Habari LeoShirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wiki ijayo litakata umeme kwa siku tano katika maeneo mbalimbali Dar es Salaam zikiwemo ofisi nyeti,hoteli za kitalii, na makazi ya Waziri Mkuu. Uongozi wa Tanesco umesema, umeme utakatwa kwa ajili ya ukarabati mkubwa wa mitambo inayosambaza umeme nishati hiyo katika maeneo hayo.
Kwa mujibu wa Tanesco,vifaa vinavyorekebisha kiwango cha umeme unaotolewa na transfoma kubwa za vituo vya Masaki na Oysterbay vimeharibika.Ofisi zitakazokumbwa na adha hiyo usiku na mchana ni pamoja na balozi za
Japan,Urusi
India, Kenya
Ufaransa, Afrika
Kusini, Nigeria,
Hospitali ya CCBRT na maeneo ya jirani.
Taarifa ya Meneja Mawasiliano wa Tanesco,Badra Masoud imesema, umeme utakatwa pia hoteli za kitalii zilizopo Masaki. Kwa mujibu wa Masoud,ukarabati huo unaotarajiwa kuanza Agosti 13,utakamilika Agosti 17 kwa kituo cha Oysterbay,na kwa Masaki utaanza Agosti 22, utakamilika Agosti 26 mwaka huu. Amesema,vifaa muhimu ndani ya tranfoma husika vitafumuliwa na zitawashwa tena baada ya kazi kukamilika.
“Kwa sababu hiyo, matengenezo katika vituo vyote viwili yatafanywa usiku na mchana hivyo vituo vitazimwa kabisa kwa siku zote tano,” ilisema taarifa.Amesema Shirika limeamua kufanya kazi hiyo kutokana na usumbufu mkubwa waliokuwa wakiupata wateja wengi wanaotumia vituo vya Masaki na Oysterbay Maeneo mengine yatakayokumbwa na adha hiyo ni Kinondoni Hananasifu,
Moscow,
Mkwajuni,
Mwananyamala,
Ada Estate,
No comments:
Post a Comment