Saturday, August 08, 2009
Tabora Boys duhhh
Mwanakijiji mwenzetu ametutumia hii picha akitukumbusha enzi zile tukiwa tunasoma katika shule yetu ya zamani maarufu kama Berlin, Tabora Boys imekuwa maarufu kwa kutoa vipaji vingi sababu ilikuwa shule ya watoto wa machifu, lakini baadaye ikawa ya vipaji maalumu na kisha inakumbukwa kwa kutoa makamanda wengi katika geshi letu la Tanzania (JWTZ), hebu cheki hili bweni pale karibu kabisa na bwalo na kisha kwa sasa inavyoonekana kwenye geti la kuingilia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
12 comments:
Cherahani..You rocky...u remind those days back @ Tabora School fighting with Afande Chacha...'''''Mi na mihela bwana" na afande Pita....hahaha was fun..big up bro...
Sure kaka nakumbuka saana mambo ya afande chacha na afande Warioba watu hawa ni watu ambao si rahisi kuwasahau, lakini pia yupo Afande Peter majasho, nakumbuka alisema siku moja kitu cha ajabu kaona dictionary ndogo unakumbuka alisemaje "Kakitabu haka ni kazuri, kana maneno mafupimafupi , lakini matamu."
ahh umenikumbusha mbali sana, 1975 hadi 1980, Msaki (Kamishina wa elimu mstahafu), Kusila(mbunge wa Bahi) Na Ndeki. Wote walikuwa waalimu wakuu wangu kwa vipindi tofauti, bila ya kumsahau mwalimu wa siasa Tarimo (sasa Rc.Jamani nani anajua alipo mwalimu wa hesabu aitwae Mwakyembe?
hahahha we acha tu noma.hiyo safi sana ...Tabora Boys bwana..wazee wa warsal na mirambo kupigania mademu wa Tabora girls......
TABORA SCHOOL ILIJULIKANA KAMA KICHWA CHWA TANGANYIKA HUKU SAINT MARY'S IKINGARA KWA BENDI YA MATARUMBETA.
KWA WALE WAENZI HIZO WATAMKUMBUKA HEADMASTER MZUNGU BWANA CRABLE. NA MWALIMU HARUBU AMBAY BAADAYE ALIUKWA CHAIRMAN WA EAC.
Mimi nimesoma Tabora Boys siku za hivi karibuni namkumbuka headmaster wetu alikuwa Katendele kisha akaja msukuma mmoja hivi aliyetokea Pugu Sekondarialikuwa akijulikana kama Wajimila , aisee tulikuwa na chifu mnoko huyo ambaye baadaye alikula mzinga yaani alipata zero.
du ebwana eee wewe seems tumemaliza wote vile..yule chief mrefu simkumbuki jina lake ila wa kule kule aliikuwa anajua kila kitu..umeondoka tabora boys lini..nimemeliza 1996 ndani ya Mrisho..wajimila aliondoka akaja mrisho..hahaha
Mzee Yatch endeleza libeneke!! Habari kutoka USA. Unajua afande Peter alichemka siku moja wakati namtaarifu kuwa naelekea Mwanza kwa dharura. Aliniambia kwa kiingereza " I think you should see Mr Nyanda, He is a very handsome man, he will help you!! Ha ha ha!!
AO - USA
Tabora school kichwa cha tanzania ,jina nalo we kote lina tajika hapa twakusanyika tupate kuelimika.
tabora school kichwa cha tanzania.maneno maarufu mbalala, unyuka, scramble, nguchilo, redo, tuku tuku, warsar, student center, numero (mke wa mrisho), Ngugu D(mr mkumba). madafu, masele, maduka, bila kusahau joint mass. bila kumsahau mzee mrisho na slogan yake. kula sana. cheza sana na soma sana na cheza sana.
Hahaahhahaa bado mshkaji umesahau mengine kuna extra drill, quarter guard, smart area, Bob Kinyesi (yule mwalimu wa Agriculture), nyangala (vitumbua) na mengi mengineyo,
Tabora School what can i say...i miss u... Tabora School Head of Tanzania...Tabora School Kichwa cha Tanzania...Siku hizi hakuna maafadnde tena, shule inaharibika...Wadau let us do something to our school...Je twawezaandaa tamasha kwa ajili ya kuisaidia shule yetu? Kwani inazidi kuchakaa majengo yake na miundombinu mingineyo...Nakumbuka sana mama Cherehani (Sijui bado yuko hai)kule jikoni, mapipo (mahindi), mbarara, unyuka, umwamba etc
Post a Comment