Tuesday, December 27, 2016

MUSOMA VIJIJINI WAJISIFU WALICHAGUA JEMBE,WAMMWAGIA SIFA PROF. MUHONGO

Mzee wa Kijiji cha Murangi- Musoma Vijijini, Clifford Biseko (kulia) akifungua rasmi mkutano wa kujadili uchumi na maendeleo ya Jimbo la Musoma Vijijini. Wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo hilo, Profesa Sospeter Muhongo. 
Madiwani wa Musoma Vijijini wakijitambulisha wakati wa mkutano wa Tathmini ya Maendeleo na Uchumi ya Jimbo la Musoma Vijijini. Wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo hilo na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. 
Wadau wa maendeleo ambao pia ni wazaliwa wa Musoma Vijijini lakini wanaishi nje ya hapo wakijitambulisha.+
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Musoma, Flora Yongolo akitambulisha watendaji mbalimbali kutoka kwenye halmashauri hiyo.


Baadhi ya wananchi wa Musoma Vijijini waliohudhuria mkutano huo wakimsikiliza Mbunge wao, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).



Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wamempongeza Mbunge wao na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa kufanya mambo makubwa ya kimaendeleo ndani ya mwaka mmoja. 

Pongezi hizo zimetolewa na wananchi wa jimbo hilo wakati wa mkutano wa Tathmini ya Maendeleo na Uchumi ya jimbo uliofanyika hivi karibuni katika Kijiji cha Murangi, Musoma Vijijini na kushirikisha wananchi wa jimboni humo, madiwani, wadau wa maendeleo na watendaji wa Halmashauri husika. 

Awali akifungua mkutano huo mzee wa Kijiji cha Murangi, Musoma Vijijini, Clifford Biseko alisema wanamusoma vijini wanajivunia maendeleo yanayodhihirika kila kukicha kutokana na mchango wa mbunge huyo. Aliongeza kwamba Profesa Muhongo ni mtu sahihi kwa nafasi hiyo na kuwa hawajuti kumchagua na wanamwombea afya njema ili azidi kushirikiana nao katika kusukuma gurudumu la maendeleo jimboni humo. 

Alisema katika kipindi kifupi cha uongozi wake, wameshuhudia masuala makubwa ya maendeleo kwenye sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, kilimo, sanaa na michezo. Akizungumzia suala la afya, Biseko alisema, Musoma Vijijini haikuwahi kuwa na gari hata moja la wagonjwa lakini tangu Profesa Muhongo awe Mbunge tayari jimbo hilo linayo magari manne. 

Aliongeza kuwa Musoma vijijini haikuwahi kupata ugeni wa madaktari bingwa kwa ajili ya vipimo, ushauri na matibabu lakini kwa Profesa Muhongo hilo liliwezekana kwani alikaribisha madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi ambao walitoa huduma bila malipo. 

Kuhusu suala la kilimo, Biseko alisema, tangu Profesa Muhongo achaguliwe, alisambaza tani kadhaa za mbegu za zao la mihogo na alizeti ili wananchi wajikwamue kwenye umasikini. Aliongeza kuwa, Profesa Muhongo alipeleka wataalamu mahiri wa kilimo kutoka ndani na nje ya nchi ili kufanya tathmnini ya kilimo bora ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri wa kilimo bora. 

Aidha, suala la elimu, Biseko alisema kuwa kulikuwa na uhaba wa madawati 8,000 kwa shule zote zilizomo jimboni humo na hilo lilitatuliwa bila wao kuchangishwa pia kusambaziwa shehena ya vitabu vya sayansi kwa shule zote. Biseko alimalizia kwa kuzungumzia sekta ya michezo na sanaa alisema kuwa Mbunge ameandaa mashindano mbalimbali na vilevile kugawa vifaa vya michezo kwenye vijiji mbalimbali jimboni humo jambo ambalo alisema limehamasisha sekta husika.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI MKOANI LINDI KWA ZIARA YA KIKAZI KATIKA WILAYA YA RUANGWA

