Kikwete, ambaye pia aliishukuru Marekani kwa kuunga mkono juhudi za Tanzania katika kupambana na umaskini na magonjwa, alisema mahitaji ya sasa yameilazimisha serikali kutafuta jengo kubwa zaidi.
Akizungumza wakati wa kumkaribisha Rais Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema jengo hilo ndilo kubwa kuliko majengo yote ya balozi za Tanzania duniani.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Ombeni Sefue alisema jengo hilo la ghorofa sita lina eneo la futi za mraba 26,240 na litagharimu dola 367,593.54 za Kimarekani (sawa na Sh477 milioni za Kitanzania) kulitunza kwa mwaka. Imeandikwa na
Mobhare Matinyi, Washington DC, Picha imepigwa na Freddy Maro wa Ikulu.

Monday, September 28, 2009

Raila meets Obama in US tour


President Barack Obama and First Lady Michelle Obama pose for a photo during a reception at the Metropolitan Museum in New York with, Kenya Prime Minister Raila Odinga and his wife Ida on September 23, 2009. Photo/WHITE HOUSE

Kipanya leo

MAMA MARIA NYERERE ALONGA NA WANAHABARI LEO!!




Mjane wa baba wa Taifa mama Maria Nyerere akiongea na wanahabari nyumbani kwake msasani jijini leo, wakati alipotoa taarifa juu ya tuzo aliyoipokea kwa niaba ya Marehemu Malimu J.K.Nyerere kutoka kwa rais wa balaza kuu la umoja wa mataifa katika kutambua mchango wake kwa nchi za bara la Afrika, kushoto ni mtoto wake Makongaro Nyerere.

Wanafunzi Kibasila watoa kali ya mwaka





ZAIDI ya wanafunzi 2,600 wa Shule ya Sekondari ya Kibasila jijini Dar es Salaam jana walifunga barabara za Mandela na Chang’ombe kwa zaidi ya saa tano na kusababisha msongamano mkubwa wa magari.

Wanafunzi hao waliendesha operesheni hiyo kuzuia magari kupita baada ya kukaa kwenye makutano ya barabara hizo mbili, wakiishinikiza serikali iweke matuta eneo hilo ambalo limekuwa na ajali nyingi tangu Barabara ya Mandela ifunguliwe kiasi cha kupachikwa jina la Machinjioni.

Ajali hizo, zikiwemo zilizotokea mwishoni mwa wiki iliyopita, zimekuwa zikichukua roho za watu wengi, na hasa wanafunzi wa shule hiyo inayopakana kwa upande mmoja na Barabara ya Mandela na upande mwingine Barabara ya Chang’ombe.

Wanafunzi hao walifunga barabara hiyo kuanzia saa 3:00 asubuhi na magari ambayo yalijaribu kupita kwa nguvu yalirushiwa mawe na vioo vya baadhi ya magari vilivunjwa.

Wakati wakiendelea kuyarushia mawe magari hayo, baadhi walikuwa wakiimba nyimbo za kutaka Mkuu wa Mkoa, William Lukuvi aende eneo hilo na kutoa ufumbuzi wa haraka kuhusu ajali hizo.

"Hatudanganyiki, tunamtaka mkuu wa mkoa," walisikika wanafunzi hao wakiimba.

Tanzania yaichapa Lesotho 33-19







WENYEJI wa michuano ya kimataifa ya netiboli 'Inter Nations Netball Tournament' Tanzania jana waliisambaratisha Lesotho kwa mabao 33-19 katika mchezo wa ufunguzi uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Tanzania iliyotawala mchezo huo tangu mwanzo, walikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 19 dhidi ya 8, huku Monica Kessy 'GS' ndiye aliyekuwa nguzo ya Tanzania katika robo ya kwanza kwa kuwaongoza kushinda mabao 11 dhidi ya matano (5) ya Lesotho.

