Monday, April 27, 2009

Abdul mshindi wa Mil 10 shindano la maisha plus






MSHIRIKI kutoka Zanzibar Abdul juzi ameibuka mshindi katika shindano la maisha plus na kujinyakulia kitita cha fedha taslim shilingi millioni 10, baada ya kuishi kijiji kwa takribani siku 56.

Kwa matokea yaliyotolewa na majaji kwa kupitia ujumbe mfupi uliokuwa ukitumwa na wananchi ambao walikuwa wakifuatilia mchezo huo kupitia mtandaoni na televisioni ya taifa (TBC, 1)

Mshindi huyo kutoka Zanzibar, Abdul ambae alikuwa akishindana vikali na Mwanadada Upendo kutoka mkoani Mwanza ambae alijiwekea uwezo mkubwa sana lakini hadi kufikia mwisho wa mashindano mshiriki huyo hakuweza kuamini ukweli wa matokeo waliyoyatangaza majaji.

Katika ya mchezo huo ambao mshiriki kutoka Mwanza Upendo alikuwa hakionekana kuwa mshindi baada ya kuwa na pointi nyingi ambazo ziliweza hata kumshinda Abdul kwa kuwa na pointi nyingi hadikufikia wiki mbili za mwisho.

Wakati mshindi wa shindano hilo akikabidhiwa kitita cha sh mil 10 na baadae wote waliweza kupatiwa siku moja ya kukutana na kubadilishana mawazo katika mbuga za wanyama zilizopo Mikumi mjini Morogoro.

Kufuatia siku hiyo ya kutembelea mbuza za wanyama washiriki ambao watakaokuwa walengwa na wale wote ambao wamefanikiwa kuingia katika kinyanganyiro cha kumi bora.

Washiriki hao ambao wameingia kumi bora na baadae kubaki washiriki watatu na ndipo alipochaguliwa mshindi mmoja na kujinyakulia shilingi milioni kumi ambayo ataweza kuwekewa kwenye akaunti yake kwa ajili ya usalama zaidi.

Washiriki hao ambao waliweza kuingia kumi bora ni Abduli,Modersta,Steve,Hamis,Maulid, makala hii fupi imeandikwa na Zaina Malongo






.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...