Sunday, August 30, 2009
Jangili anaswa na nyara
Askari wa wanyama poli katika mbuga ya wanyama ya Wami-Mbiki iliyopo mkoa wa Morogoro na Pwani, Lucas Peter (51) kushoto akitoa minofu ya nyama baada ya jangiri Kaburu Yamungu Moshi kukamatwa na askari hao katika kijiji cha
Kidudwe wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro akidaiwa kuwinda kinyume na sheria. Picha na Juma Mtanda
Futari na Rais
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki la Dar Es Salaam, Mhashamu Method Kilaini, mara baada ya kumalizika kwa shughuli ya futari ambayo Rais Kikwete aliwaandalia viongozi wa dini na madhehebu mbali mbali nchini jana, Jumamosi, Agosti 29, 2009, Ikulu, Dar Es Salaam.
Maonyesho ya JWTZ miaka 45
Marubani wa ndege za kivita za kijeshi wakiwa wamejipanga tayari kumpokea amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama nchini Rais Jakaya Kikwete.
Rubani wa kwanza wa kike Tanzania kwa ndege za kivita za Jeshi la Wananchi Tanzania, Luteni Rose Katila, mwenye barret ya bluu.
Rubani wa kwanza wa kike Tanzania kwa ndege za kivita za Jeshi la Wananchi Tanzania, Luteni Rose Katila ni mmoja wa marubani waliofanya mambo makubwa sana katika maonyesho ya miaka 45 ya Jeshi la Wananchi Tanzania, hakika kama hujamuona umekosa uhondo amefanya mambo mmakubwa mno, hongera dada Rose.
Maonyesho hayo ambayo ni ya kwa jeshi la Tanzania yamekuwa yakihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kisiasa na vikosi vya majeshi yaliyopo nchini,jana yalitembelewa na kiongozi wa kambi ya uongozi bungeni Hamad Rashid ambae aliongozana na mbunge wa Gando Khalifa Khalifa ambae ni mjumbe wa kamti ya bunge ya nje ulinzi na usalama.
Rashid alisema kwa kuwa gharama za ulinzi ni kubwa na hasa zinakuwa kubwa unapo haribika ulinzi jeshi hivyo, aliiomba serikali kulifanya jeshi hilo kuwa la kisasa ili litakapopata matatizo makubwa waweze kuyakabili kwa gharama ndogo.
“Pamoja na gharama hizo kuwa kubwa ni vizuri serikali ikajikaza ili kukahakikisha jeshi letu linakuwa ni jeshi la kisasasa”aliongeza Rashid.
Tunawaahidi sisi kama wabunge tutajitaidi kutumia nafasi zetu katika bunge kuona kwamba mali ghafi ‘resource’ zinazokuja zinafika kwa wakati na ikarabati wa zama zinawasaidia kufanya jeshi liwe la kisasa.
Maonyesho hayo yanayotarajiwa kuchukua wiki moja kuanzia Agosti 25 yatafikia kilele chake kesho ambapo yatafungwa rasmi na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Hussein Mwinyi.
Friday, August 28, 2009
Thursday, August 27, 2009
JWTZ na maadhimisho ya miaka 45
Mambo yote haya unayapata pale Ukonga Airwing kila lizana la kiviuta la kutisha linapatikana katika maonyesho haya, kila mmoja anaweza anajionea mwenyewe hapo zamani ilikuwa siri, hivi sasa mambo yote hadharani wahi kabla ya Jumanne Septemba 1.
Kifaru cha kurushia makombora. Vifaa mbalimbali na silaha vinaoneshwa kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya JWTZ kutimiza miaka 45. Kwa Taarifa zaidi za sherehe hizi waweza tembelea FATHER KIDEVU
Miss Utalii Tanzania 2009 -Temeke
Lina Deus (19)
Jennifer Festo (19)
Erica Allan (23)
LINA Deusi, Jenifa Festo, Glori Mlayi, Neema Simbo, Happy Felix, Zainabu Matangi, Erica Allan
Zainabu Matangi.
Picha za Warembo wanaoshiriki shindano la Miss Utalii Tanzania 2009 -Temeke, picha zote zimepigwa jana wakati wa mazoezi katika Ukumbi wa City Garden (Gerezani Zamani) shindano hilo litafanyika siku ya Sept 25 hapo hapo City Garden Kariakoo, Dar es Slaam.
Mazoezi yameanza wiki hii Jumatatu na warembo zaidi wanatakiwa kufika katika mazoezi hayo ili kukamilisha mchakato mzima maandalizi kabla ya kwenda kutembelea katika hifadhi za Taifa ambako watajifunza masuala mbalimbali yanayohusiana na Utalii wa nchi hii.
Mratibu ama mhandaaji wa Miss Utalii Tanzania 2009 Temeke ni miss Utalii Tanzania- Vipaji 2005, Linda Masanche.
Jennifer Festo (19)
Erica Allan (23)
LINA Deusi, Jenifa Festo, Glori Mlayi, Neema Simbo, Happy Felix, Zainabu Matangi, Erica Allan
Zainabu Matangi.
Picha za Warembo wanaoshiriki shindano la Miss Utalii Tanzania 2009 -Temeke, picha zote zimepigwa jana wakati wa mazoezi katika Ukumbi wa City Garden (Gerezani Zamani) shindano hilo litafanyika siku ya Sept 25 hapo hapo City Garden Kariakoo, Dar es Slaam.
Mazoezi yameanza wiki hii Jumatatu na warembo zaidi wanatakiwa kufika katika mazoezi hayo ili kukamilisha mchakato mzima maandalizi kabla ya kwenda kutembelea katika hifadhi za Taifa ambako watajifunza masuala mbalimbali yanayohusiana na Utalii wa nchi hii.
Mratibu ama mhandaaji wa Miss Utalii Tanzania 2009 Temeke ni miss Utalii Tanzania- Vipaji 2005, Linda Masanche.
Rais ashiriki mazishi ya Askofu Mayalla
Wednesday, August 26, 2009
Mama Kikwete azindua kampeni ya Vodacom
Basi laua wanane, lajeruhi 52 katika ajali Morogoro
WATU wanane wamefariki dunia papo hapo na wengine 52 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya Scanlink walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka kijiji cha Maguha, tarafa ya Dumila wilayani Kilosa, mkoa wa Morogoro.
Ajali hiyo ilitokea Agosti 26 majira ya saa 5:15 asubuhi wakati basi hilo aina ya Scania lilipokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mwanza.
Kati ya watu waliofariki dunia wanne ni wanawake na watatu ni wanaume na mmoja ni mtoto wa kike mwenye umri wa miezi sita aliyetambuliwa kwa jina la Kwimba Sengeti, ambaye mama yake alijeruhiwa na kulazwa katika hospitali hiyo.
Marehemu wengine bado hawajatambulika na miili yao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya mkoa wa Morogoro. Majeruhi pia wamelazwa katika hospitali hiyo wakiendelea na matibabu na hali zao sio nzuri.
Watu walioshuhudia ajali hiyo walieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni utelezi baada ya mvua kunyesha katika eneo hilo na kusababisha basi hilo kuyumba na kupoteza muelekeo na kisha kupinduka.
Dereva wa basi hilo hakuweza kufahamika kutokana na hali za majeruhi waliofikishwa hospitalini kuwa mbaya. Hata hivyo polisi kwa kushirikiana na madaktari wanaendelea kufanya uchunguzi wa kumtambua dereva wa basi hilo.
Majeruhi walionusurika katika ajali hiyo walieleza kwa masikitiko kuwa, baada ya kupata ajali hiyo walivamiwa na watu wanaoishi karibu na kijiji hicho na kuwapora baadhi ya mali zao, zikiwemo simu na fedha.
Walisema baada ya polisi kufika katika eneo hilo watu hao walitoweka na wengine kujifanya wanatoa msaada na hivyo kushindwa kubainika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Thobias Andengenye alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kwamba, jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi, ili kujua chanzo cha ajali hiyo.
Tuesday, August 25, 2009
Mashindano ya kusoma kwa kukariri Kuran
Salma Khamis (12)
Vijana mbalimbali kutoka vyuo mbalimbali vya kiislamu wakishindana kusoma kwa kukariri quran, mashindano hayo yalifanyika juzi katika Viwanja vya Mwembe YangaTandika, Dar es Salaam.
Msemaji wa Kituo cha Ubalozi wa Iran, Mostafa Kanjibar, akikabidhi zawadi ya Feni kwa mshindi wa kusoma juzuu 7, Yassin Abass, yaliyofanyika katika viwanja vya mwembe Yanga, Dar es Salaam.