Kuingia kwa Neema Emmanuel mchezaji wa timu ya taifa ya mpira wa kikapu, volleyball na mpira wa mikono aliyechukua nafasi ya Anges Simkonda 'GA' kuliongeza nguvu kwenye kikosi cha Tanzania.

Hadi robo ya tatu inamalizika Taifa Queens walikuwa mbele kwa mabao 25 -14 ya Lesotho. Mabao ya wageni yalifungwa na Maresenyeho 'GS' na Thato Lelehoane 'GA'. Habari imendikwa na Jesca Nangawe na Picha kupigwa na Michael Matemanga wote wa Mwananchi.

Hebu nipe tofauti kati ya shule zetu na zao





Kuna tofauti kubwa saana kati ya shule zetu na zao hebu angalia shule zetu zilivyo na kisha uhusianishe na shule zao, miundombinu tofauti, vifaa vya kufundishia tofautio, mbinu za ufundishaji ndo usiseme, yaani basi hata majina yanakatiosha tamaaa, hivi watoto wanaotoka katika shule hizi zao la mwisho ni lipi litakaloongoza taifa, jibu unalo mwenyewe hebu nambie.

Thursday, September 24, 2009

Michezo ya watoto


Michezo ya watoto bwana inashangaza, wanaweza kufanya michezo ya hatari mpaka ukashangaa, hebu angalia hawa watoto wa Dar es Salaam wanavyoogelea kwenye mto mchafu, kemikali zimemwagwa humoo hakuna usalama, lakini watoto wanajimwaga mto Msimbazi ni hatari tupu.

Utata waibuka kesi ya Mramba, Yona



MAWAKILI upande wa utetezi katika kesi ya kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh 11 bilioni, inayomkabili Waziri wa zamani wa Wizara ya Fedha, Basil Mramba na wenzake, wamekana kuutambua waraka namba mbili wa mwaka 1999 wa aliyekuwa Jaji Mkuu, Francis Nyarali.

Jopo hilo, la mawakili liliukataa waraka huo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam mbele ya jopo la mahakimu watatu, lililokuwa likongozwa na Hakimu, John Lutamwa wakati kesi hiyo, ilipokuja kwa ajili ya usikilizaji wa awali.

Mawakili hao, waliukataa waraka namba mbili wa mwaka 1999 ambao unautaka upande wa utetezi kutaja idadi ya mashahidi wao kabla ya upande wa mashtaka kuanza kutoa ushahidi wao na mahakama kuthibitisha kama washtakiwa wana hatia au la, kwa madai kuwa ulitengenezwa kinyume cha sheria.

Wakili wa Mramba, Hurbert Nyange alidai kwa heshima na taadhima kifungu cha sheria cha 192, kifungu kidogo cha nne cha mwenendo wa kesi za jinai, mwenye mamlaka ya kutengeneza taratibu za kisheria ni Waziri wa Sheria akishauriana na Jaji Mkuu.

“Ni rai yangu kuwa sheria yoyote ambayo imetengenezwa chini ya kifungu hiki, lazima itangazwe kwenye gazeti la serikali," alidai Nyange.

Alidai waraka huo, hauonyeshi ni lini utaanza kutumika na kwamba kama kweli hiyo ni sheria haikutengenezwa chini ya mamlaka husika.

Alidai anaiheshimu nafasi ya jaji mkuu ya kutoa miongozo ya sheria kuhusiana na mienendo ya kesi na kwamba kama wakili na ofisa wa mahakama anawajibu wa kufikia maamuzi kwa misingi ya kisheria.

“Kwa heshima kubwa mbele ya mahakama nimeangalia karatasi ya Mei 5,1999 ambayo ni ya Jaji Mkuu, mwisho nikaona haina saini ya aliyekuwa Jaji Mkuu marehemu Francis Nyarali hivyo nina wasiwasi nayo,” alidai Nyange.

Alidai kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha 231 cha Mwenendo wa Mashauri ya Jinai mtuhumiwa anapaswa kueleza idadi ya mashahidi wake hadi hapo upande wa mashtaka utakapofungua kesi yao na mahakama kumuona ana hatia.

