Monday, September 28, 2009

Tanzania yaichapa Lesotho 33-19







WENYEJI wa michuano ya kimataifa ya netiboli 'Inter Nations Netball Tournament' Tanzania jana waliisambaratisha Lesotho kwa mabao 33-19 katika mchezo wa ufunguzi uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Tanzania iliyotawala mchezo huo tangu mwanzo, walikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 19 dhidi ya 8, huku Monica Kessy 'GS' ndiye aliyekuwa nguzo ya Tanzania katika robo ya kwanza kwa kuwaongoza kushinda mabao 11 dhidi ya matano (5) ya Lesotho.

Kuingia kwa Neema Emmanuel mchezaji wa timu ya taifa ya mpira wa kikapu, volleyball na mpira wa mikono aliyechukua nafasi ya Anges Simkonda 'GA' kuliongeza nguvu kwenye kikosi cha Tanzania.

Hadi robo ya tatu inamalizika Taifa Queens walikuwa mbele kwa mabao 25 -14 ya Lesotho. Mabao ya wageni yalifungwa na Maresenyeho 'GS' na Thato Lelehoane 'GA'. Habari imendikwa na Jesca Nangawe na Picha kupigwa na Michael Matemanga wote wa Mwananchi.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...