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Lindi Godfrey Zambi mara alipowasili katika uwanja wa ndege wa Nachingwea kwa ajili ya ziara ya kikazi katika wilaya ya Ruangwa Mkoani lindi kushoto ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi  Alli Mohamed Mtopa
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mkurugenzi wa Nachingwea (DED) Bakari Mohamedi Bakari katika kiwanja cha ndege cha Nachingwea wakati wa mapokezi ya waziri mkuu wilayani hapo waziri mkuu amefika kwa ziara ya kikazi katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi 
Waziri mkuu Kassim Majaliwa na mkewe Mery Majaliwa wakifurahia ngoma ya kikosi cha JKT  843KJ kilichopo Nachingwea ambacho kilikuwepo katika mapokezi ya Waziri Mkuu katika uwanja wa ndege wa Nachingwea .Picha na Chris Mfinanga

Friday, December 23, 2016

WAZIRI NAPE NNAUYE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA MWANAHABARI MPOKI BUKUKU

index

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa wapiga picha pamoja na Wanahabari wote nchini kufuatia kifo cha mwanahabari na mpiga picha Mpoki Bukuku kilichotokea leo katika Taasisi ya Mifupa (MOI)
Mhe. Nape Nnauye pamoja na watendaji wa Wizara wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mwanahabari huyo kwani ni pigo katika tasnia ya habari nchini.
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha mwanahabari Mpoki Bukuku. Kifo chake ni pigo katika tasnia ya habari hususani katika picha , nimehuzunishwa sana kwa sababu Marehemu wakati wa uhai wake ametoa mchango mkubwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo magazeti ya  Majira, Business Times , The Guardian , Nipashe na Mwananchi na The Citizen.”
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amina
Imetolewa na Idara ya Habari(MAELEZO)
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Dar es Salaam
23 Desemba, 2016

RAIS DKT MAGUFULI NA MKEWE MAMA JANETH MAGUFULI WAMTEMBELEA ASKOFU MKUU POLYCARP KARDINALI PENGO

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiongea na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es salaam Muadhama Polycarp Kardinali Pengo walipomtembelea kumpa pole kufuatia kifo cha dada yake nyumbani kwake Kurasini jijini Dar es salaam leo Desemba 23, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiongea na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es salaam Muadhama Polycarp Kardinali Pengo walipomtembelea kumpa pole kwa kufiwa na dada yake nyumbani  kwake Kurasini jijini Dar es salaam leo Desemba 23, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa kwenye picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es salaam Muadhama Polycarp Kardinali Pengo walipomtembelea kumpa pole kwa kufiwa na dada yake nyumbani  kwake Kurasini jijini Dar es salaam leo Desemba 23, 2016

PICHA NA IKULU

TUME YA MIPANGO YATEMBELEA KIWANDA CHA VINYWAJI CHA AZAM

 Meneja anayesimamia Ubora wa Bidhaa, Lilian Mwashigadi (aliyevaa koti jeupe) akiwaonesha maofisa wa ukaguzi wa miradi kutoka Tume ya Mipango hatua za mwisho za uzalishaji wa juisi katika kiwanda cha uzalishaji wa vinywaji kilichopo eneo la Mwandege Mkoani Pwani.
 Meneja anayesimamia Ubora wa Bidhaa, Bibi Lilian Mwashigadi (mwenye koti jeupe) akionesha mtambo unaotumika katika uzalishaji katika kiwanda hicho.
 Wataalam kutoka Tume ya Mipango wakimsikiliza Meneja anayesimamia Ubora wa Bidhaa, Bibi Lilian Mwashigadi wakati wa ziara ya Tume ya Mipango katika kiwanda cha uzalishaji wa vinywaji kilichopo eneo la Mwandege Mkoani Pwani.
 Meneja anayesimamia Ubora wa Bidhaa, Bibi Lilian Mwashigadi pamoja na wataalamu kutoka Tume ya Mipango wakiwa wameshika vichupa vidogo vinavyotanuliwa kwenye mitambo na kuwa chupa kubwa za kufungashia kunywaji aina ya Energy.
 Bidhaa ya vinywaji aina ya Energy katika hatua za mwishoni za uzalishaji.
 Bidhaa zikiwa zinapangwa baada ya kupitia hatua mbalimbalikatika katika kiwanda cha uzalishaji wa vinywaji kilichopo eneo la Mwandege Mkoani Pwani.
Baadhi ya mitambo ya  kiwanda cha uzalishaji wa vinywaji kilichopo eneo la Mwandege Mkoani Pwani. PICHA ZOTE NA ADILI MHINA, TUME YA MIPANGO

Na Adili Mhina, Pwani.
Tume ya Mipango imetembelea kiwanda cha vinywaji cha Azam kilichoko eneo la Mwandege Mkoani Pwani na kuonesha kuridhishwa na shughuli za uzalishaji za kiwanda hicho ikiwa ni moja ya mikakati ya kutekeleza malengo ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21) wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

Timu ya wataalamu wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya Mipango ilifanya mazungumzo na Meneja anayesimamia ubora wa bidhaa kiwandani hapo, Bibi Lilian Mwashigadi na kuelezwa kuwa kiwanda hicho kipo katika hali nzuri na kinaendelea na shughuli za kuzalisha bidhaa zenye ubora unaotakiwa katika kukidhi mahitaji ya soko. 

