Tuesday, August 16, 2016

BENKI YA DCB WATOA MSAADA WA MADAWATI 100 KATIKA SHULE MPYA YA MSINGI YA LUBAKAYA JIJINI DAR ES SALAAM

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akikabidhiwa madawati na Mkuu wa kukabiliana na majanga wa Benki ya DCB, Kulwa Deteba jijini Dar es Salaam jana, madawati ambayo yatapelekwa katika shule Mpya ya Lubakaya iliyopo Kata ya Zingiziwa jijini Dar es Salaam.
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akikabidhiwa madawati na Mkuu wa kukabiliana na majanga wa Benki ya DCB, Kulwa Deteba wakimkabidhi madawati Mkuu wa Shule ya Msingi, Lubakaya (Katikati) jijini Dar es Salaam jana. Katika Hafla iliyofanyika katika Shule ya Msingi Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko na Mkuu wa kukabiliana na majanga wa Benki ya DCB, Kulwa Deteba wakiwa wamekaa kwenye madawati mara baada ya kukabidhi madawati kwenye shule ya Msingi Lubakaya iliyopo kata ya Zingiziwa  jijini Dar es Salaam jana.
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko madawati na Mkuu wa kukabiliana na majanga wa Benki ya DCB, Kulwa Deteba wakiwa wamekaa kwenye madawati na wanafunzi wa shule ya Msingi Mnazi Mmoja wakiwawakilishi wanafunzi wa shule ya Msingi Lubakaya iliyopo kata ya Zingiziwa  jijini Dar es Salaam jana.
   Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko na Mkuu wa kukabiliana na majanga wa Benki ya DCB, Kulwa Deteba wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa shule na wa serikali katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi madawati 100 kutoka benki ya DCB jijini Dar es Salaam jana.
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akizungumza katika Hafla Fupi ya Kuwakabidhi madawati 100 ya  shule ya Msingi Lubakaya iliyopo kata ya Zingiziwa  jijini Dar es Salaam jana.

Mkuu wa shule ya Msingi Lubakaya iliyopo kata ya Zingiziwa, Said Chitumba akiwashukuru Benki ya DCB akiwashukuru benki ya DCB mara baada ya kukabidhiwa madawati 100. 

Benki ya DCB COMMERCIAL imetoa madawati 100 kwa shule ya msingi Lubakaya iliyopo Kata ya Zingiziwa jijini Dar es Salaam, ikiwa ni ukamilishaji wa ahadi yake ya kuchangia madawati 300 kwa shule za manispaa tatu za mkoa wa Dar es Salaam.

Mkuu wa kukabiliana na majanga wa Benki ya DCB, Kulwa Deteba akizungumza na waanafunzi pamoja na viongozi mbalimbali jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa benki ya DCB imeguswa na tatizo la ukosefu wa madawati kwa shule ya msingi hapa nchini.

Amesema kuwa bodi na uongozi wa benki ya DCB inaunga mkono juhudi za serikali katika kukabiliana na tatizo la madawati hapa nchini inetoa madawati 100 katika shule ya Msingi Lubakaya jijini Dar es Salaam jana.

Nae Mkuu wa shule ya Msingi Lubakaya iliyopo kata ya Zingiziwa, Said Chitumba amewashukueu benki ya DCB kwa mchango wao kwa kutoa madawati 100 katika shule hiyo ikiwa shule hiyo inavyumba 16 vya madarasa na sasa wanaukosefu wa madawati 300.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...