Tuesday, August 16, 2016

WATU WATATU WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUGUSHI VYARAKA MBALIMBALI ZA IDARA YA AFYA

 Baadhi ya vyeti vya kugushi vilivyokamatwa
Mihuri iliyokamatwa katika tukio hilo. 
 Kompyuta mpakato,Laptop,Printer na Scarner pamoja na mihuli  ni vifaa vilivyokamatwa katika Steshanari hiyo.

 RPC MTUI akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya tukio hilo
 Baadhi ya Wanahabari wakiwa ofisini kwa RPC Mtui wakipata maelezo kuhusiana na tukio hilo.


Na,Abel Daud-
KIGOMA,

Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma kwa kushirikiana na wataalamu kutoka baraza la Famasia linawashikiria watu watano kwa tuhuma za kugushi vyeti mbalimbali vya idara ya afya, ambavyo vinasadikika kutumiwa kufanya kazi katika sekta ya afya.

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake mapema leo hii Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma Kamishina Msaidizi wa Polisi FERDINAND MTUI, amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao ambapo amebainisha kuwa miongoni mwa watuhumiwa hao ni pamoja na MGENI NYABUZOKI mzanaki mwenye umri wa miaka 52 ambaye ni askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania mkazi wa mlole ambaye ndiye mmiliki wa stationary inayotumika kutengeneza vyeti hivyo vya kugushi.

Kamanda Mtui ameongeza kuwa wengine walio kamatwa katika tukio hilo ni pamoja na Dikson Mshahilizi (47),ambaye ni muuguzi katika Hospital ya rufaa Maweni,mkazi wa Air pot,Zawadi James  (42) muuguzi katika kituo cha afya Ujiji, mkazi wa Kazegunga Stephano Erasto (18) mkazi wa mlole na mwanafunzi wa shule ya sekondary mlole pamoja na Jonson Nyabuzoki ,ambaye ni mwanafunzi wa shule ya sekondari Mlole na mtaalamu wa kutumia Kompyuta mpakato katika kutengeneza vyeti hivyo.

Kwa upande wake Mratibu wa maduka ya dawa muhimu baraza la Famasi Taifa Domick Mfoi ,amesema kuwa kutokana na huduma inayotolewa na watu ambao hawakupitia mafunzo katika sekta ya afya inapelekea madhara makubwa ya vifo kwa umma,kwani huduma watakayoipata haitaendana na huduma sitahiki kwa mgonjwa.

Ameongeza kuwa katika kudhibiti hali hiyo msako na uchunguzi wa kina utaendelea kufanyika ili kubaini kama kuna watu wengine wanaofanya kazi katika vituo mbalimbali vya afya hapa nchini.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...