Wednesday, September 23, 2009

Three men to hang for Tanzania albino murder

Tanzania's high court on Wednesday sentenced three men to hang for the murder of a 13-year-old albino boy, killed for his body parts in the country's northwest, local media and a rights group said.

At least 53 albinos have been killed since 2007 in the east African nation and their body parts sold for use in witchcraft, especially in the remote northwest regions of Shinyanga and Mwanza where superstition is rife.

Witchdoctors say the body parts of albinos -- who lack pigment in their skin, eyes and hair -- bring luck in love, life and business. One of the accused was found with two legs belonging to the deceased, Matatizo Dunia, local radio said.

Canadian albino rights group, Under The Same Sun, welcomed the court's decision but noted that this was just one judgment out of 53 deaths.

"This is one conviction. There are 52 other families still awaiting justice," Peter Ash, the group's founder and director, told Reuters by telephone from London.

The government has opened at least 15 cases against suspects involved in the killings, in which body parts like hair, genitals, arms and legs are taken for use by witchdoctors.

Authorities have arrested more than 90 people, including four police officers, for their involvement in the murders or trade of albino body parts.

The killings have sullied Tanzania's reputation for relative calm in the region, and drawn condemnation from the United Nations and European Union. Continued...

Gadafi atoa kali ya mwaka UN


NEW YORK, Marekani
Kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi amehutubia mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa wa kila mwaka akasema kuwa Umoja huo wa mataifa hauko fair kwanza unajali nchi tajiri kuliko masikini, unasimamia mambo ya ajabu, vita 65 vimeshatokea bila ya idhini ya UN. Kama mzaha vile akatishia kutaka kuchana charter ya UN.

Anasema Marekani wala siyo sehemu nzuri, ni kama vile jela ya Guantanamo, sababu kuna mikwala mingi ili kuingia
kwanza daktari wake kanyimwa viza, halafu alikwenda na ndege zake tatu lakini wakamlazimisha aongezewe rubani mmoja wa akiba wa ndege yake wakati yeye anao marubani wataalamu.

Kisha ametaka mataifa tajiri yaziheshimu nchi masikini na pia hatua kali zichukuliwe kwa mataifa yanayokiuka
alipofika Marekani amekataa kupangiwa katika hoteli yoyote ile badala yake ametafuta sehemu akasimika mahema yake, marekani imemkatalia.

Sasa anataka Afrika ipewe kiti cha kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Anapinga kabisa mfumo uliopo wa Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa.

Tayari Rais Barack Obama wa Marekani ameshahutubia UN na ameitaka Jumuiya ya Kimataifa kujihusisha kwa vitendo, akisema Marekani pekee yake haiwezi kutatua migogoro na changamoto zote zinazoukabili ulimwengu.

Akizungumza katika hotuba yake ya kwanza katika kikao cha mkutano wa baraza kuu la umoja wa Mataifa mjini New York, Obama alisema wenye uzoefu wa kuitia adabu Marekani kwa madai ilibeba mzigo wa ulimwenguni pekee yake, wakati huu hawawezi kukaa kando wakisubiri Marekani itatue matatizo yote ya ulimwengu.

Obama alitoa mfano wa hali mbaya ulimwengu utajikuta iwapo jumuiya ya kimataifa haitoshirikiana kutatua matatizo mengi. Rais huyo wa Marekani alisema kuna uwezekano wa makundi yenye siasa kali kuongezeka, vita na mizozo kuzidi, pamoja na mauaji ya halaiki.

Swala la nchi nyingi kujipatia silaha za nuklia, ongezeko la ujoto duniani kufuatia mabadiliko ya hali ya hewa, umaskini na kuongezeka kwa maradhi pia ni mifano Obama ilitoa endapo jumuiya ya kimataifa haitashikana mikono kushirikiana. Kiongozi wa Libya Kanali Muammar Ghadaffi pia alikihutubia kikao hicho cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza.

