Sunday, August 12, 2007

Wafanyakazi wamtikisa JK wampa siku 30





Katika kuonyesha kweli wamekereka na ahadi wanazodai hazitekelezeki wafanyakazi mkoani Dar es Salaam, wamempa siku 30 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (Tucta), Nestory Ngulla, kufikisha malalamiko yao kwa Rais Jakaya Kikwete na kurejeshewa majibu, kuhusu nyongeza duni ya mishahara, ili kuepusha hatua nyingine watakazotumia kudai mishahara.

Tamko hilo lilitolewa na wafanyakazi hao kupitia risala yao iliyosomwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam baada ya kuhitimisha maandamano ya amani yaliyoandaliwa na vyama 18 vya wafanyakazi nchini kupinga kima cha chini cha mshahara wa serikali, kilichopitishwa na bunge hivi karibuni.

Baadhi ya vyama hivyo, ni pamoja na cha Walimu (CWT), Sekta ya Afya (Tughe), Migodi, Nishati, Ujenzi (Tamico), Serikali za Mitaa (Talgwu), Mabaharia (Tasu), Walinzi binafsi (Tupse), Mashambani (Tpawu), Shughuli za Meli (Dowuta), Mawasiliano (Tewuta), Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Habari na Utafiti (Raawu), Waandishi wa Habari (TUJ) na Chodawu. Picha ya Mpoki Bukuku

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...