Monday, December 05, 2016

WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA HOSPITALI YA MKOA WA ARUSHA, AANZA ZIARA YA MONDULI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waganga na Wauguzi wa hospitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru wakati al;ipoitembelea Desemba 4, 2016.
Mmoja wa wauguzi katika hospitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru akideki katika wodi ya wazazi wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotembela wodi hiyo akiwa katika ziara ya mkoa wa Arusha Desemba 4, 2016.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwafariji wanawake waliolazwa kwenye wodi ya wazazi katika hospitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru wakati alipotembelea wodi hiyo na kukuta wakiwa wamelala watatu kwenye kitanda kimoja Desemba 4, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akielekea kwenye wodi ya wazazi katika hospitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru wakati a;lipoitembelea Desemba 4, 2016. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Monduli baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa wilaya hiyo kuanza ziara ya siku moja ya kazi wilayani humo Desemba 4, 2016. 

Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Monduli baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Monduli kuanza ziara ya kazi wilayani humo Desemba 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...