Sunday, August 30, 2009

Maonyesho ya JWTZ miaka 45



Marubani wa ndege za kivita za kijeshi wakiwa wamejipanga tayari kumpokea amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama nchini Rais Jakaya Kikwete.

Rubani wa kwanza wa kike Tanzania kwa ndege za kivita za Jeshi la Wananchi Tanzania, Luteni Rose Katila, mwenye barret ya bluu.

Rubani wa kwanza wa kike Tanzania kwa ndege za kivita za Jeshi la Wananchi Tanzania, Luteni Rose Katila ni mmoja wa marubani waliofanya mambo makubwa sana katika maonyesho ya miaka 45 ya Jeshi la Wananchi Tanzania, hakika kama hujamuona umekosa uhondo amefanya mambo mmakubwa mno, hongera dada Rose.

Maonyesho hayo ambayo ni ya kwa jeshi la Tanzania yamekuwa yakihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kisiasa na vikosi vya majeshi yaliyopo nchini,jana yalitembelewa na kiongozi wa kambi ya uongozi bungeni Hamad Rashid ambae aliongozana na mbunge wa Gando Khalifa Khalifa ambae ni mjumbe wa kamti ya bunge ya nje ulinzi na usalama.

Rashid alisema kwa kuwa gharama za ulinzi ni kubwa na hasa zinakuwa kubwa unapo haribika ulinzi jeshi hivyo, aliiomba serikali kulifanya jeshi hilo kuwa la kisasa ili litakapopata matatizo makubwa waweze kuyakabili kwa gharama ndogo.
“Pamoja na gharama hizo kuwa kubwa ni vizuri serikali ikajikaza ili kukahakikisha jeshi letu linakuwa ni jeshi la kisasasa”aliongeza Rashid.

Tunawaahidi sisi kama wabunge tutajitaidi kutumia nafasi zetu katika bunge kuona kwamba mali ghafi ‘resource’ zinazokuja zinafika kwa wakati na ikarabati wa zama zinawasaidia kufanya jeshi liwe la kisasa.

Maonyesho hayo yanayotarajiwa kuchukua wiki moja kuanzia Agosti 25 yatafikia kilele chake kesho ambapo yatafungwa rasmi na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Hussein Mwinyi.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...