Bibi Mwashigadi alieleza kuwa kiwanda hicho ambacho kina jumla ya wafanyakazi 800 ambapo kati hao 500 ni ajira za moja kwa moja (direct labor) na 300 ni ajira zisizo za moja kwa moja (indirect labor) kina mikakati ya kuendelea kupanua soko la bidhaa zake kimataifa ambapo kwa sasa kinauza bidhaa katika nchi za Kenya na Rwanda. 

Kuhusu upatikanaji wa matunda ya kutosheleza kiwanda hicho, Meneja huyo alieleza kuwa hakuna changamoto kwani hapa nchini kuna matunda yenye ubora unaokidhi mahitaji ya viwanda na kiwanda chake kinategemea malighafi hiyo kutoka kwa wakulima wadogo wadogo kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Pamoja na hayo, Bibi Mwashigadi aliongeza kuwa kiwanda chake kimeendelea kununua matunda kwa bei nzuri ambayo inaendana na bei ya kawaida ya soko lengo likiwa ni kuhakikisha mkulima anaona faida ya kujishughulisha na kilimo cha matunda. 

Hata hivyo alitoa wito kwa Tume ya Mipango kuangalia namna ya kutengeneza sera itakayosaida kumnufaisha zaidi mkulima mdogo kwani kwa sasa madalali ndio wanaochukua matunda toka kwa wakulima na kupeleka kiwandani na mkulima anaishia kupata faida kidogo huku madalali wakiendelea kunufaika.

MASAUNI KUYAFUTA MASHIRIKA YANAYOBARIKI USHOGA NCHINI, AWATAKA VIJANA KUISHI KWA KUFUATA MAADILI MEMA YA DINI

sao-1
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza katika Ziara ya Shekhe Uwesu bin Muhammad Alqadiriya iliyofanyika katika Zawiya ya Shekhe Mahadh Kigamboni,  jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake Masauni aliwataka vijana kuwa makini na mashirika ambayo yanahamasisha ushoga nchini, na pia alitangaza kuyafuta mashirika hayo endapo yakigundulika. Kulia kwake ni Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Hamid Masoud Jongo.
sao-2
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia aliyekaa) akimsikiliza Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Hamid Masoud Jongo alipokuwa akizungumza na Waislam katika Ziara ya Shekhe Uwesu bin Muhammad Alqadiriya iliyofanyika katika Zawiya ya Shekhe Mahadh Kigamboni, jijini Dar es Salaam leo. Mgeni rasmi katika sherehe hiyo, Mhandisi Masauni, katika hotuba yake aliwataka vijana kuwa makini na mashirika ambayo yanahamasisha ushoga nchini, na pia alitangaza kuyafuta mashirika hayo endapo yakigundulika. 
sao-3
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia aliyekaa) na  Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Hamid Masoud Jongo (wapili kulia waliokaa) wakimsikiliza Shekhe wa Wilaya ya Kigamboni, Abdalla Idd alipokuwa akizungumza na Waislam katika Ziara ya Shekhe Uwesu bin Muhammad Alqadiriya iliyofanyika katika Zawiya ya Shekhe Mahadh Kigamboni, jijini Dar es Salaam leo. Mgeni rasmi katika sherehe hiyo, Mhandisi Masauni, katika hotuba yake aliwataka vijana kuwa makini na mashirika ambayo yanahamasisha ushoga nchini, na pia alitangaza kuyafuta mashirika hayo endapo yakigundulika.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Na Felix Mwagara (MOHA)
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amewataka vijana nchi kuwa makini na baadhi ya Mashirika yasiyokuwa ya Serikali ambayo yanajishughulisha na uhamasishaji wa mapenzi ya jinsia moja (ushoga).
Mhandisi Masauni alisema, Mashirika hayo hayapaswi kuwepo nchini kwani yanafanya kazi kinyume na mila na desturi ya nchi yetu na yanapaswa kufutwa haraka iwezekanavyo endapo yatagundulika.
Akizungumza katika Ziara ya Shekhe Uwesu bin Muhammad Alqadiriya iliyofanyika katika Zawiya ya Shekhe Mahadh Kigamboni,  jijini Dar es Salaam, Mhandisi Masauni aliongeza kuwa, vijana wanapaswa wawe makini katika maisha yao, kamwe wasikubali kupotoshwa pamoja na kuendeshwa na kundi lolote ambalo linafanya kazi kinyume na taratibu za nchi.
“Kuna baadhi ya mashirika ambayo yanajihusisha kwa kutoa elimu na kuhamasisha ndoa za jinsia moja, mashirika hayo yanafanya kazi kinyume na sheria ya nchi, hivyo tunayachunguza na tukiyagundua hakuna cha Mswalie Mtume, tutayafuta haraka iwezekanavyo,” alisema Masauni.
Pia aliwataka Watanzania kutoa taarifa ya uwepo ya taasisi hizo binafsi zinazofanya shughuli hizo nchini muda wowote wakizigundua ili zifuatiliwe kwa umakini na hatimaye zifutwe haraka iwezekanavyo kwa kuwa zinaharibu jina zuri la Tanzania.
Masauni ambaye alikuwa na Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Hamid Masoud Jongo katika sherehe hiyo, licha ya kuwashukuru waandaaji wa tukio hilo kwa kumualika, pia aliwahasa Waislam nchini wawe na umoja, wapendane na waache kulalamika kwa kuwa mafundisho ya dini hiyo yanaelekeza mambo mema ambayo kila Muislam anatakiwa kuyafuata.

