Tuesday, September 15, 2009

WAZIRI MKUU AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA INDIA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa India, S. M. Krishna kabla ya mazungumzo yao kwenye jumba la Hyderabad jijini New Delhi,leo mchana. Pinda yuko India kwa ziara ya kikazi.

Pinda akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa India, S. M. Krishna kabla ya mazungumzo yao kwenye jumba la Hyderabad jijini New Delhi, leo.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Makamu wa Rais wa India, M. Hamid Ansari kwenye Ofisi ya Makamu huyo wa Rais, jijini New Delhi akiwa katika ziara ya Kikazi nchini India.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Makamu wa Rais wa India, M. Hamid Ansari, ofisini kwa makamu huyo wa Rais jijini New Delhi , akiwa katika ziara ya kakazi nchini India , Septemba 15, 2009. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...