Monday, August 17, 2009

Zombe Huru





Hukumu iliyosomwa na Jaji Salum Masati iliyochukua takribani masaa sita, leo katika Mahakama Kuu ya Tanzania imewaachia huru watuhumiwa wote saba katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini na dereva taksi mmoja, iliyokuwa ikiwakibili aliyekuwa Afisa upelelezi wa mkoa wa Dar es Salam Abdallah Zombe na wenzake.

Zombe na wenzake walikuwa wanatuhumiwa kwa kosa la kufanya mauaji kwa kukusudia Sabinus Chigumbi, maarufu kama Jongo na ndugu yake Ephrahim Chigumbi na Mathias Lunkombe ambao ni wafanyabiashara wa Mahenge.

Mwingine ni dereva teksi wa Manzese jijini Dar es salaam, Juma Ndugu. Akisoma hukumu hiyo JAJI Masati amesema kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaonesha kuwa watuhumiwa hao walihusika katika kufanya mauaji ya wafanyabiashara hao.

Hivyo Mahakama haikuweza kuwatia hatiani. Watu wengi wali waliokuwepo Mahakamani wameonesha kutoridhishwa na hukumu hiyo, hali ambayo inabakisha kitendawili juu ya hatima ya maisha ya waliokua watuhumiwa katika kesi hiyo wakiwa uraiani.

1 comment:

SEDOUF said...

DEREVA ALIYEPATA AJALI AFUNGWA ZAIDI YA MIAKA 25.
WAUAJI WANAOTOA ROHO ZA WATU KWA MAKUSUDI WANAANCHIWA HURU.
HII NDIO HALI HAPA KWETU