Wednesday, August 10, 2016

MAKAMU WA RAIS AIPONGEZA NHIF, AVUTIWA NA KAZI ZAKE

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu ameupongeza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kazi nzuri na kubwa ya upimaji wa afya za wananchi iliyofanyika katika maonesho ya Kitaifa ya Nane Nane mkoani Lindi.

Pongezi hizo alizitoa wakati alipotembelea banda hilo katika kilele cha maonesho hayo ambapo alisema kuwa kazi inayofanywa na Mfuko inawasaidia wananchi kutambua afya zao lakini pia elimu ya kuepukana na maradhi yasiyoambukizwa.

“NHIF nawapongeza sana kwa kazi kubwa mliyoifanya mahali hapa, nimepata taarifa zenu kwamba mnapima afya za wananchi bure...hongereni sana na fursa hii iwafikie na wengine” alisema Makamu wa Rais.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bernard Konga akitoa maelezo ya huduma zilizotolewa na Mfuko katika maonesho ya Nane Nane mkoani Lindi kwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu wakati alipotembelea banda hilo. Kati kati ni Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Mama Anne Makinda. 

Katika maonesho hayo, Mfuko ulitoa huduma mbali zikiwemo za elimu ya namna ya kunufaika na huduma za Mfuko, usajili wa wanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii, upimaji wa afya kwa wananchi ikiwemo saratani ya matiti, hali lishe, sukari na shinikizo la damu pamoja na elimu ya kuepukana na magonjwa hayo.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Mama Anne Makinda alitoa mwito kwa Watanzania kuhakikisha wanatumia fursa zinazotolewa na Mfuko ikiwemo kujiunga na huduma za Mfuko ili wawe na uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wowote.
Meneja wa Mkoa wa Lindi Fortunata Raymond akitoa maelezo ya huduma kwa Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Mama Anne Makinda alipotembelea kuona huduma zinazotolewa. 

Alisema kuwa Mfuko umejipanga kuhakikisha unahudumia idadi kubwa ya Watanzania hivyo ni vyema wakachangamkia huduma zilizopo kwa kuwa zinagusa makundi mbalimbali yakiwemo ya Watoto, wanafunzi, watu binafsi, wajasiliamali na makundi mengine.

“Nawahamasisha tu Watanzania kujiunga na huduma za Mfuko huu kwani zimezingatia mahitaji ya kila Mtanzania na huu ndio mpango wa Serikali wa kuhakikisha kila mwananchi anakuwa kwenye Mfumo wa Bima ya Afya,” alisema Mama Makinda.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko Bw. Bernard Konga aliwahakikishia Watanzania kuwa, Mfuko uko imara na umejipanga kutoa huduma bora ambazo zitakidhi mahitaji yao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene akizungumza na Meneja wa NHIF Lindi baada ya kuona huduma zinazotolewa na Mfuko huo. 

Alisema kuwa Mfuko unaendelea kufanya maboresho mbalimbali katika huduma zake kwa kuzingatia makundi mbalimbali ya wananchi ili kuwezesha mpango wa Serikali wa afya bora kwa wote.

“Tunaendelea na kasi ya utoaji wa elimu ya huduma zetu kwa wananchi na kwa sasa huduma zetu zipo mpaka ngazi ya chini kabisa kwa kuwa tuna ofisi za Mfuko kila mkoa zinazofanya kazi ya kuwafikia wananchi mpaka ngazi ya kaya,” alisema Bw. Konga.
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dr, Charles Tizeba akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa NHIF, Bernard Konga katika banda la Mfuko.
Wananchi wakiwa katika banda la Mfuko kwa ajili ya kupata huduma za elimu na upimaji wa afya zao.
Maofisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakiwajibika kuwahudumia wananchi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene akipima uzito katika banda la NHIF ambalo lilitoa huduma mbalimbali.
Meneja wa NHIF Mkoa wa Lindi akitoa elimu kwa wananchi.
Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Mama Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mfuko baada ya kumalizika kwa maonesho ya Kitaifa Nane Nane.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...