Friday, October 09, 2015

MGOMBEA UBUNGE KUPITIA ACT WAZALENDO ESTOMIH MALLA AFARIKI


unnamedmmMgombea ubunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya ACT WAZALENDO Ndugu Estomih Malla amefariki dunia usiku wa leo saa saba Oktoba 9, 2015 katika hospitali ya KCMC Moshi.
Ndugu Malla alipelekwa KCMC jana mchana kutokea Hospitali ya St. Thomas iliyopo Arusha mjini baada ya kulazwa hapo kwa siku mbili kwa sababu ya kupata tatizo la shinikizo la juu la damu.
Hali hiyo ilimtokea siku ya tarehe 6/10/2015 mara baada ya kumalizika mkutano wa kampeni uliokuwa unafanyika Ngaramtoni,ambapo alilalamika kusikia kizunguzungu na baadae kukimbizwa hospital ya St Thomas ambapo madaktari wa pale walisema ndugu Malla anasumbuliwa na uchovu na hivyo anatakiwa kupumzika kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Chama Cha ACT Wazalendo, Abdallah Khamis, ameithibitishia JamiiForums kutokea kwa kifo hicho na kwamba marehemu alifariki usiku huu wa Oktoba 9, 2015 saa Saba usiku.
Amesema taarifa zaidi zitatolewa baadae baada ya uongozi wa chama hicho kufanya mawasiliano na viongozi waliopo mkoani Arusha.
Sisi sote ni wa mola na hakika kwake sote tutarejea.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...