Malipo ya waathirika Mbagala vilio tupu
Malipo ya waathirika wa mabomu Mbagala yameanza kutolewa leo katika Ofisi za Manipaa ya Temeke Dar es Salaam. Walio na malalamiko waliwasilisha baada ya kupokea Hundi au kabla. maana wapo wanaolipwa 30,000 wakati alitaraji milioni kadhaa. Watu kibao wanalia kupita kiasi walitarajia makubwa na wamepata kiduchuu!!!!!!!!!! picha na zaidi hebu cheki hapa kwa http://mrokim.blogspot.com/2009/08/malipo-mbagala-yaanza.html
Monday, August 24, 2009
Wanafunzi walioteketea na moto kuzikwa
SERIKALI imefunga Shule ya Sekondari ya Idodi kwa muda wa siku 21 kufuatia vifo vya wanafunzi wa kike 12 na kujeruhi wengine 23 baada ya bweni la wasichana la Shule hiyo kuteketea kwa moto.
Akizungumza ana wanafunzi wa shule hiyo wakiwemo walionusurika na ajali hiyo pamoja na wazazi wao jana, Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi stadi, ProfesaJumannne Maghembe aliyefuatana na Naibu wake, Mwantumu Mahiza alisema wamefikia hatua hiyo ili kuweza kupata nafasi nzuri ya kuisitiri miili ya wanafunzi waliokufa na kujipanga.
Alisema ajali hiyo ni kubwa na inatia huzuni kwa wanafunzi,wazazi na majirani wanaoishi katika eneo na endapo shule haitafungwa itakuwa ni hatari kubwa kwa wanafunzi walionusurika.
Alisema wanafunzi 326 walinusurika hawana mahali pa kulala baada ya bweni hilo kuteketea na moto ambalo linachukua watoto 461 lenye vyumba 25 kuteketea kabisa na moto huo uliozuka usiku wa manane Agosti 23 mwaka huu.
Maghembe alisema kuwa kuwa shule hiyo imefungwa rasmi Agosti 23 na itafunguliwa Septemba 13 mwaka huu ili kutoa nafasi kwa serikali kufanya ukarabati wa bweni hilo lenye vyumba 25 yalioharibiwa kwa kuteketezwa na moto uliosababishwa na mshumaa uliokuwa ukitumiwa na mmoja wa wanafunzi, Naomi Nyange aliyekuwa akijisomea.
Alisema pia serikali inaangalia uwezekano wa kuweka umeme na muundo wa ujenzi wa mabweni iwe na milango mingi ili inapotokea janaga kama hilo iwe rahisi kuokoka.
Naye Kaimu Mkuu wa mkoa wa Iringa Aseri Msangi akizungumzia kuhusu mazishi alisema kuwa wanafunzi wote 12 waliofariki dunia watazikwa kwa pamoja katika eneo la shule kesho, Agosti 25 mwaka huu. Imeandikwa na Hakimu Mwafongo.
Matatizo ya wafugaji Longido
Mfugaji akiswaga ndama walio salia baada ya Ng'ombe wake zaidi ya 700 kufa kwa ukame.
Rais Jakaya Kikwete juzi alitembelea Wilaya ya Longido kuangalia athari za Ukame na upungufu wa chakula uliopo Wilayani humo na kuahidi kuwapatia msaada.
Blogu hii ya jamii inawaomba viongozi wa serikali kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa haraka na bila usumbufu.
Hebu nipeni kapsheni ya hii picha
Waijua ming'oko
Friday, August 21, 2009
Mama Obama
Uonapo barabarani ajali imetokea
Thursday, August 20, 2009
KUSAKA UBUNGE SI LELE MAMA
WAZIRI DKT,BATILDA BURIANI AKIPIGA MPIRA KAMA ISHARA YA UFUNGUZI WA MICHUANO YA ROLLING STONE KATIKA UWANJA WA SHEIKH AMRI ABEID ARUSHA,NYUMA YAKE ALIYEVALIA SUTI NYEUSI NI MRATIBU MKUU WA MICHUANO HIYO,WILLYBROAD ALPHONCE NA ALIYEVALIA KOTI JEKUNDU NI ASHA MTUMWA MKURUGENZI WA ROLLING STONE. PICHA YA MOSSES MASHALLAH
Wednesday, August 19, 2009
Askofu Mayalla afariki dunia
ASKOFU mkuu wa jimbo kuu la Mwanza, kanisa Katoliki Mhashamu Anthony Petro Mayalla (69) amefariki dunia jana mchana kutokana na maradhi ya moyo baada ya kuugua ghafla akiwa ofisini kwake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na mkurungenzi wa mawasiliano wa baraza la Maaskofu (TEC) kanisa katoliki, Padri Revocatus.
