Thursday, April 30, 2009

Chenge aongezewa shtaka

Marehemu Beatrice Costantine!

Marehemu Vicky Makanya!
Mzee wa vijisenti

MBUNGE wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge jana aliongezewa shtaka katika kesi inayomkabili ya mashtaka matatu ya kuendesha gari kizembe na bila tahadhari na kusababisha vifo vya watu wawili na uharibifu wa pikipiki ya matairi matatu, maarufu kama Bajaji.

Waziri huyo wa zamani wa miundombinu ambaye pia alikuwa mwanasheria mkuu wa serikali alifikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kinondoni jana na kusomewa mashtaka yake mapya ambayo sasa yanakuwa manne.

Chenge ameongezewa shtaka la kuendesha gari aina ya Toyota Hilux Double Cabin ambayo ilikuwa haina bima. Pia katika kesi hiyo ameunganishwa mmiliki wa Bajaji hiyo, Majid Ghalid, 26.

Chenge, ambaye alijiuzulu wadhifa wake wa Waziri wa Miundo Mbinu baada ya kutajwa kwenye kashfa ya ununuzi wa rada, alitinga mahakamani hapo tofauti kabisa na awali, akionekana kutokuwa na woga na alisalimiana na wananchi waliokuwa wamefurika mahakamani.

Akisoma hati ya shtaka la kwanza kwanza, mwendesha mashtaka wa polisi, David Mafwimbo alidai kuwa alfajiri ya Machi 27 mwaka huu Chenge alitenda kosa la kwanza kwenye makutano ya Barabara ya Haile Salasie na Karume alipoendesha gari hilo kwa uzembe kwenye makazi ya watu na kushindwa kuchukua tahadhari na kuigonga Bajaji kusababisha kifo cha Victoria Goerge.

Katika shtaka la pili, Mafwimbo alisema siku na wakati kama huo, Chenge alisababisha kifo cha Beatrice Constantine.

Mafwimbo alidai kuwa Chenge alitenda kosa la tatu katika muda na tarehe kama hiyo kwa kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha uharibifu wa Bajaj iliyokuwa inatoka upande wa pili. habari imeandikwa na Kuruthum Ahmed.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...