Friday, December 16, 2016

WAZIRI MUHONGO AKUTANA NA WAINGEREZA WENYE NIA YA KUZALISHA UMEME NCHINI

 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia), akiwasikiliza Viongozi Waandamizi kutoka Kampuni ya ‘Solar Securities’ ya Uingereza, Nicholas Richardson ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji (katikati) na Manoli Yannaghas – Mkurugenzi (kushoto); walipomtembelea ofisini kwake hivi karibuni kwa lengo la kuonesha nia yao ya kuwekeza kwenye sekta ya umeme nchini.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akisisitiza jambo katika kikao baina yake na Ujumbe kutoka Kampuni inayojishughulisha na masuala ya nishati mbadala kutoka Uingereza, ‘Solar Securities (hawapo pichani)
 Mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Masele (kulia), akifurahia jambo wakati wa kikao baina ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Ujumbe kutoka Kampuni inayojishughulisha na masuala ya nishati mbadala kutoka Uingereza, ‘Solar Securities (hawapo pichani). Masele ni mshirika wa Kampuni hiyo. Kulia ni Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Nishati Mbadala, Jacob Mayala.

Kutoka Kulia ni Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Nishati Mbadala, Jacob Mayala, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Solar Securities Nicholas Richardson, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Manoli Yannaghas, Mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele na Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Umeme, Mhandisi Innocent Luoga, wakiwa katika kikao ambacho Ujumbe kutoka Kampuni husika ulionesha nia kuwekeza kwenye sekta ya nishati nchini.



Kutoka Kulia ni Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Nishati Mbadala, Jacob Mayala, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Solar Securities Nicholas Richardson, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Manoli Yannaghas, Mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele na Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Umeme, Mhandisi Innocent Luoga, wakiwa katika kikao ambacho Ujumbe kutoka Kampuni husika ulionesha nia kuwekeza kwenye sekta ya nishati nchini.