Makonge Askofu huyo amefariki baada ya madaktari wa Hospitali ya rufaa ya Bugando kuhangaika kumpatia matibabu bila ya mafanikio.
Alisema kuwa marehemu aliamuka salama jana na kuendelea na shughuli zake za kila siku ofisini kwake mpaka majira ya saa 4:00 asubuhi ambapo alizidiwa ghafla na kukimbizwa Hospitali ya rufaa ya Bugando.
Habari kutoka katika ofisi ya aksofu huyo, zimeeleza kuwa alipatwa na maradhi hayo wakati akiwa katika maandalizi ya ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Vatican ambaye alikuwa akitarajiwa kufanya ziara jimboni kwake Oktoba 5 mwaka huu kwa ajili ya kufungua ujenzi wa hospitali ya watoto.
“Baada ya kufikisha hospitalini hapo madaktari waliahangaika kuokoa maisha yake lakini nahati mbaya lifariki dunia majira ya saa 8;30 mchana,” alieleza Padri Revocatus Makonge.
Askofu Mayalla alizaliwa Aprili 23 mwaka 1940 katika katika kijiji cha Nera wilayani Kwimba na kupata elimu yake ya msingi katika wilaya hiyo na masomo ya sekondari.
Askofu Mayalla alikuwa amehitimu shahada ya kwanza ya elimu aliyopita katika chuo kikuu cha Loyola huko Chicago Marekani mwaka 1973 hadi 1975. Frederick Katulanda, Mwanza.
Tuesday, August 18, 2009
Illuminata huyoooo
Monday, August 17, 2009
Mwanafunzi mkongwe afariki dunia
Mwanafunzi mkongwe kuliko pengine wote aliyekuwa akihudhuria masomo ya aelimu ya msingi Kimani Maruge (front) amefariki dunia he attended class at Kapkenduiywo Primary School in Langas, Eldoret, 300km west of the Kenyan capital Nairobi, in this October 6, 2006 file photo. Maruge, a farmer celebrated in Kenya as the world's oldest school pupil, has died in the east African country aged 90, local media said on August 14, 2009. REUTERS/Thomas Mukoya/Files. Alifariki dunia Ijumaa.
Zombe Huru
Hukumu iliyosomwa na Jaji Salum Masati iliyochukua takribani masaa sita, leo katika Mahakama Kuu ya Tanzania imewaachia huru watuhumiwa wote saba katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini na dereva taksi mmoja, iliyokuwa ikiwakibili aliyekuwa Afisa upelelezi wa mkoa wa Dar es Salam Abdallah Zombe na wenzake.
Zombe na wenzake walikuwa wanatuhumiwa kwa kosa la kufanya mauaji kwa kukusudia Sabinus Chigumbi, maarufu kama Jongo na ndugu yake Ephrahim Chigumbi na Mathias Lunkombe ambao ni wafanyabiashara wa Mahenge.
Mwingine ni dereva teksi wa Manzese jijini Dar es salaam, Juma Ndugu. Akisoma hukumu hiyo JAJI Masati amesema kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaonesha kuwa watuhumiwa hao walihusika katika kufanya mauaji ya wafanyabiashara hao.
Hivyo Mahakama haikuweza kuwatia hatiani. Watu wengi wali waliokuwepo Mahakamani wameonesha kutoridhishwa na hukumu hiyo, hali ambayo inabakisha kitendawili juu ya hatima ya maisha ya waliokua watuhumiwa katika kesi hiyo wakiwa uraiani.
Sheria Ngowi Fashion Show
Sheria Ngowi Fashion Show Red Carpet! Mens Collection 09 Bangalore,India. Kwa taarifa za kina hebu msome Haki Ngowi
Sunday, August 16, 2009
Malima awatoa hofu Bahi
The Deputy Minister for Energy and Resources Adam Malima address Bahi Sokoni residents in Bahi District, Dodoma region over the weekend where refuted false information allegedly spread by such NGOs that residents of 80 villages would face eviction comes uranium mining activities in the district Photo/Jube Tranquilino
CC- NEC za CCM mambo magumu mnooo
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Kepteni Mstaafa John Chilighati (kulia) akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma jana baada ya kumalizika kwa mkutano wa kamati kuu. Picha na Jube Tranquilino
Speaker of the National Assemby Samwel Sitta listens to Abdulahman Kinana before the opening of NEC meeting in Dodoma yesterday. Photo/Jube Tranquilino
Hasheem Thabeet
Subscribe to:
Posts (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...