Tuesday, September 22, 2009

BASI LAWAKA MOTO SINGIDA







AJALI NYINGINE YA MOTO BASI LA ABIRIA KUTOKA SINGIDA KWENDA DODOMA LILIPATA HITILAFU YA UMEME NA KUWAKA MOTO.
MOTO HUO KWA BAHATI NJEMA ABIRIA WALIKUWA CHINI WAKICHIMBA DAWA LAKINI DEREVA ALIKUWA AKICHUNGULIA CHANZO CHA MOTO, NDIPO TAIRI HILO LILIPOPASUKA NA KUMJERUHI MACHONI DEREVA WA BASI HILO NA KUKIMBIZWA HOSPITALI YA MANYONI
KWA MATIBABUZAIDI.

POLISI WALIFIKA KWA KUCHELEWA INGAWA SIMU ZILIPIGWA MAPEMA MNO. NA
AHATA POLISI WALIPOFIKA WALIKUWA WAMESHEHENA SILAHA KALI BILA HATA NDOO
YA KUSAIDIA KUZIMIA MOTO HUO.

PICHA ZAIDI KWA HISANI YA MDAU EMMANUEL MGONGO

Waziri Nchimbi ziarani Lebanon, Yerusalem


Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Emmanuel Nchimbi, akiwa ziarani Lebanon ambapo alikwenda kujionea mwenyewe operesheni za ulinzi wa amani zinavyofanyika huko na hapa anaonekana akitembelea eneo mwamba ambao alijipumzisha Yesu enzi zile akisambaza neno la Mungu.

Hapa ni eneo ambapo Nabii Mussa aliweza kuonyesha muujiza baada ya kuchapa fimbo jangwani na maji yakatiririka, maji haya yanatiririka hadi leo hii kama unavyoona katika bomba.



Nchimbi akikagua kombania ya vikosi vya Umoja wa Mataifa vya kulinda amani nchini Lebanon.Picha kwa hisani ya Wizara ya Ulinzi.

Sunday, September 20, 2009

Eid el Fitr



Baadhi ya waumini wa Kiislam wakiswali swala ya Idd jana asubuhi katika msikiti wa Gadaffi mjini Dodoma jana. Picha na Jube Tranquilino.

Miss Tanzania waahidi nidhamu mtindo mmoja




Warembo wanaowania taji la Vodacom Miss Tanzania wameahidi kuonyesha nidhamu na kufuata maelekezo ya walezi wao  katika kipindi chote hiki walichopo kambini.
 
Wakizungumza baada ya kutembelewa na ndugu na jamaa zao katika kambi yao iliyoko katika hoteli ya Girrafe walisema kwamba wao wanaamini kwamba siku zote nidhamu ndiyo silaha kubwa ya mafanikio.
 
"Kwa kweli tutajitahidi kuwa na nidhamu ili tuweze kufanikisha malengo yetu ya kuwa mfano bora katika jamii," anasema Evelyn Gamasa mrembo kutoka Kanda ya Ilala.
 
Warembo hao wamemaliza ziara yao ya kutembelea vivutio vya utalii katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro na kufuatia ziara hiyo wamesema wamejifunza mengi kuhusu sekta ya utalii.
 
Wakizungumzia ziara hiyo wamesema wamebaini kwamba Tanzania ni nchi iliyobarikiwa na Mungu kuwa na vivutio vya kipekee Duniani na kwamba kama vitatumiwa ipasavyo vinaweza kuboresha maisha ya Watanzania wengi hasa kwa upande wa sekta ya ajira.
 
Kwa upande wao baadhi ya wazazi wameonyesha kufurahishwa na jinsi mdhamini wa shindano hilo Vodacom Tanzania anavyowasaidia vijana nao.
 
Wamesema mdhamini huyo amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kwamba maisha ya Watanzania wengi yanaboreka hasa kwa upande wa ajira.
 
"Kwa kweli mdhamini huyu Vodacom anastahili sifa, amewaweka vijana wetu katika hoteli nzuri na pia kuwapatia huduma bora, hii inatupa moyo," anasema mmoja wa wazazi hao.
 
