Friday, October 02, 2015

NMB YAJIVUNIA MIAKA 10 YA MAFANIKIO

nmb (1)nmb (2)
Mkurugenzi wa NMB - Ineke Bussemaker (katikati) akizungumza na Wajumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (Tanzania Editors Forum) jijini Dar es Salaam jana kuhusu maadhimisho ya miaka 10 ya benki hiyo tangu ilipobinafsishwa na hatua ilizopiga katika maendeleo ya benki.
nmb (3)
Wajumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (Tanzania Editors Forum) wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (katikati) jijini Dar es Salaam jana kuhusu maadhimisho ya miaka 10 ya benki hiyo tangu ilipobinafsishwa na hatua ilizopiga katika maendeleo ya benki.
nmb (4)
Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania jana kwenye makao makuu ya NMB.
nmb (5)
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kushoto) na Wajumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (Tanzania Editors Forum) wakiangalia filamu fupi kuhusu maadhimisho ya miaka 10 ya benki ya NMB tangu ilipobinafsishwa na hatua ilizopiga katika maendeleo yake jijini Dar es Salaam jana.
nmb (6)
Mkurugenzi wa NMB – Ineke Bussemaker akisalimiana na Mhariri na Mmiliki wa ABM FM ya Dodoma – Abdallah Majura kwenye mkutano kati ya NMB na Jukwaa la Wahariri.
nmb (7)Mratibu wa Jukwaa la Wahariri – Prisca Kabendera akielezea kuhusu Jukwaa la wahariri na shughuli inazofanya.

Benki ya NMB jana ilianza maadhimisho ya miaka 10 tangu kubinafsishwa huku ikiweka bayana mafanikio makubwa iliyoyapata ikiwemo kuongeza matawi kutoka chini ya 100 miaka 10 iliyopita mpaka matawi 173 leo hii, kutoka kutokuwa na ATM mpaka ATM zaidi ya 600 na wateja kufikia zaidi ya milioni 2 kutoka laki 6 miaka 10 iliyopita.

NMB pia imefanikiwa kuwa na matawi katika kila wilaya nchini. Hii inaonesha ni jinsi gani Benki imekuwa kwa kasi na kuwa benki namba moja kwa ukubwa na faida kuliko benki nyingine yoyote nchini Tanzania.

Kwa miaka 10 pia NMB imetumia zaidi ya shilingi Bilioni 7 kusaidia shughuli za maendeleo ya jamii ikiwemo kusaidia madawati mashuleni, vifaa vya hospitali katika hospitali mbalimbali za serikali huku ikichangia kuongeza ufanisi wa utoaji huduma katika sekta ya afya na elimu.

NMB Pia imechangia zaidi ya Bilioni 365 ndani ya miaka 5 tu fedha ambayo imechangia sana kwenye bajeti ya serikali na hivyo kutumika kwa maendeleo ya watanzania. Huo ni mchango mkubwa kuliko benki yoyote nchini. 

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...