Je wewe ni mwanablogu (Blogger) au mdau wa habari na mawasiliano kwaumma kwa kutumia mtandao? Kama jibu ni ndio, tafadhali unaombwakujiorodhesha kwa ajili ya maandalizi ya Kongamano Maalumu la Kitaifakwa ajili Wanablogu (Bloggers) na wadau wa habari na mawasiliano waTanzania (Tanzanians Bloggers Summit) linalotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu jijini Dar-es-salaam,Tanzania.
Dhumuni la kongamano hili ni Kuelimishana, Kufahamiana, KuamshaUtambuzi Rasmi Kuhusu Tekinolojia ya Blogu na Mawasiliano ya Umma kwaKutumia Mitandao, Kusaidia Utambuzi Rasmi juu ya mchango wa blogunchini Tanzania kama chombo muhimu cha habari na mawasiliano, Kuelimishana jinsi gani blogu zinaweza kutumika katika kuletamaendeleo katika nyanja za kijamii, kisiasa na kiuchumi, kuburudisha, kukuza utamaduni nk.
Wataalamu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wataalikwa kutoa madana mafunzo mbalimbali kuhusiana na tekinolojia ya kublogu, zananyinginezo za mawasiliano mtandaoni kama vile mitandao jamii(socialnetworking), online forums nk.Kutakuwa na vipindi vya maswali namajibu.Ili kufanikisha maandalizi ya Kongamano hili la kihistoria,kujiorodhesha kwako ni muhimu sana. Muda wa kujiodhoresha ni kuanziatarehe 12/8/2009 (Jumatano) mpaka 12/9/2009 (Jumamosi) tu.Kinachohitajika ili kujiandikisha ni :Jina Lako, Anuani yako ya barua pepe (E-mail), Mahali Ulipo auunapoishi (Nchi,mji nk), Namba ya Simu (sio lazima) na Anuani auURL(Universal Resource Locator) ya blogu yako (mfanowww.kongamano.blogspot.com/wordpress.com/.com/typepadVyeti vyaUshiriki vitatolewa kulingana na habari utakazoziorodhesha hapa.Unaweza kujiorodhesha kwa kutuma ombi lako kwa barua pepe kwenda;summit@bongocelebrity.com.
Zingatia tarehe za kujiandikisha. Ni mwezi mmoja tu! Asante kwa ushirikiano. UMOJA NI NGUVU!
No comments:
Post a Comment