Tuesday, September 29, 2009
Serikali yanunua jengo la Ubalozi Washington
RAIS Jakaya Kikwete juzi alifungua jengo jipya la ofisi za ubalozi wa Tanzania mjini Washington DC lililonunuliwa kwa dola 10.415 za Kimarekani (sawa na Sh13.5 bilioni za Kitanzania).
Akihutubia wakati wa sherehe za ufunguzi, Rais Kikwete alisema jengo hilo pia ni ishara ya kisiasa na kidiplomasia ya kukua kwa uhusiano baina ya Tanzania na Marekani.
Rais Kikwete aliwaambia mabalozi wa nchi mbalimbali, maofisa wa serikali ya Marekani na viongozi wa asasi mbalimbali za kimataifa kwamba uhusiano wa Tanzania na Marekani haujawahi kuwa mzuri kama ilivyo sasa.
Rais Kikwete, ambaye pia aliishukuru Marekani kwa kuunga mkono juhudi za Tanzania katika kupambana na umaskini na magonjwa, alisema mahitaji ya sasa yameilazimisha serikali kutafuta jengo kubwa zaidi.
Akizungumza wakati wa kumkaribisha Rais Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema jengo hilo ndilo kubwa kuliko majengo yote ya balozi za Tanzania duniani.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Ombeni Sefue alisema jengo hilo la ghorofa sita lina eneo la futi za mraba 26,240 na litagharimu dola 367,593.54 za Kimarekani (sawa na Sh477 milioni za Kitanzania) kulitunza kwa mwaka. Imeandikwa na
Mobhare Matinyi, Washington DC, Picha imepigwa na Freddy Maro wa Ikulu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment