Thursday, August 16, 2007

Mtukufu Aga Khan




KIONGOZI wa kidini wa Jumuiya ya Ismailia duniani Imam Aga Khan ameleezea nia yake ya kutaka kujenga Chuo kikuu kipya hapa nchini.

Akizungumza na Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein jana Ikulu Jijini Dar es Salaam Imam Aga Khan alisema chuo hicho kitajengwa mkoani Arusha na kwamba kitakuwa cha aina yake katika Afrika kutokana na kuhusisha masomo ya taaluma muhimu pekee.

Mara baada ya ndege aina ya LX-PAK kutua katika viwanja hivyo kwenye saa 12:30 mlango ulifunguliwa na kisha kiongozi mwakilishi wa Mtandao wa Maendeleo ya Aga Khan aliingia ndani ya ndege hiyo kwa ajili ya kumuongoza Aga Khan aweze kushuka.

Mara baada ya kushuka, Aga Khan alipokelewa na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya ndani, Joseph Mungai.

Kisha wimbo maalumu wa jumuiya yao ulipigwa na Brass Bendi ya polisi na baada ya wimbo huo kiongozi huyo alipata fursa ya kuangalia ngoma ya asili yao, sarakasi pamoja na ngoma ya kimasai iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili yake.

Akizungumza mara baada ya mapokezi hayo, Mungai alisema ujio wa kiongozi huyo ni kwa ajili ya kusherehekea miaka 50 ya uimamu wake katika madhehebu ya kiismailia.

Mungai alisema, Aga Khan ameweza kuwa na ushirikiano mkubwa katika nyanja ya kimaendeleo hususani kwenye sekta ya Eimu na Tiba.

“Nataka niwahakikishieni kuwa katika hili la Elimu, shule ya kwanza ya wasichana iliyoko kule Zanzibar ilianzishwe na babu yake huyu Aga Khan, pia anaendelea na juhudi kubwa za kuendeleza Elimu katika taifa letu,” alisema Mungai. Mdau Mpoki Bukuku alikuwako huko na picha hii ni kwa hisani yake.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...