MKUU wa Wilaya ya Tunduru Juma Madaha ameumizwa vibaya kichwani baada ya kushambuliwa sehemu mbali mbali za mwili wake na kusukumwa katika fumanizi lililotokea katika hoteli ya Angorn Arms Mjini Songea.
Akizungumza na Mwananchi jana wakati wa kikao cha kwanza cha kamati ya mkoa ya usimamizi wa pembejeo Mkuu huyo amesema, tukio hilo limetokea jana usiku majira ya saa nne wakati akiwa katika chumbani alichopanga no 102 katika hoteli hiyo alivamiwa na kundi la watu wakiwemo waandishi wa habari na kumtaka afungue mlango na alipofungua walianza kumpiga na kumvua nguo na kumwacha akiwa uchi wa mnyama huku wakimpiga picha za utupu.
Anasema, chanzo cha tukio hilo ambalo yeye ameliita ni la ujambazi ni wivu uliotokana na mwandishi mmoja wa habari kukataliwa, anasema akiwa chumbani humo na mwanamke ambaye anadaiwa kuwa naye ni mwanahabari alishitukia akipigwa na kuvuliwa nguo.
Alisema, katika vurugu hizo amepoteza pesa taslimu Sh laki mbili, simu ya mkononi aina ya Nokia namba N78 yenye thamani ya shilingi laki tano pamoja na pete yake ya ndoa.
"Tukio hilo limetokana na wivu kwani kuna mwandishi wa habari niliwahi kuwa na mahusiano naye siku za nyuma na baada ya kumwacha ameingiwa na wivu na kuamua kunifanyia vurugu hata hivyo nimesharipoti tukio hilo katika vyombo vya usalama nasubiri hatua za kisheria zifuate mkondo wake,"alisema DC huyo.
Alisema watu hao walimshambulia kwa makusudi na hawakufata taratibu zozote za uongozi wa hoteli, wala kumchukua mwenyekiti wa serikali za mtaa ndiyo maana analichukulia swala hilo kama ni ujambazi kwani wamefanyia ukatili kuingia katika chumba chake na kumshambulia.Habari ya Joyce Joliga, Songea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment