Mkurugenzi wa MM Connects Ltd, Emmanuel Makaki( kushoto) akifurahia tuzo yake ya ubora katika Mauzo ya Rejareja iliyotolewa na Vodacom Tanzania, mara baada ya kukabidhiwa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshangilia ni timu ya wafanyakazi wa kampuni hiyo kitengo cha Mauzo ya Rejareja ambao walitembeklea duka hilo lililopo Kariakoo jijini.
Mkurugenzi wa MM Connects Ltd, Emmanuel Makaki (kushoto) akipokea tuzo yake ya ubora katika Mauzo ya Rejareja iliyotolewa na Vodacom Tanzania, mara baada ya kukabidhiwa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wafanyakazi wa Vodacom kitengo cha mauzo walipotembelea duka la kampuni hiyo lililopo Kariakoo. Anayekabidhi tuzo hiyo ni Mkuu wa kitengo cha Mauzo ya Rejareja wa kampuni hiyo,Brigita Stephen.
Mkurugenzi wa MM Connects Ltd, Emmanuel Makaki (kushoto) akiwakaribisha wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kitengo cha Mauzo ya Rejareja wakati waliotembelea duka lake la Vodacom Kariakoo jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mkuu wa kitengo cha Mauzo ya Rejareja wa Vodacom Tanzania, Brigita Stephen.
Wateja wa Vodacom Tanzania, wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa kitengo cha Mauzo ya Rejareja wa Vodacom Tanzania, Brigita Stephen (wa pili kushoto) wakati yeye na timu ya wafanyakazi wenzake wa kitengo hicho walipotemvbelea duka la Vodacom Samora Avenue jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Deltaafrica, Mohamme Araz (kulia) na wafanyakazi wenzake wakifurahia tuzo yao ya ubora katika Mauzo ya Rejareja iliyotolewa na Vodacom Tanzania, wakati wafanyakazi wa kitengo cha Mauzo ya Rejareja walipotemblea duka lake la Vodacom Samora Avenue jijini Dar esSalaam.
Mkuu wa kitengo cha Mauzo ya Rejareja wa Vodacom Tanzania, Brigita Stephen (kushoto) akimkabidhi mteja wa kampuni hiyo, John Kyashama, wakati timu ya wafanyakazi wa wa kitengo hicho walipotemvbelea duka la Vodacom la Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Akiwa mwenye furaha ni mteja wa Vodacom Tanzania, John Kyashama (kulia) baada ya kukabidhiwa zawadi na Mkuu wa kitengo cha Mauzo ya Rejareja wa Vodacom Tanzania, Brigita Stephen, wakati timu ya wafanyakazi wa wa kitengo hicho walipotembelea duka la Vodacom la Mlimani City jijini Dar es Salaam .
No comments:
Post a Comment