Wazazi wamesema kwamba pia zawadi zinazotolewa na Vodacom ni nzuri na kwamba zinasaidia kuboresha maisha ya vijana wao.
 
Fainali ya Vodacom Miss Tanzania itafanyika tarehe mbili mwezi ujao na mshindi wa kwanza atapata zawadi ya gari Suzuki Grand Vitara lenye thamani ya sh. milioni 53 na fedha taslim shilingi milioni tisa.

Wednesday, September 16, 2009

Msafiri kafiri


Wasafiri wanaotumia usafiri wa shirika la Reli nchini (TRC) wakiwa wamekwama katika stesheni ya mkoa wa Morogoro wakati wakisubiria usafiri wa kwenda mikoa ya bara baada ya treni ya mizigo kuanguka katika Kijiji cha Msua na Kwala mkoani Pwani treni hiyo ilikuwa likitokea Dar es Salaam.Picha na Juma Mtanda

Tuesday, September 15, 2009

Pumzika kwa amani mpakanjia




Marafiki,ndugu na jamaa wakiwa wamejumuika makaburi ya kisutu Upanga leo mchana wakisubiri mwili wa marehemu kuwasili sehemu ya maziko.

Ufisadi mpya BoT


VIGOGO wanne wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na shtaka la Uhujumu Uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh104 bilioni.

Vigogo hao ambao wote ni wakurugenzi wa BoT wa vitengo tofauti, walifikishwa mahakamani hapo asubuhi chini ya ulinzi mkali wa polisi.

Wameshtakiwa chini ya Sheria ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 2002.

Wakurugenzi hao wanashtakiwa kwa makosa tofauti ikiwamo kosa la tatu linalowahusisha wote wanne ambao ni Mkurugenzi wa Benki ya BoT, Simon Eliezer Jengo, Naibu Mkurugenzi wa Fedha wa benki hiyo Kisima Thobias Mkango, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Bosco Ndimbo Kimela na Mkurugenzi wa benki, Ally Farijallah Bakari.

Mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Benny Lincon alimwambia hakimu Samuel Maweda kuwa vigogo hao wanne, wakiwa watumishi wa umma walitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti na kuisababishia serikali hasara ya Sh104,158,536,146.

“Kwa pamoja na kwa makusudi walishindwa kuchukua tahadhari au kusahau majukumu yao katika mazingira nyeti, kwa udanganyifu walitayarisha nyongeza kwenye mkataba wa 2001 unaohusiana na uchapaji wa noti za benki kwa gharama kubwa ambapo bei ya mkataba huo iliisababishia serikali hasara ya Sh104,158,536,146,” alidai Licon.

Licon aliendelea kuieleza mahakama kuwa mwaka 2004 washtakiwa Jengo na Mkango wakiwa ndani ya jiji na Mkoa wa Dar es Salaam na wakiwa wameajiriwa katika utumishi wa umma katika nyadhifa tofauti ndani ya BoT, kwa pamoja na kwa makusudi, wakiwa na lengo la kuvunja kanuni walitangulia kutoa ofa kwa wasambazaji wa noti za benki.Pauline Richard na Salim Said.

WAZIRI MKUU AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA INDIA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa India, S. M. Krishna kabla ya mazungumzo yao kwenye jumba la Hyderabad jijini New Delhi,leo mchana. Pinda yuko India kwa ziara ya kikazi.

