Tuesday, September 08, 2009

Mbunge aswekwa rumande kwa shambulizi


 
JESHI la Polisi Mkoani Morogoro linamshikilia mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini-Mashariki, Samir Lotto kwa tuhuma za kumshambulia na kumpora vifaa vya kazi mfanyakazi mmoja wa Mamlaka ya Maji safi na Majitaka Manispaa ya Morogoro (Moruwasa).
 
Mbunge huyo alikamatwa jana saa 6:00 mchana katika eneo la nyumba yake ya ghorofa anayojenga kando ya barabara ya zamani ya Dar es salaam.

Mbunge huyo alikamatwa baada ya kudaiwa kukaidi wito wa polisi wa kufika Kituo Kikuu cha Polisi kutoa maelezo dhidi ya shtaka la shambulio lililofunguliwa Agosti 20 na mfanyakazi huyo wa Moruwasa, Michael Mapunda katika jalada namba MO/RB/8186/09.

Kamanda wa polisi mkoani Morogoro,Thobias Andengenye aliliambia gazeti hili jana kuwa mbunge huyo atafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya upelelezi wa tuhuma zinazomkabili, kukamilika.

"Kweli tunamshikilia Mheshimiwa Lotto na sasa maelezo yake yanachukuliwa na kama ambavyo mnajua tumekuwa tukimtafuta pasipo mafanikio; askari wameshakwenda kwake mara nyingi na kumkosa na mara nyingi huelezwa kuwa amesafiri  nje ya nchi. Pamoja na kwamba mbunge hana kinga juu ya hilo, tunachokifanya sisi ni kusimamia sheria za nchi," alisema Andengenye.

Inadaiwa kuwa Agosti 20 majira ya saa 6:00 mchana, mbunge huyo alimzaba vibao mfanyakazi huyo na kumkaba koo na baadaye kumnyang'anya vifaa vya kazi na Sh150,000 zilizokuwa kwenye makabrasha. Samuel Msuya na Lilian Lucas Morogoro

2 comments:

Anonymous said...

ninyi wabongo hamwishi kuchagua viongozi wadosi kwani hao wana kiburi cha tambuu kenya wenzenu hawawapi nafasi wadosi

Anonymous said...

safi sana we mwarabu koko waruguru wamelala mna watu wasomi wa kiruguru kibao nafasi hamuwapi mnaishia ufisadi wape mbata sana ndio maana nimewakimbia.

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...