KUNDI la Wanachama wa Tanzania Labour Party (TLP), wametangaza kujiengua na uongozi wa chama hicho na kuteua viongozi wapya wa mpito kutokana na kutopewa haki zao za kidemokrasia katika uchaguzi mkuu uliofanyika juzi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam akiwa ameambata na wajumbe wa TLP kutoka mikoani, Mwenyekiti mteule wa Taifa, Maxmilliam Lyimo alisema kutokana na kutotendewa haki ya kidemokrasia katika uchaguzi wa juzi wajumbe wameteua viongozi wao wa mpito wa Taifa ili kukinusuru chama.
“Ndugu waandishi wa habari tumewaita ili kuelezea uchaguzi wa kihuni uliofanyika jana uliofanywa na Mrema akishirikiana na Kikwete ili wahakikishe tunashindwa uchaguzi” alisema Lyimo.
Pia Lyimo aliongeza kuwa; “Kutokana na hali hiyo ili kukinusuru chama ndipo kamati Mpya ya mpito wa mkutano mkuu umeteua viongozi wa mpito mpaka hapo utakapofanyika uchaguzi wa kidemokrasia”
Aidha, Lyimo aliwataja viongozi wapya wa mpito wateule wa Kitaifa watakaokuwa wanakiongoza chama hicho mpaka hapo utakapofanyika uchaguzi Mkuu na sio uchaguzi wa kihuni uliofanyika juzi Mbagala.
“Nafasi ya Mwenyekiti nimeteuliwa mimi, Joram Kinanda ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti, Benedicto Mtungirehi Katibu Mkuu na naibu Katibu ameteuliwa James Haule na pia wajumbe kutoka mkoani wamepita kuwa wajumbe,” alisema Lyimo.
Lyimo aliongezea kwa kutoa mpya kuwa Mrema ameletwa na serikali ili akivuruge chama na pia ni usalama wa Taifa na ushaidi anao kwani alishatangaza wakati akiwa kwenye mkutano na wananchi wa Umbwe Moshi Vijijini mwaka 1986. Taarifa imeandikwa na Felix Mwagara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment