Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimuelekeza jambo Sheikh Mkuu wa Tanzania,Mufti,Abubakary Zubeir namna ujenzi wa ghorofa hilo utakavyokuwa,mara baada ya kukabidhiwa mchoro wa jengo hilo litakalogharimu zaidi bilioni tano,kulia ni Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam , Alhaji Mussa Salum.PICHA NA MICHUZI JR.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pampja na Sheikh Mkuu wa Tanzania,Mufti,Abubakary Zubeir wakitazama mchoro wa ramani wenye ghorofa tatu,ambapo ujenzi wake utagharimu zaidi ya shilingi bilioni tano,ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ujenzi wa jengo jipya la Baraza hilo.
,kulia ni Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam , Alhaji Mussa Salum .
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pamoja naSheikh Mkuu wa Tanzania,Mufti wakionesha mchoro wa ramani wenye ghorofa tatu kwa wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo fupi iliyofanyika jijini Dar mapema leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizaungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi mchoro wa ramani wenye ghorofa tatu kwa uongozi wa Baraza Kuu la Waislamu nchini,BAKWATA ikiwa ni maandalizi ya ujenzi wa jengo jipya la Baraza hilo.
Sheikh Mkuu wa Tanzania,Mufti Abubakary Zubeir akifafanua jambo mbele ya wageni waalikwa,kabla ya kukabidhiwa mchoro wa ramani wenye ghorofa tatu kwa uongozi wa Baraza Kuu la Waislamu nchini,BAKWATA ikiwa ni maandalizi ya ujenzi wa jengo jipya la Baraza hilo.
Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam , Alhaji Mussa Salum akimkaribisha Sheikh Mkuu wa Tanzania,Mufti Abubakary Zubeir mbele ya wageni waalikwa,kabla ya kukabidhiwa mchoro wa ramani wenye ghorofa tatu kwa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar ES Salaam,Mh Paul Makonda.
Baadhi ya Wageni waalikwa wakifuatilia yalikuwa yakijiri kwenye hafla hiyo fupi.
Baadhi ya Wageni waalikwa wakifuatilia yalikuwa yakijiri kwenye hafla hiyo fupi
Na Bakari Issa Madjeshi, Globu ya Jamii
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekabidhi mchoro wa ramani wenye ghorofa tatu kwa uongozi wa Baraza Kuu la Waislamu nchini,BAKWATA ikiwa ni maandalizi ya ujenzi wa jengo jipya la Baraza hilo.
Pamoja na kukabidhi ramani hiyo, Mkuu wa Mkoa huyo amesema jengo hilo litagharimu kiasi cha fedha 5, 080, 155, 600 ili kukamilika. Pia amesema jengo hilo mpaka kukamilika litakuwa la kipee na kupewa hadhi kama Taasisi kubwa ya Kiislamu na kusisitiza ujenzi wa jengo hilo hautazidi miezi 14.
Amesema amekabidhi mchoro huo kutokana na kutambua na kuthamini umuhimu wa BAKWATA katika Taifa pamoja na kuwataka Waislamu na wasiokuwa waislamu kujitokeza katika kutoa misaada hiyo. Pia ametoa shukrani kwa waislamu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kushereheka nao pamoja katika Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ambapo amesema mwezi huo ndio uliokuwa chimbumbo la ujenzi wa jengo hilo la BAKWATA.
Amesema amekabidhi mchoro huo kutokana na kutambua na kuthamini umuhimu wa BAKWATA katika Taifa pamoja na kuwataka Waislamu na wasiokuwa waislamu kujitokeza katika kutoa misaada hiyo. Pia ametoa shukrani kwa waislamu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kushereheka nao pamoja katika Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ambapo amesema mwezi huo ndio uliokuwa chimbumbo la ujenzi wa jengo hilo la BAKWATA.
Akitoa shukrani zake kwa Mkuu wa Mkoa huyo, Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abuubakari Zuberi amewataka Waislamu kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa huyo ikiwa kuwataka kuamini ya kuwa na haki ya kupokea misaada kama Waislamu.
No comments:
Post a Comment