Wednesday, April 29, 2009

Mabomu Dar balaa







HALI ni tete, Jiji la Dar es Saalam na vitongoji vyake, jana lilizizima kwa mishindo mkubwa na mitetemo ya mabomu na makombora yaliyolipuka kwa kupishana kutoka katika kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), 671 Mbagala.

Mtafaruku huo, pia uliyakumba maeneo jirani na kusababuisha vifo vya watu, mamia kujeruhiwa, nyumba kuungua, huku watoto 200 wakipotezana na familia zao.

Mamia ya wakazi wa jiji hilo hasa Mbagala na vitongoji vyake walionekana kuchanganyikiwa walikuwa wakihangaika kukimbia nyumba zao kwa lengo la kujiokoa.

Katika harakati za kujiokoa baadhi ya wananchi ho walitumbukia mtoni huku baadhi yao wakiwasahau watoto wao na vikongwe nyumba bila msaada wowote

Barabara ya Kilwa kuanzia eneo la uwanja wa Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara, Kambi ya Jeshi ya Twalipo hadi Mbagala Kizuiani ilipo kambi hiyo ya kikosi cha 671, ilijaa askari wa JWTZ waliojipanga kando na kuongoza magari, huku wakizuia mengine kuelekea karibu na eneo la tukio.

Majira ya saa tano asubuhi mshindo mzito wa kwanza ulisikika na ambao ulitikisa takriban majengo yote katikati ya jiji, huku moshi mweusi ukionekana angani upenda wa barabara ya Kilwa na dakika chache baadaye magari ya vikosi vya zima moto, polisi, JWTZ na waandishi wa habari vilihangaika kuelekea kwenye tukio.

Hata hivyo misafara hiyo ilikwamishwa njiani na msururu mrefu wa magari na wananchi waliokuwa wakikimbia kutoka eneo karibu na tukio kuelekea katikati ya jiji, hivyo kulazimika kutafuta njia nyingine ya kufika eneo la tukio.

Vikosi vya zima moto viliwahi eneo la tukio, huku milipuko ilikuwa ikiendelea kwa mpishano wa dakika kati ya tatu na sita majira ya asubuhi na saa za jioni ilipugua kwa mpshano wa robo saa hadi dakika 20.

1 comment:

Dennis Mwasalanga said...

full fledged..your blog is tite.
Bombings in countries like Tanzania its uzembe wa majeshi yetu. kwanini wahifadhi mabomu mazito hivyo kwa nchi ya amani kama hii?

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...