Pinda akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa India, S. M. Krishna kabla ya mazungumzo yao kwenye jumba la Hyderabad jijini New Delhi, leo.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Makamu wa Rais wa India, M. Hamid Ansari kwenye Ofisi ya Makamu huyo wa Rais, jijini New Delhi akiwa katika ziara ya Kikazi nchini India.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Makamu wa Rais wa India, M. Hamid Ansari, ofisini kwa makamu huyo wa Rais jijini New Delhi , akiwa katika ziara ya kakazi nchini India , Septemba 15, 2009. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Ajali ya treni




Lori la kubeba mchanga likiwa limeharibika vibaya baada ya kugongwa na treni ya mizigo katika eneo la Makulu mjini Dodoma jana baada ya lori hilo kukatiza reli sehemu ambayo haina kivuko. Hakuna aliyereruhiwa katika ajali hiyo. Picha na Jube Tranquilino

Monday, September 14, 2009

Mchungaji kizimbani kwa mauaji


Mchungaji wa kanisa la e Winners' Chapel, Denis Mlazi, akisindikizwa kuingia kwenye chumba cha mahakama ya Temeke leo akikabiliwa na mashtaka ya kumuua mkewe, Rosemary Munseri.

DC ajeruhiwa katika fumanizi

MKUU wa Wilaya ya Tunduru Juma Madaha ameumizwa vibaya kichwani baada ya kushambuliwa sehemu mbali mbali za mwili wake  na kusukumwa katika fumanizi lililotokea katika hoteli ya Angorn Arms Mjini Songea.

Akizungumza na Mwananchi jana wakati wa kikao cha kwanza cha kamati ya mkoa  ya usimamizi wa pembejeo  Mkuu huyo amesema, tukio hilo limetokea jana usiku majira ya saa nne wakati akiwa katika chumbani alichopanga  no 102 katika hoteli hiyo alivamiwa na kundi la watu wakiwemo waandishi wa habari na kumtaka afungue mlango na alipofungua walianza kumpiga na kumvua nguo na kumwacha akiwa uchi wa mnyama huku wakimpiga picha za utupu.

Anasema, chanzo cha tukio hilo ambalo yeye ameliita ni la ujambazi ni wivu uliotokana na mwandishi mmoja wa habari kukataliwa, anasema akiwa chumbani humo na mwanamke ambaye anadaiwa kuwa naye ni mwanahabari alishitukia akipigwa na kuvuliwa nguo.
Alisema, katika vurugu hizo amepoteza pesa taslimu Sh laki mbili, simu ya mkononi aina ya Nokia namba N78 yenye thamani ya shilingi laki tano pamoja na pete yake ya ndoa.

"Tukio hilo limetokana na wivu kwani kuna mwandishi wa habari niliwahi kuwa na mahusiano naye siku za nyuma na baada ya kumwacha ameingiwa na wivu na kuamua kunifanyia vurugu hata hivyo nimesharipoti tukio hilo katika vyombo vya usalama nasubiri   hatua za kisheria zifuate mkondo wake,"alisema DC huyo.

Alisema watu hao walimshambulia  kwa makusudi na hawakufata taratibu zozote za uongozi wa hoteli, wala kumchukua mwenyekiti wa serikali za mtaa ndiyo maana analichukulia swala hilo kama ni ujambazi kwani wamefanyia ukatili kuingia katika chumba chake na kumshambulia.Habari ya Joyce Joliga, Songea.

Mpakanjia aaga dunia



MOHAMED Mpakanjia, ambaye alikuwa mume wa mbunge viti maalum kwa tiketi ya CCM, marehemu Amina Chifupa, amefariki dunia ikiwa ni takriban miaka miwili tangu mkewe aage dunia.

Mpakanjia, ambaye alikuwa mfanyabiashara maarufu jijini Dar es salaam, alifariki dunia jana alasiri akiwa hospitali ya Lugalo jijini Dar es salaam inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi (JWTZ).

Kifo cha Mpakanjia kimetokea takribani miaka miwili na miezi kadhaa tangu mkewe Amina Chifupa, ambaye aliibukia kwa nguvu kwenye siasa na kuzimika ghafla, kufariki dunia katika hospitali hiyo Juni 27, 2007 baada ya kusumbuliwa na homa ya kisukari na malaria.

Habari kutoka kwa watu wa karibu na marehemu zinasema kuwa Mpakanjia, ambaye alikuwa akimiliki alifikishwa katika hospitali ya Lugalo juzi usiku baada ya kusumbuliwa na homa ya Pneumonia.

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...