Na Veronica Simba
Ujumbe kutoka Kampuni inayojishughulisha na masuala ya nishati mbadala kutoka Uingereza, ‘Solar Securities’, umemtembelea Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ofisini kwake na kufanya mazungumzo kuhusu nia yao ya kuwekeza kwenye sekta ya nishati hapa nchini.
Viongozi waandamizi kutoka Kampuni hiyo, Nicholas Richardson (Mkurugenzi Mtendaji) na Manoli Yannaghas (Mkurugenzi), walimweleza Waziri Muhongo kuwa lengo lao ni kuwekeza nchini kwa kuzalisha umeme wa jua.
Akitoa mwongozo wa nia iliyowasilishwa na Ujumbe huo, Profesa Muhongo aliwaeleza kuwa, Serikali imeanzisha utaratibu mpya wa uwekezaji nchini hususan katika sekta ya nishati, ambapo wawekezaji walioonesha nia ya kuwekeza watashindanishwa kwa uwazi na wale watakaokidhi vigezo ndiyo watapata fursa ya kuwekeza.
Alisema kuwa, kwa kuanzia, mwongozo wa utaratibu huo mpya kwa upande wa sekta ndogo ya gesi na mafuta uko mbioni kukamilika na utafuatiwa na miongozo husika kwa sekta nyingine za nishati.
Alitumia fursa hiyo kuwaalika wawekezaji wote wenye nia ya kuwekeza katika sekta husika kuutumia ipasavyo mwongozo husika pindi utakapokuwa tayari ambapo alisema utasambazwa duniani kote ili waweze kuelewa vyema fursa za uwekezaji katika sekta hiyo.
 Vilevile, alieleza kuwa, Serikali hususan wizara yake, imefanya mabadiliko katika utaratibu wa majadiliano baina yake na wawekezaji wanaoonesha nia za kuwekeza nchini, ambapo sasa majadiliano yatatumia muda mfupi tofauti na ilivyokuwa zamani ili kuleta tija kwa pande zote mbili.
“Awali, tulikuwa tukipoteza muda mrefu katika majadiliano. Sasa majadiliano yanachukua muda mfupi na kufikia makubaliano,” alisisitiza.
Profesa Muhongo alimwagiza Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Umeme, Mhandisi Innocent Luoga, kufuata utaratibu huo wenye kutumia muda mfupi kwa kuandaa kikao kitakachohusisha pande zote likiwemo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na wataalam kutoka wizarani, kujadili maombi yaliyowasilishwa na Kampuni hiyo ili kufikia muafaka ndani ya muda mfupi.

SIKU YA KWANZA YA SAFARI YA WANAHABARI NA ASKARI WA JESHI LA ULINZI (JWTZ) KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KUSHEREHEKEA MIAKA 55 YA UHURU WA TANZANIA BARA

Waandishi wa Habari walioshiriki changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara wakinyanyua kuashiria kuanza safari hiyo atika lango la Marangu.
Safari ya kupanda ikaanza katika lango la Marangu majira ya saa 5 asubuhi kila mmoja akiwa na nguvu za kutosha na shauku ya kutzama madhari ya Mlima Kilimanjaro ambao siku ya kwanza safari inaanza kwa kupita katika msitu mnene.
Wapandaji waliokuwa wamevalia nguo za kuzuia baraidi mapema wakati safari ya kupanda mlima inaanza baadae kidogo kidogo walilazimika kuzipunguza kwa sababu pindi unapotembea joto la mwili pia huongezeka.
Safari ya kupanda mlima kwa kundi hili la Wanahabari na Askari wa jeshi la Ulinzi (JWTZ) wakiongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu,George Waitara lilikuwa pia na ulinzi wa kutosha. 
Safari ya kupanda vilima vidogo ndani ya Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro iliendelea.
Maeneo mengine yalikuwa ni ya Madaraja na Mito.
Hatimaye safari kafika eneo la Kisambioni ikiwa ni nusu ya safari ya kuelekea katika kituo cha Mandara ,eneo ambalo hutumika kwa ajili ya kupata chakula.
Baadae safari ya kuelekea kituo cha Mnadara ikaendeleo.
Maeneo mengine Washiriki walilazimika kupumzika kwa ajili ya kupata nguvu mpya ya kuendelea na safari.
Majira ya saa 12 jioni hatimaye Safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa siku ya kwanza ikafika katika kituo cha Mandara na washiriki wakapata nafasi ya kupata picha ya pamoja na kupumzika kwa ajili ya siku ya pili kuendele na safari ya kwenda kituo cha Horombo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyekuwa katika safari hiyo.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA HALMSHAURI YA NGORONGORO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na watumishi wa   serikali na Halmashauri  ya Wilaya ya  Ngorongoro uliopo  kwenye ukumbi wa halmashauri  hiyo iliyopo Wasso  Desemba 15, 2016.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 1A7872, 1a7873,   Baadhi ya watumishi wa   serikali na  halmashauri   ya wilaya ya  Ngorongoro    wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo uliopo Wasso wilayani Ngorongoro Desemba 15, 2016. (Picha  na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...