TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUHUSU TUHUMA ZA KUKAMATWA KWA BVR MACHINE
Tume ya Taifa ya uchaguzi inapenda kutoa taarifa kwa vyombo vya Habari na Umma kwa ujumla kuwa Tume ilipokea taarifa toka kwa mmoja wa viongozi wa CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) kuwa kuna uandikishaji wa wapiga kura unaofanyika katika eneo la viwanda Mikocheni.
Baada ya Tume kupata taarifa hiyo, kwa kushirikiana na Viongozi wa CHADEMA ilichukuwa jukumu la kufuatilia suala hilo ili kubaini ukweli na kuchukuwa hatua stahiki kama kungekuwa na zoezi hilo ambalo ni kinyume cha za sheria za Uchaguzi.
Hata hivyo, baada ya Uongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na uongozi wa CHADEMA kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kufuatilia suala hilo katika kiwanda cha MM Intergrated Steel Mills ilibainika kuwa vifaa hivyo vilikuwa vinatumika kwa minajili ya kuandaa kanzi data (data base) ya wafanyakazi wa kiwanda hicho ili kuwa na taarifa sahihi za wafanyakazi wao.
No comments:
Post a Comment